Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumanne, 31 Januari 2017

ANNA ABDALAH AWATAKA VIONGOZI WANAWAKE WAWAFUNDE WASICHANA ILI WAWE VIONGOZI BORA WA BAADAYE

Posted by Esta Malibiche on JAN31,2017 IN NEWS

 Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimvisha beji Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Zakhia Meghji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah 


Na Richard Mwaikenda

MJUMBE wa Bodi mpya ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Anna Abdalah, amewataka viongozi Wanawake kukutana na Wasichana kuwapiga msasa wa kuwaaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalah ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu nchini, aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TGGA, Mikocheni Dar es Salaam juzi.

Alisema ana mpango wa kuwaalika viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akutane na Wasichana wanachama wa TGGA wawafundishe maadili ya uongozi kwa lengo la kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalla alisema kuwa  hata yeye na Zakia Meghji pamoja na baadhi ya viongozi wengine wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali nchini, enzi za usichana wao walipitia kwenye chama hicho na kulelewa vizuri. 

Pia katika kikao kijacho cha Bunge, anatarajia kukutana na Wabunge Wanawake na kuwaeleza umuhimu wamara kwa mara  kukutana na wasichana  kuwafundisha kwa kuwapa hamasa uongozi ili nao wawe kuwa wabunge na hata miongoni mwao kuwa Spika na mawaziri.

"Nataka siku za usoni,tuwaalike viongozi mbalimbali akiwemo, Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Bunge, Wabunge na Mawaziri Wanawake ili mje mjumuike nao pamoja, mjifunze mambo mbalimbali ya uongozi na mhamasike, ili siku moja nanyi mje kuwa kama, Samia, Kamishna, Spika wa Bunge, Wabunge na hata uwaziri pia" alisema Anna Abdalah, huku akipigia makofi na waalikwa katika hafla hiyo.

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Engera Kileo, ilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho, wakiwemo pia wasichana watatu waliotoka Rwanda, Uganda na Madagasca waliokuwepo 

nchini katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamaduni. Wasichana hao ni; Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), Recheal Baganyire (Uganda) na Andriambolamanana Vahatrimama. 

Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, aliwataja Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni; Zakia Meghji, Anna Abdalah, Grace Makenya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia  Mjema na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda. Mwenyekiti wa Bodi hiyo  atateuliwa miongoni mwao.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Anna Abdalah wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TGGA wakati wa hafla hiyo. Aliyekaa kushoto ni Mariamu Kimbisa  ambaye ni Kamishna wa Kimataifa wa TGGA. Wa tatu kulia waliosimama ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
 Wasichana Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), kulia, Recheal Baganyire (Uganda), katikati, na Andriambolamanana Vahatrimama wa Madagascar ambao wapo nchini kaitika programu ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na maadili.wakiwa katika hafla hiyo.
 Wakipiga makofu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Anna Abdalah

 Anna Abdalah akihutubia katika hafla hiyo
 Mmoja wa wabia wa moja kati ya majengo ya TGGA, akisalimiana na Anna Abdalah
 Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shebe akitoa shukrani kwa wajumbe wapya wa bodi na wageni waalikwa kwa kuhudhuria uzinduzi huo.
 Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA pamoja na wanachama wa chama hicho.
 Sasa ni wakati wa msosi




 Wajumbe wa Bodi wakijadiliana jambo na watendaji wa TGGA
 Profesa Qooro akimuaga Zakia Meghji. Katikati ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
 Qooro akigana na Anna Abdalah. Kushoto ni Hangi
Mjumbe wa Bodi Grace Makenya akiaga

UZINDUZI WA SHEREHE ZA MIAKA 40 TANGU KUZALIWA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM, MKOA WA IRINGA WAVUNA WANACHAMA WAPYA 120









Jumatatu, 30 Januari 2017

RAIS DK. MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA KUTANGAZA JINA RASMI LA KITUO CHA AMANI NA USALAMA KILICHOPEWA JINA LA MWALIMU JULIUS NYERERE KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRICA (AU) ADDIS ABABA NCHINI ETHIOPIA

Posted by Esta Malibiche on JAN 30,2017 IN NEWS

 Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli akiwa na viongozi wa Nchi mabalimbali katika picha ya pamoja mbele ya jengo jipya la Kituo cha  Amani na Usalama la Julius Nyerere lililopo Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia.
 Rais Dk. John Magufuli akihutubia Viongozi Wakuu wa Nchi mbalimbali kuzindua Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa, Ethiopia, leo Januari 29, 2017.
 Rais Dk. John Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.
 Rais Dk. John Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia, leo. 
Rais Dk. John Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia, leo.  PICHA NA IKULU

UONGOZI WA BODABODA MKOANI MWANZA WAPONGEZA KAZI YA UKAGUZI WA INAYOFANYWA NA POLISI.

Posted by Esta Malibiche on JAN30,2017 IN NEWS

Binagi Media Group
Umoja wa waendesha bodaboda mkoani Mwanza umepongeza zoezi la ukaguzi wa vyombo hivyo linaloendeshwa na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.
Jana Mwenyekiti cha umoja huo, Makoye Kayanda, amesema zoezi hilo linaangazia maeneo makuu manne ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa watumiaji wa bodaboda wakiwemo abiria.
“Cha kwanza ni uvaaji wa kofia ngumu, cha pili leseni ya udereva, cha tatu kuwa na BIMA na ni ubebaji wa mishikaki. Kuna baadhi ya abiria zaidi ya 14 wametozwa faini kwa kukataa kuvaa kofia ngumu, sasa lazima tufuate sheria bila shuruti”. Alisema Kayanda huku akipongeza zoezi hilo.
Kayanda aliwasihi waendesha bodaboda wote kuzingatia utii wa sheria bila shuruti ili kuondokana na mazoea yanayoweza kuhatarisha maisha yao na abiria wao pia huku akiwaonya baadhi ya abiria kuepuka tabia ya kukataa kutumia kofia ngumu kwa kisingizio cha uchafu.
“Kupanga ni kuchagua, kama hutaki kuvaa kofia nguvu ya unayopewa na bodaboda, nunua ya kwako ama mfuko wa plastiki ili ukipewa kofia uvalie maana kuna watu wanapata ajali wanapasuka vichwa na inakuwa ni tatizo kwa familia zao na taifa kwa ujumla”. Alihimiza Kayanda.
Mwenyekiti wa bodaboda mkoani Mwanza, Makoye Kayanda

MADINI AINA YA BUNYU YAGUNDULIWA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

Posted by Esta Malibiche on JAN30,2017 IN NEWS

Lindi Yetu


.
Machimbo

Na. Ahmad Mmowa, Lindi
Utafiti uliofanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara (kanda ya kusini) umesababisha kugunduliwa kwa mashapo ya madini aina ya bunyu (kinywe) yenye uzito wa tani 689.7 milioni
 Hayo yameelezwa na mhandisi wa migodi wa kanda ya kusini, Aidan Mhando kwenye kongangamano la siku moja la wadau wa mradi wa uchimbaji wa madini ya bunyu katika vijiji vya Namangale, Utimbula vilivyo katika wilaya Lindi na mkoa wa Lindi, Chidya na Chiwata vilivyopo katika wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara. Yaliyofanyika katika manispaa ya Lindi.

Mhandisi Mhando ambae pia ni kaimu kamishna msaidizi wa madini wa kanda ya kusini, alisema kazi ya kuchimba kiasi hicho kilichogunduliwa inakaribia kuanza hivi karibuni.

Kwasababu hatua iliyobaki ni kupata leseni ya uchimbaji baada ya hatua nyingine kukamilika. Aliyataja maeneo ambayo uchimbaji huo utafanyika kuwa ni Namangale, Utimbula, Chiwata na Chidya. Ambapo mitambo mikubwa ya kuchakata itajengwa katika vijiji vya Utimbula na Namangale vilivyopo katika wilaya ya Lindi. Kutokana na uwingi wa madini hayo katika vijiji hivyo.

Alisema soko la bunyu ni zuri na kubwa kutokana na kuzalishwa na nchi chache wakati mahitaji ni makubwa. Akibainisha kwamba wazalishaji wakubwa walikuwa ni nchi ya China. Hata hivyo hivi sasa nchi hiyo haizalishi kwa wingi.
"Kuna haja ya kuanza uchimbaji haraka ili kuwahi soko kutokana na baadhi ya nchi jirani, ikiwamo Msumbiji inatani takribani bilioni mbili za madini hayo," alisema Mhando.

Mhandisi Mhando alizitaja kampuni za kampuni za utafiti ziligundua madini hayo kuwa ni Urinex inyofanya utafiti katika wilaya ya Ruangwa iliyogundua mashapo yenye uzito wa tani 174 milioni, Nachi katika wilaya ya Lindi (tani milioni 446), Lindi jumbo (tani milioni29.6) katika wilaya ya Ruangwa, na Ngwena (tani milioni 25) katika wilaya Ruangwa na Nachingwea.

Mhando alibainisha kuwa kampuni nyingine zinaendelea kufanya utafiti katika wilaya za Nachingwea na Ruangwa. 
Huku akizitaja kampuni hizo kuwa ni Nazareti, Pacco na ASA.

Aidha kaimu kamishna huyo alisema hadi sasa zimeshatolewa leseni ndogo za utafiti 4183 katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Ambapo katika mkoa wa Lindi zimetolewa 3625, na Mtwara 558.

Nae mwakilishi wa kampuni ya Nachi, mhamdisi Jimmy Ijumba alisema kampuni hiyo ambayo itachimba madini hayo inatarajia kusafirisha tani 100,000 hadi 180,000 kwa mwaka.

Ijumba alizitaja baadhi ya faida zitakazo patikana kupitia mradi huo pindi uchimbaji utakapoanza kampuni hiyo itawaajiri watu 270. Ambapo watu 220 kati ya hao watakuwa wazawa.
"Mradi utakuwa na faida nyingine, ikiwa ni pamoja na kuvutia uwekezaji mwingi wa huduma na uzalishaji mali ambao utapelekea utengenezaji wa fursa na ajira zaidi kwa wakazi wa maeneo ya mradi," alisema Ijumba.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Masasi, Semani Mzee alitoa wito kwa wawekezaji. Ikiwamo kampuni ya Nachi watumie uzoefu wa utekelezaji wa miradi iliyofanyika ili kuepuka kuwa chanzo cha migogoro kutokana kutolipa fidia kwa wakati kwa wanachi wanaachia maeneo na mali zao kwa ajili ya kupisha miradi mbalimbali.

Ambapo pia alitoa wito kwa wananchi wenye tabia ya kuendeleza maeneo ambayo yameshafanyiwa tathimini kwa lengo la kulipwa fidia kubwa waache tabia hiyo.

Kongamano hilo lililokuwa na lengo kuwajengea uelewa wadau hao kuhusu mradi huo uliwashirikisha pia wawakilishi kutoka kata za Chiwata na Namangale na viongozi wa serikali za vijiji vya Utimbula, Namangale A na B.

SERIKALI YALAANI VIKALI MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUENDELEA KUCHOCHEA MGOGORO WA PORI TENGEFU LA LOLIONDO

Posted by Esta Malibiche on JAN 30,2017 IN NEWS
01
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Waandishi wa habari jana  mjini Dodoma,  kuhusiana na  uchochezi unaofanywa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi kuchunga, kulima na kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo hali inayochangia kukausha  vyanzo maji yanayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
02
Kundi la mifugo likiwa ndani ya Pori Tengefu la Loliondo, karibu kabisa na mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inalaani vikali uchochezi unaofanywa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi kuchunga, kulima na kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo hali inayochangia kukausha  vyanzo maji yanayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana  mjini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema maelfu ya mifugo  kutoka nchi jirani ya Kenya imekuwa ikiingizwa  ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti muda wa saa 11 jioni,
Amesema katika kukabiliana na changamoto ya uharibu wa chanzo kikuu cha maji ya Serengeti kwa asilimia 47.2 ya maji yote, tayari mifugo 1700 imeshakamatwa
Mbali na mifugo  hiyo, Waziri Maghembe alisema kuwa maelfu ya Matrekta ya kutoka nchini Kenya yameletwa kulima katika maeneo yanayopakana na Serengeti
Aliongeza kuwa  hivi karibuni kilimo kimeshamiri ambapo kipindi cha nyuma wakazi  walikuwa wanalima na ng’ombe (maksai) ila sasa matrekta ya Kenya yanalima na kufungua mashamba makubwa.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Maghembe ameagiza kuwa raia wa Kenya wenye  mifugo  Loliondo warudi makwao mara moja, Mkoa na Wilaya uchukue hatua kuwaondoa mara moja
Pia, Matrekta yote ya nchi ya Kenya yawe na usajili wa kodi (Tax Clearance) toka TRA au yarudi kwao mara moja
Aidha, ameagiza kuwa  eneo la 1,5002km liwekewe alama mara moja na uwekaji alama ukamilike ifikapo  tarehe 30 Machi, 2017.
Kwa upande wa Utalii, Ameziagiza kampuni zote za utalii ambazo hazina usajili wa kitaifa zinazofanya biashara kwa mikataba ya vijiji ziripoti Wizarani ndani ya siku saba, Ikiwa pamoja na kuonyesha usajili wao, kuonyesha vitalu walivyopewa na Serikali pamoja kuiridhisha Serikali kama wanalipa kodi.
Awali, akizungumzia kuhusu mgogoro huo wa Pori Tengefu la Loliondo, Waziri Maghemba alisema anatambua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo  anasimamia mazungumzo ya wadau wote ili kuleta utatuzi wa mgogoro huo.
‘’Nimeambiwa kuwa mwelekeo wa mazungumzo ni mzuri nahimiza mazungumzo yaendelee, lakini  nimeona  nikingoja hadi mazungumzo hayo  yaishe Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  itakuwa haipo.’’ alisisitiza

TAARIFA YA UOKOZI WACHIMBAJI MADINI WALIOFUKIWA NA KIFUSI- GEITA

Posted by Esta Malibiche on JAN 30,2017

RZ1
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuufahamisha  umma kuwa, Zoezi la kuwaokoa wachimbaji 15 waliofukiwa na kifusi  tarehe 26/01/2017 kwenye mgodi wa dhahabu eneo la kijiji cha Mawemeru, Nyarugusu Wilayani Geita limekamilika kwa mafanikio.
Ajali ya kufukiwa wachimbaji hao iliyohusisha Watanzania 14 na raia 1 wa China ilitokea kwenye leseni ya uchimbaji wa Kati wa madini ya dhahabu yenye Namba ML 492/2013 inayomilikiwa na Bw. Ahmed Mubarak Adam.
Chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni kuanguka kwa shaft ya mgodi huo na kufukiwa na kifusi wakati wachimbaji hao wakifanya kazi mgodini chini ya ardhi.
Tukio la uokoaji limefanikiwa leo tarehe 29/01/2017 ambapo wahanga hao walianza kutolewa shimoni kuanzia saa 5 hadi saa 5:30 asubuhi wote 15 wakiwa hai ingawa walikuwa wamedhoofika kiafya.  Aidha, wachimbaji hao wamepewa huduma ya kwanza katika eneo la ajali na kisha kukimbizwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Geita. Hadi sasa wachimbaji hao wapo Hospitali wakiendelea na matibabu kwa uchunguzi zaidi wa afya zao.
Juhudi za kuokoa wachimbaji hao  ambazo zilifanyika kwa kufukua kifusi katika eneo la ajali zilianza mara baada ya tukio hilo kutokea. Uongozi wa Mkoa wa Geita ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa Meja. Jen.(Mst) Ezekiel E. Kyunga ulishirikiana na Wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni za Madini mbalimbali mkoani Geita katika zoezi la ufukuaji kifusi ili kuokoa maisha ya wchimbaji hao. 
 Kampuni zilizoshiriki kwa kutoa mitambo na vifaa mbalimbali ni Kampuni ya Busolwa Mining Ltd; Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM); Kampuni ya Nyarugusu Mining Ltd; Nsangano Mining Project; Metchell Tanzania Drilling; WAJA Hospital pamoja na wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Geita wakiongozwa na Viongozi wa wachimbaji madini Wilaya, Mkoa na Taifa.
Akizungumza mara baada ya kuokolewa wachimbaji hao, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard amewashukuru wadau wote walioshiriki kwa hali na mali kufukua kifusi na hatimaye kufanikiwa kuwatoa wachimbaji chini ya ardhi wakiwa hai.
Dkt. Kalemani amewaomba Watanzania kuendelea na moyo huo pale majanga kama haya yanapotokea. Aidha, Dkt. Kalemani ameagiza shughuli zifungwe kwa muda wa siku tano kwenye mgodi uliopata ajali kuanzia tarehe 29/01/2017 ili kutoa nafasi kwa Kamishna wa Madini kufanya tathmini ya hali ya usalama wa mgodi na kutoa maelekezo kabla ya shughuli kuanza.
Vilevile, amewataka wachimbaji wawe watulivu katika kipindi ambacho tathmini ya hali ya usalama wa mgodi inafanyika na kuagiza Uongozi wa Mkoa kuhakikisha kuwa ulinzi unaimarishwa eneo la mgodi ili watu wasiweze kuingia na kuhatarisha maisha yao.
Pia, ameagiza ukaguzi wa kina ufanyike kwenye migodi mingine ya wachimbaji wadogo na ya kati eneo la Nyarugusu na kwingineko nchini ili kuhakikisha kuwa migodi inakuwa salama kwa wachimbaji wa migodi husika.
Imetolewa na;
KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
29/1/2017