Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumatano, 31 Mei 2017

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA PHILEMON NDESAMBURO

Posted by Esta Malibiche on MEI 31,2017  IN NEWS

MWIGULU NCHEMBA MGENI RASMI UZINDUZI WA NYIMBO ZA INJILI MAFINGA MKOANI IRINGA

Posted by Esta Malibiche on MEI 31,2017


CAG AITUNUKU HATI SAFI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI


Posted by Esta Malibiche on MEI 31 in NEWS
f
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Profesa Riziki Shemdoe Picha kutoka maktaba ya Kitengo cha habari.

Na Afisa Habari Mufindi


Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serilkali nchini CAG ameitunuku hati safi ya hesabu na matumizi sahihi ya Fedha za Umma Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha na matumizi yaliyozingatia taratibu, Sheria na kanuni za fedha  za Umma  kwa mwaka wa Fedha wa 2015 – 2016.

Akizungumza mapema leo hii na mtandao huu wa habari A fisa habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimmyake Mwakapiso, amesema kuwa CAG ametunuku hati hiyo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi wa kawaida wa kila mwaka kwa mujibu wa sheria za fedha zinazompa mamlaka ya kukagua hesabu za mamlaka za serikali za Mitaa.

Mwakapiso, ametanabaisha baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa kwenye ukaguzi huo, kuwa ni pamoja na ujenzi wa miradi inayoendana na thamani ya fedha zilizotumika, uzingatiaji wa  sharia na taratibu za Manunuzi ya tenda, matumizi mazuri ya fedha za miradi ya maendeleo na zile za zatumizi ya kawaida sanjari na uandaaji wa taarifa za fedha unaozingatia viwango vya kimataifa( IPSAS)
""Huu ni mwaka wa 05 mfululizo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi inapata hati safi ya CAG. 
"" Alisema Mwakapiso
Aidha alisema  kuwa kwa mujibu wa kanuni  za ukaguzi, Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali mara baada ya kukamilisha ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha husika, anaweza kutoa moja kati ya hati zifuatazo Hati safi, Hati yenye mashaka au Hati chafu.

Alhamisi, 18 Mei 2017

IKUNGI WAANZISHA MFUKO WA ELIMU ILI KUONDOA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO.

Posted by Esta Malibiche on MEI 18,2017 IN NEWS

Mkuu wa Wilaya Ikungi Miraji Mtaturu katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya ns viongozi wa halmashauri baada ya kumaliza kikao nao. 
Mjumbe mwakilishi wa madhehebu ya dini sheikh Salum Ngaa akichangia hoja wakati wa kikao kilichoongozwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu pichani wakiwa na wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya. 
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Haika Massawe akichangia hoja wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya. 
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akitoa maelekezo wakati alipokutana na kamati ya mfuko wa elimu ya wilaya. 

…………………………….. 

MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu amekutana na kamati ya mfuko wa elimu wilaya na kuwaomba kuwa wazalendo katika kutafuta njia za kutatua changamoto za elimu wilayani humo. 

Mfuko huo umeundwa baada ya uanzishwaji wake kuridhiwa na kikao cha baraza la madiwani kilichoketi hivi karibuni. 

Akizungumza katika kikao cha kuwapatia majukumu yao Mtaturu amesema mfuko huo utakuwa na jukumu la kuratibu masuala yote yatakayosaidia kuboresha utoaji wa elimu katika shule za msingi na sekondari. 

“nawapongezeni kwa heshima mliyopewa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa kamati hii,naimani kuwa mtafanya kazi kwa uzalendo mkubwa ili matunda ya uwepo wenu yaonekane kwa kuitoa elimu yetu hapa ilipo na kuipeleka mbali zaidi,”alisema Mtaturu. 

Alisema wakifanikiwa kuondoa changamoto zilizopo watakuwa wameboresha mazingira ya utoaji elimu na kuongeza ufaulu wa watoto jambo ambalo waliazimia walipokutana wadau wa elimu. 

Akitoa taarifa kwenye kikao hicho katibu wa mfuko huo Salum Athuman alisema ili kutatua changamoto za elimu zilizopo katika wilaya hiyo zinahitajika jumla ya shilingi bilioni 26 kwa ajili ya miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,nyumba za walimu,maabara,matundu ya vyoo na mabweni. 

Aidha mwenyekiti wa kamati hiyo Hamis Maulid kwa niaba ya wajumbe alisema wamepokea kazi hiyo na wataifanya kwa uadilifu mkubwa ili malengo yaliyokusudiwa yatimie. 

Disemba mwaka jana mkuu wa wilaya huyo alikutana na wadau wa elimu ili kubaini changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ambapo waliweka maazimio yapatayo 37 yenyek ulenga kuboresha elimu wilayani humo na moja ya mkakati waliouweka ndio umezaa wazo la kuanzishwa kwa mfuko huo wenye wajumbe 15 ambao wameanza kazi rasmi ili kutafuta njia ya kutatua changamoto za elimu wilayani humo. 

Wilaya hiyo ina jumla ya shule za sekondari 30 ikiwemo za kidato cha sita 3 na shule za msingi 108.

MABASI YANAYOBEBA WANAFUNZI MKOANI SINGIDA YAKAGULIWA.

Posted by Esta Malibiche on MEI 18,2017 IN NEWS

Askari wa usalama barabarani mkoani Singida, E.8763. Sgt. Benes Lucas akikagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi mjini hapa jana.
Baadhi ya mabasi kati ya 20 yanayotumika kusafirisha wanafunzi Mkoani Singida yakifanyiwa ugazi na askari usalama barabarani kwa lengo la kujiridhisha ubora wake.
RTO Mkoa wa Singida Mrakibu wa polisi Peter Raphael Majira akitoa taarifa ya zoezi la ukaguzi wa mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi kwa lengo la kukagua ubora na pia kuwakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo juu ya sheria za usalama barabarani.


MAELEZO YA PICHA.

…………………..

Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Singida limeanzisha zoezi kambambe la kukagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi huku likisisitiza kuwa zoezi hilo kuwa endelevu.

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida, RTO Mrakibu wa Polisi Peter Raphael Majira, amesema zoezi hilo lililoanza jana litaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Singida.

Amesema lengo ni kuhakikisha mabasi hayo yanakidhi mahitaji yote ya sheria za usalama barabani, wakati wote yanapokuwa barabarani.

Amesema pia wanatoa elimu na wanawakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo, juu ya wajibu wao na umuhimu wa kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani. 


Aidha RTO Peter amesema wanawakumbusha madereva kujenga utamaduni wa kuwa na tahadhari zaidi na kitendo hicho kitapunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.

Pia ametumia fursa hiyo kuwataka wenye watoto wanaotumia mabasi hayo wahakikishe mtoto anakaa kwenye kiti chake na si kuchangia kiti.

“Mzazi/mlezi usikubali kabisa mwanao achangie kiti, umelipitia kiti kwa nini achangie na wanafunzi mwingine. Na ninyi wamiliki wa mabasi haya kama kuna hafla wanafunzi wanakwenda kuhudhuria iwapo wamejaa (yaani kila mwanafunzi ana kiti chake), peleka hao waliopata viti halafu urudie wengine” amesisitiza mrakibu Peter.

Kwa upande wao madereva hao wamelipongeza jeshi la polisi mkoa wa Singida kwa kuendesha ukaguzi huo na kuwakumbusha juu ya sheria za usalama barabarani.

Mmoja wa madereva wa mabasi ya wanafunzi Mkoani Singida Pyuza Gyumi amesema kwenye mafunzo hayo ya muda mfupi wameagizwa kwamba ni marufuku wanafunzi kuchangia kiti kimoja kwa madai ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za usalama barabarani.

“Tumekumbushwa kwamba wakati tukiwa barabarani tuwe makini wakati wote wa kuendesha na tuwe na utulivu wa hali ya juu. Pia tumekumbushwa kuwa makini wakati tunavusha kwa miguu wanafunzi ng’ambo yingine ya barabara. Kwa ujumla binadamu anatakiwa mara kwa mara akumbushwe wajibu wake hii itasaidia kufanya kazi zetu kwa ufanisi”, amesema.

Aidha amesema jeshi la polisi kuwakutanisha na waajiri wao itasaidia kupunguza kero mbalimbali zinazowakabili kati yao na waajiri wao.

“Kuna wakati tunashindwa kuelewana na matajiri wetu wakati wanapotulazimisha kutenda mambo ambayo ni nje ya sheria za usalama barabarani. Baada ya mafunzo haya ya muda mfupi waajiri wenye tabia hizo watabadilika na kutuunga mkono uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani”, amesema Gyumi

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 28, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 18, 2017.

Posted by Esta Malibiche on MEI 18,2017 IN NEWS

8994-Mhe.Makamba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
 Naibu Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson  akiongoza    kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
8950-Mhagama na Makamba
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba   katika kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
8987-Mhe.Kijaji
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akifafanua jambo katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
8994-Mhe.Makamba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
9004-Naibu Waziri wa Habari
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
9090-Mhe.Manyanya
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng.Stella Manyanya akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
9046-Mhe.Mwakyembe
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk Harrison Mwakyembe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
9110-Waziri Mwakyembe na Naibu Waziri
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk Harrison Mwakyembe akizungumza jambo na Naibu wake Mhe.Anastazia Wambura  katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
9234-Mhe.Kigwangala
 Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.

Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

JAMALI JUMA AWATAKA VIONGOZI WA VIJIJI KUFUATA SHERIA ZA KIJIJI KUWAONGOZA WANANCHI

Posted by Esta Malibiche on MEI 18,2017 IN NEWS

Kushoto ni Jamali Juma afisa mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira kwa vitendo (LEAT) akifuatiwa na Afisa habari wa LEAT Edina Tibaijuka pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili wakati wa mkutamo wa hadhara wa kijiji cha kibada ukiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha kibada 
Hawa ni baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo wa hadhara wenye lengo la kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na Maliasili za kijiji

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Ili kuongoza au kusimamia jamii ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuondoa migogoro mbalimbali inajitokeza na itakayo kujitokeza kwa sababu ya kuzivunja sheria na taratibu hizo.

Hayo yamesemwa na Afisa mradi wa Mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira Jamali Juma wakati wa mkutano wa kijiji cha kibada kilichopo kata ya sadani wilayani Mufindi Mkoani Iringa kwa kuwataka viongozi na wananchi kutimiza wajibu na haki ili kukifanya kijiji kiwe na maendeleo.

Juma alisema kuwa sheria na taratibu zilizopo hapa kijiji zitanatakiwa kufuatwa kwa ajili ya manufaa ya sasa na ya kizazi kichacho lakini pia inajenga imani na amani ya kijiji.

"Leo hii usipofuata sheria na taratibu za kijiji lakina utakwazana na viongozi au wananchi na kupelekea migogoro ndani ya kijiji kwa kuwa sheria zinakuwa zimekiukwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977" alisema Juma

Aidha Juma aliwataka viongozi wa kijiji cha kibada kuitisha mikutano ya hadhara na kuwasomea mapato na matumizi ili wananchi wajue wapi kijiji kimetoka kimaendeleo na ipi mikakati ya kimaendeleo kijiji.

"Ukipita vijiji vingi unakuta migogoro mingi inayotokana na kutosomewa mapato na matumizi kwa sababu binafsi za viongozi husika hivyo ni lazima viongozi wa vijiji kuongoza vijiji kwa kufuata sheria na taratibu za kijiji"alisema Juma

Lakini Juma aliwataka wananchi wa kijiji cha kibada kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na Maliasili walizonazo na kuacha kuishi kwa mazoea ili kuboresha Mazingira ili yarudi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa kulima kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia.

"Jamani kuna njia nyingi za kulima mboga mboga kwa njia ya kisasa kwa mfano unaweza kuchukua gunia au sarufeti na kuuweka mchanga kisha kupanda mbegu za mboga na kumwagilia maji machafu unayokuwa unayatumia nyumbani kwao na kuvifanya vyanzo vya maji kuwa salama" alisema Juma

Fadinard yilikwipande,Shauri na Stephano waliitaka serikali kuanga upya sheria za kilimo cha mboga mboga kilinacholimwa kwenye utongo mnyevumnye au karibu na vyanzo vya maji kwa akili ya kilimo changu kwa ajili ya kujiongezea kipato chao.

"Sisi tunalima kwenye vijaruba vidogo vidogo tu maarufu kama vinyungu wala hatuleti madhara yoyote ya uharibifu wa vyanzo vya maji na mbona miaka yote tulikuwa tunalima bila kuharibu Mazingira na serikali itambue kuwa Kilimo hiki ni cha kitamaduni sasa inatakiwa kutofautisha sheria za mambo ya asili au ya kitammaduni"walisema wananchi wa kibada

Kwa upande wake Afisa habari wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira kwa vitendo (LEAT) Edina Tibaijuka aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha kibada kuzifuata sheria walizoletewa za kulinda Mazingira na vyanzo vya maji hadi pale serikali itakapoa tamko liingine kuhusu hiyo sheria.

"Jamani sheria ni msumeno hivyo mnapaswa kuzifuata kwa kuwa msipozifuta mtatiwa nguvuni na kupelekwa mahakama hivyo itakuwa inawapunguzia nguvu kazi yenu na kupelekea Msumbufu kwa familia zenu,Mimi nawaomba tiini sheria bila shuruti ili kuepukana na hayo matatizo" alisema Tibaijuka

Tibaijuka aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha kibada kupelekea malalamiko yao kwa viongozi wa serikali, madiwani na wabunge wao ili kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo la sheria hiyo mpya iliyokuja baada makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Samia Suluhu la kukataza Kilimo chochote kile kwenye vyanzo vya maji.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili aliwaomba viongozi wa serikali kuifikiria upya sheria waliyoitunga juu ya matumizi ya vyanzo vya maji kwa kuangalia utamaduni wa watu Vijijini hasa kwenye swala la Kilimo cha kipindi cha kiangazi maeneo ya mabondeni kwa kuwa wananchi wa Vijijini wantegemea kilimo hicho.

"Hivi kama huku wilaya ya Mufindi wakulima wanategemea Kilimo cha kulima kwenye mabonde maarufu kama Kilimo cha kwenye vinyungu kwa kupanda mboga mboga pamoja na mahindi ya msimu wa kiangazi"alisema Nyavili

WAZEE SIMBA WAMKATAA MOHAMED DEWJI ‘MO’ WAMUANDIKIA BARUA RAIS MAGUFULI

Posted by Esta Malibiche on MEI 18,2017 IN MICHEZO,

Wazee wa klabu ya Simba kupitia kikao cha hii leo kwa pamoja wameazimia kwenda kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ili kumueleza kilio chao baada ya kugundua kuwa kuna shinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali wakihitaji klabu hiyo auziwe Mohamed Dewji.
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari mratibu wa wazee wanachama wa Simba Felix Makuwa alisema kwamba wazee hao kwa upande wao hawana imani na Mohamed Dewji kwani ndie analeta mvurugano usiokuwa na tija ili afanikiwa kuinunua timu.
Nae mwanachama wa klabu hiyo Chuma Suleiman maarufu kwa jina la Bi hindu ameendelea kusisitiza swala hilo akitaka Rais Magufuli awasaidie kwenye jambo hilo kwani wanahisi kuna chembechembe za rushwa zenye lengo la kuidhohofisha Simba.

NAIBU MKURUGENZI WA IMF AKUNWA NA UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA, AAHIDI KUFUNGUA DIRISHA LA MIKOPO KWA TANZANIA



Posted Esta Malibiche on MEI 18,2017 IN NEWS

BEN1
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia) akielezea mpango wa Serikali wa kuboresha kilimo ili kukuza uchumi wa viwanda alipofanya Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (wa tatu kushoto), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
BEN2
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akielezea kuhusu ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) ambapo alisema itasaidia kuchochea maendeleo si tu kwa Tanzania bali na nchi jirani, wakati wa Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu.
BEN3
Naibu Mkurugenzi  wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto) akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani) kuhusu nia ya Shirika hilo kufungua fursa zaidi za mikopo kwa Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
BEN4
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa nne kushoto) na Naibu Mkurugenzi  wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
BEN5
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto) wakiagana baada ya kumaliza mkutano kati yao, katika Mkutano huo Zhang aliipongeza Serikali kwa hatua nzuri za ukuaji wa Uchumi.
BEN6
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kushoto) baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
……………………………………………………………………………….
Na Benny Mwaipaja, WFM
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang ameahidi kufungua madirisha ya mikopo kwa nchi ya Tanzania kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali za kukuza uchumi.
Bw. Zhang aliyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), katika ofisi za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
“Shirika la Fedha la Kimataifa limeziona jitihada za kukuza uchumi wa nchi ambapo mpaka sasa Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki na ipo juu ya wastani wa ukuaji wa uchumi Barani Afrika” Alisema Bw. Zhang.
Ameishauri Serikali kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi  katika ukuaji wa Uchumi ili uchumi huo uwe endelevu. Aidha ameitaka Serikali kuwa na mfumo shirikishi wa kifedha utakao wanufaisha wananchi wengi.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amesema kuwa juhudi za Tanzania  kwa sasa ni  kuchochea ukuaji wa Kilimo na kuongeza uzalishaji wenye tija
“Umasikini haujatatuliwa kwa kiwango ambacho Serikali ingependa kukiona, kwa kuwa mpaka sasa watu walio katika  umasikini na ukosefu wa huduma za lazima ni takribani asilimia 34.4 “, aliongeza Dkt. Mpango
Kama nchi imeamua kwenda kwenye uchumi wa kati na jambo ambalo linatiliwa mkazo ni upatikanaji wa umeme wa kutosha na wenye bei nafuu .
Amesema kuwa Serikali imefanya juhudi za kupeleka umeme mpaka vijijini lakini bado kazi hiyo haijakamilika. Pia suala la miundombinu ya ya usafirishaji ni changamoto, ukiwemo usafiri wa reli kutoka Mashariki hadi Magharibi mwa nchi ambao ni wazamani na umeharibika.
“Serikali imeamua kujenga Reli yenye kiwango cha Kimataifa (Standard gauge)  ambayo ni ya gharama, na kwa makadirio ya awali zinahitajika Dola Bilioni 7.6, lakini umechukuliwa uamuzi huo ili kuharakisha Maendeleo”aliongeza Dkt. Mpango
“Tayari tumeanza ujenzi wa reli hiyo kwa fedha za ndani kwa takribani Kilometa 200 kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro na tutaendelea na ujenzi kadri fedha zinavyo patikana” alifafanua Waziri Mpango .
Amesema kuwa, kumekuwa na tatizo la ahadi za Wahisani kutotekelezwa kwa wakati jambo linalofanya baadhi ya shughuli za maendeleo kutotekelezwa kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba, alisema ni  vema Serikali ikaendelea kuangalia vipaumbele  katika ujenzi wa miundombinu ili iweze kuchochea uchumi.
“Suala la ajira hasa kwa vijana linatakiwa kufanyiwa kazi na pia kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa Sekta Binafsi kwa kuwa Sekta Binafsi imekuwa na mchango mkubwa katika Maendeleo kwa nchi nyingi Duniani” Alishauri Bw. Mkwezalamba.
Ameishauri Tanzania kuendelea kuwekeza kikamilifu katika Sekta ya Elimu kwa kuwa ni moja ya eneo ambalo kama likifanyiwa kazi kikamilifu litaleta Matokeo chanya na ya haraka katika ukuaji wa Uchumi.
Akitoa ufafanuzi wa hoja hizo, Waziri Mpango, amesema Serikali imeendelea kuhakikisha kunakuwa na viwanda vingi ili vijana wengi waweze kupata ajira. Aidha tayari Tanzania imeanza kutekeleza Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kupata elimu

Jumatano, 17 Mei 2017

SERIKALI YAIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA

Posted by Esta Malibiche on MEI 17,2017 IN NEWS


Naibu waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo akisalimiana na wakuu wa Idara mara baada ya kuwasili katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya kilolo mkoani Iringa ,ikiwa ni moja ya ziara yake aliyoifanya jana
 
Naibu waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo akielekea kukagua ujenzi unaoendelea katika jengo la Hospitali ya wilaya ya kilolo Mkoani Iringa,katika moja ya ziara yake aliyoifanya jana.PICHA NA ESTA MALIBICHE
Na Esta Malibiche
KILOLO

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipongeza Halmsahauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa kwa utendaji wake mzuri  katika kutekeleza na kukamilisha shughuli za Maendeleo   kwa wakati,kuendana na fedha zilizotumika.

Pongezi hizo zimetolewa kutokana  na ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya kilolo unaoendelea kujengwa kwa kasi,ambayo mpaka kukamilika kwake kunatarajia kugharimu kiasi cha shilingi Billion 12.

Akizungumza  mapema leo hii[jana]mara baada ya kutembelea na kukagua  ujenzi huo namna unavyoendelea,Naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa[ TAMISEMI]Suleiman Jaffo alilidhishwa jinsi ujenzi huo unavyoendelea kujengwa katika kiwango cha hali ya juu na kuahidi kuwa,serikali iko tayari  kutoa kiasi cha fedha kilichobakia ili mradi huo uweze kukamilika kuanza kutoa huduma mara moja.

Jaffo alisema kuwa pamoja na kuridhishwa na kazi ya ujenzi huo,serikali inataka kuona ujenzi huo ukikamilika kwa wakati ili kupunguza msongamano kwenye Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

''Nimefurahishwa na kasi hii ya ujenzi na ubora wa jengo lenyewe.Hivi ndivyo serikali inataka miradi ijengwe,kwa usimamizi huu na uaminifu mliouonyesha nitahakikisha namshauri Mh. Rais ili fedha iliyobaki kukamilisha iweze kutengwa na hatimae tukamilishe kwa wakati ili iweze kuanza kutumiaka.''Alisema Jaffo

Awali akisoma taarifa  ya ujenzi wa mradi huo,Afisa mipango wa Halmashauri ya kilolo Josephine Mukungu,alisema  ujenzi wa Hospitali hiyo unaoendelea umelenga kuboresha huduma za Afya kwenye wilaya hiyo na kupunguza changamoto za kusafirisha wagonjwa wa Rufaa umbali mrefu,pia kupunguza vifo vya akina mama na watoto waliochini ya miaka mitano.

Mukungu alisema lengo kuu la ujenzi wa Hospital hiyo  ni kusogeza huduma za Afya karibu na jamii ikiwa ni utekelezaji wa sera ya Afya ya mwaka 2009 na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama  Tawala ya mwaka 2015na kusema kuwa Mradi huo ukikamilika utawezakuwanufaisha wananchi zaidi ya 222,146,kutokana na  kasi ya ukuaji wa watu unaolkadiliwa kuwa 1.7%  kwa mwaka kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012.

''Kwa kuzingatia ramani uya wizara ya Afya,waanawake,wazee,jinsia na watoto ili kukamilisha miundombinu yote,zaidi ya tssh. 12,000,000,000 zinahitajika.Hivyo kwa hatua za awali ili Hospitali iweze kufanya kazi kiasi cha Tsh. 4,200,000,000 zinahitajika''alisema Mukungu

Alisema kutokana na andiko lililowasilishwa wizara ya fedha na mipango,Halmashauri imekwisha pokea kiasi cha Tsh. 1,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo muhimu,ambapo kwa kuanzia Halmashauri hiyo imeanza kujenga majengo  matano ya ghorofa moja moja  kati ya majengo saba yatakayokamilisha Hospitali hiyo.

''Katika kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa ufanisi na kuendana na thanmani ya fedha kwa kiwango kinachohitajika,Halmashauri imetoa zabuni kwa wakandarasi watatu chini ya usimamizi wa wakala wa majengo Tanzania[TBA]  kujenga miundombinu ya awali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jingo la mionzi na umalizaji wa jingo la opd,ambao upo chini mkandarasi pancha building Construction ambae ameingia mkataba na Halmashauri kwa kaisi cha Tsh.1,199,255,387.50.Kati ya fedha hizo Tsh.292,345,00 kwa ajili ya ukamilishaji wa jingo la opd na kiasi cha Ts.906,910,387.5 ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mionzi'''Alisema Mukungu

''Ujenzi wa jengo la OPD umefikia hatua ya kuzekwa,kupigwa lipu,kuweka dari,mifumo ya umeme na ujenzi unaendelea.Jumla ya Tsh. 277,324,000.80 zimelipwa kati ya Tsh.1,199,255,387.5 kutoka mkataba Namba LGA\027\LGDG\SP\201\2017\W\01’’’’alisema Mukungu.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliishukuru serikali ya awamu ya tano jinsi inavyoijali jamii kwa kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wananchi ikiwa nipamoja na ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Kilolo.

Asia alimshukuru Naibu waziri Suleiman Jaffo kwa kutekeleza ahadi yake aliyowaaahidi wananchi katika moja ya ziara yake aliyoifanya mwaka jana  kuwa,serikali itahakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati,kuendeleza ujenzi wa Hospitali hiyo na kuhakikisha anasimami.

Nae Mbunge wa jimbo la Kilolo Venus Mwamoto alisemani  zaidi ya miaka  kumi  sasa imepita toka kuanzishwa kwa wilaya hiyo  lakini,kwa muda wote huo hakukuwa na Hospitali ya wilaya,hivyo mara ujenzi huo ukikamilika wananchi watapata matibabu kwa wakati na haraka tofauti na ilivyokuwa hapo awali wakitumia umbali mrefu kusafiri.