Jumatano, 31 Mei 2017

CAG AITUNUKU HATI SAFI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI


Posted by Esta Malibiche on MEI 31 in NEWS

f
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Profesa Riziki Shemdoe Picha kutoka maktaba ya Kitengo cha habari.

Na Afisa Habari Mufindi


Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serilkali nchini CAG ameitunuku hati safi ya hesabu na matumizi sahihi ya Fedha za Umma Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha na matumizi yaliyozingatia taratibu, Sheria na kanuni za fedha  za Umma  kwa mwaka wa Fedha wa 2015 – 2016.

Akizungumza mapema leo hii na mtandao huu wa habari A fisa habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimmyake Mwakapiso, amesema kuwa CAG ametunuku hati hiyo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi wa kawaida wa kila mwaka kwa mujibu wa sheria za fedha zinazompa mamlaka ya kukagua hesabu za mamlaka za serikali za Mitaa.

Mwakapiso, ametanabaisha baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa kwenye ukaguzi huo, kuwa ni pamoja na ujenzi wa miradi inayoendana na thamani ya fedha zilizotumika, uzingatiaji wa  sharia na taratibu za Manunuzi ya tenda, matumizi mazuri ya fedha za miradi ya maendeleo na zile za zatumizi ya kawaida sanjari na uandaaji wa taarifa za fedha unaozingatia viwango vya kimataifa( IPSAS)
""Huu ni mwaka wa 05 mfululizo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi inapata hati safi ya CAG. 
"" Alisema Mwakapiso
Aidha alisema  kuwa kwa mujibu wa kanuni  za ukaguzi, Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali mara baada ya kukamilisha ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha husika, anaweza kutoa moja kati ya hati zifuatazo Hati safi, Hati yenye mashaka au Hati chafu.

0 maoni:

Chapisha Maoni