Jumatano, 1 Juni 2016
KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ATEMBELEA MRADI WA UZALISHAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA GEREZA LA MTEGO WA SIMBA NA GEREZA KUU LA WANAWAKE KINGOLWIRA
04:55
No comments
04:54
No comments
| mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu (kulia) akimpokea waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba alipofanya ziara ya kikazi wilaya ya Manyoni jana |
| Waziri Nchemba akisalimiana na mbunge Nyalandu (kulia) |
| Waziri wa kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali kuingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku Manyoni |
| Mbunge Lazaro Nyalandu kulia akiwa na waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba wakati akisaini kitabu cha wageni ofisi ya mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida |
| Waziri Nchemba akiingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku manyoni |
| Wakulima wa Tumbaku wakisalimiana na waziri Nchemba |
| Baadhi ya madiwani wakulima wa Tumbaku manyoni wakimpokea waziri Mwigulu Nchemba |
| Baadhi ya wakulima wa Tumbaku wakiwa ukumbi wa mkutano kati yao na waziri Nchemba |
| Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu akitambulisha viongozi mbali mbali kabla ya mkutano wa wakulima wa Tumbaku kuanza |
| Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akizungumza na wakulima wa Tumbaku wilaya ya manyoni mkoa wa Singida jana |
| Wakulima wa Tumbaku wakitoa kero zao kwa waziri Nchemba (hayupo pichani) |
| Wabunge wakisikiliza kero za wakulima wa Tumbaku |
Waziri
wa Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza kwa makini
Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu wakati akieleza kilio
cha wakulima wa Tumbaku wilaya ya Manyoni wakati wa mkutano wa waziri
Nchemba na wakulima wa Tumbaku uliofanyika ukumbi wa CCM Manyoni jana
…………………………………………………………………………………………….
Na MatukiodaimaBlog,Manyoni
WAZIRI wa kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba amefuta
michango hewa iliyokuwa ikichangiwa na wakulima wa Tumbaku kwa UNION
kwa kupitia kitengo cha AMIS huku akiagiza serikali ya wilaya ya
Manyoni kuwachukulia hatua kali aofisa ushirika mkoa Andru Msafiri
na afisa ushirika Wilaya hiyo Bw Alfred Sekiete iwapo watabainika
kuhusika deni la bilioni 7 ambalo wanadaiwa benki wakulima wa
tumbaku.
Waziri Nchemba alilazimika kutoa maagizo hayo baada ya
wakulima wa zao hilo la Tumbaku kulalamikia utaratibu mbaya wa baadhi
ya viongozi wa UNION na APEX pamoja na baadhi ya maofisa ushirika
kujinufaisha kupitia mgongo wa wakulima hao.
Akitoa agizo hilo jana mjini Manyoni wakati wa
mkutano wa pamoja kati yake na wakulima wa Tumbaku na viongozi
mbali mbali wa Serikali ya wilaya ya Manyoni na wabunge wanaotoka
wilaya ya Maeneo yanayolimwa Tumbaku mkoani Singida.
Waziri Nchemba alisema kuwa baadhi ya mambo ambayo
serikali ya Rais Dr John Magufuli haipendi kuona ni pamoja na
wakulima kubebeshwa mizigo mikubwa ambayo kimsingi haiwasaidii kupiga
hatua kimaendeleo zaidi ya kuwatesa .
Alisema inashangaza kuona wakulima hao kuendelea kuumizwa
na viongozi wachache ambao wamegeuza wakulima ni kichaka cha wao
kujificha kujinufaisha kupitia wakulima.
“ Mambo ya ajabu sana hiki kitu kinaitwa AMIS ni kuwatoza
wakulima michango ya ajabu ajabu eti wakulima kutozwa dola 1200 kwa
ajili ya kusafirisha Tumbaku toka Dar es Salaam kwenda UNION pia
wanachangia dola 10 kwa kutunza kumbukumbu zao ,dola 3 kupakia na
kushusha mara mchango kwa ajili ya ADMIN mambo ya ajabu kabisa
wakulima wanahusika vipi na malipo maadmin yani wanatumia lugha za
kijanja kijanja kuwaibia wakulima ADMIN wa makundi kama yale ya
Whatsap kwa wakulima tena…sasa kuanzia leo natangaza kufuta michango
hii isiyo na maelezo ya kutosha na kuagiza kujipanga upya kwa
kuwashirikisha wakulima na taarifa hiyo ndani ya siku 7 niipate “
Waziri chemba alisema kuwa kabla ya kuanza kuwatoza
wakulima hao michango ni vizuri makubaliano ya michango hiyo
yafanyike upya kwa kuwashirikisha wakulima na sio kuendelea kutumia
taratibu za zamani ambazo ni mzigo kwa mkulima.
Kuhusu maafisa ushiriki kudaiwa kukopa benki kupitia mgongo
wa wakulima wa tumbaku na kupelekea wakulima hao kudaiwa deni
benki la Tsh bilioni 7 aliagiza mkuu wa wilaya ya Manyoni kuagiza
wakaguzi na wataalam wake kufanya uchunguzi na iwapo itabainika
kuwa maofisa hao walihusika na deni hilo hatua stahiki kuchukuliwa
dhidi
Heri ya Kuzaliwa Mwanalibeneke wa Lukaza Blog – Josephat Lukaza
04:53
No comments

Kwanza Napenda kuchukua Nafasi hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kuniwezesha kuiona siku ya Leo maana Si kwa uwezo wangu bali ni kwa Uwezo wake Muumba wetu aliye Juu.
Leo
ni siku muhimu sana kwangu maana inanikumbusha siku niliyoletwa Duniani
na Mungu kupitia Mama yangu kwa kusudi maalumu hapa duniani.
Napenda
Kumshukuru Mungu kwa maana neema na rehema zake ni Za milele. Nasema
asante kwa kunifanya kuongeza mwaka mwingine huku nikiwa na afya njema.
Kiukweli Sina cha Kumlipa Mwenyezi Mungu zaidi ya Kumsifu na Kumwabudu yeye kwa maana Sio kwa uwezo wangu.Napenda kuwashukuruni wote Ambao Mmekuwa mkiniombea na kunitakia heri ya kuzaliwa kwangu Nasema asante na Mungu awabariki sana.
Kiukweli Sina cha Kumlipa Mwenyezi Mungu zaidi ya Kumsifu na Kumwabudu yeye kwa maana Sio kwa uwezo wangu.Napenda kuwashukuruni wote Ambao Mmekuwa mkiniombea na kunitakia heri ya kuzaliwa kwangu Nasema asante na Mungu awabariki sana.
Nakukabidhi
wewe bwana njia zangu na kukutumainia kwasababu umeagiza kila
akukabidhie njia zake na kukutumainia unaenda kumtendea. Zaburi 37: 5
Leo nasema asante sana kwa Maana kila napokuita Wewe unaitika.
Naomba
pia uendelee kuziimarisha hatua zangu kwa maana uliagiza katika Zaburi
37:23 Kuwa “Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake”
Hakika wewe ni Mungu wa Wote.
Nachukua
fursa hii kuwa shukuruni wote Ambao mmenitakia baraka na heri katika
siku hii muhimu sana kwangu ambayo inanifanya nitafakari matendo yangu
hapa duniani, Uhusiano wangu na Mungu wangu, Uhusiano wangu na Ndugu
zangu, Uhusiano na Jamii yangu pamoja na rafiki zangu hakika Namshukuru
Mungu sana kwa kuniwezesha kupatana na Ndugu zangu, jamii yangu na hata
marafiki zangu. Kiukweli Namshukuru Mungu kwasababu Ni kwa neema zake na
Rehema zake ndio zimenifikisha hapa wala sio kwa ujanja wangu wala mimi
sio mwema sana kuzidi wengine.
Wewe
Ni Mungu wa wote, Huchelewi wala Huwahi Hakika nitakusifu na kukuabudu
siku zote za maisha yangu kwa maana matendo yako makuu uliyonitendea
Nayaona na kuyafurahia.
Asante
sana Mungu wangu naomba uendelee Kutimiza haja za Moyo wangu.
Nitaendelea Kukushangilia na Kukusifu kwa maana kila napokuita unaitika.
Happy Birthday to You Josephat Lukaza – Lukaza Blog
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI NCHINI PAPUA NEW GUINEI LEO
04:52
No comments
DKT SHEIN KUZUNGUMZA NA MABALOZI WILAYA MJINI LEO
04:51
No comments
TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO (TASWA)
04:50
No comments
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imemteua Makamu
Mwenyekiti wa TASWA, ambaye pia Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya
Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM), Egbert Mkoko kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za
Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2015/2016.
Pia TASWA imeteua wajumbe tisa
wa kamati hiyo. Majina yao na vyombo vyao katika mabano ni Mahmoud
Zubeiry (Bin Zubeiry Sports- Online), Jane John (TBC), Baruani Muhuza
(Azam Media), Limonga Justine (Redio Uhuru), Maulid Kitenge (E-FM
Redio), Deogratias Rweyunga (Redio One/ITV), Shaffih Dauda (Clouds
Media), Asha Muhaji (Bingwa) na Nelly Mtema (Daily News).
Kamati inaweza kuongeza wajumbe
wengine au kupunguza kwa kadri itakavyoona inafaa. Utaratibu wa
kuizindua kamati hiyo unaandaliwa na sekreterieti ya TASWA. Jukumu la
kamati itakuwa ni kuandaa utaratibu wa kuwapata wanamichezo watakaowania
tuzo hiyo na pia kuteua washindi kwa kila mchezo.
Tuzo za Wanamichezo Bora
zinazotolewa kila mwaka na TASWA zimepangwa kufanyika Agosti 26, mwaka
huu, Dar es Salaam zikihusisha michezo mbalimbali.
B; ZIARA YA MAFUNZO NAIROBI
TASWA kwa kushirikiana na Chama
cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya, vimeanzisha program ya ziara
ya mafunzo na kubadilishana uzoefu baina ya vyama hivyo viwili, ikiwa
katika makundi tofauti ya wahariri/waandishi waandamizi na kundi lingine
la waandishi wa habari chipukizi.
Kwa kuanzia wahariri wa habari
za michezo 18 au wale wenye uzoefu katika uandishi usiopungua miaka kumi
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wataenda Nairobi kwa ziara
ya mafunzo kuanzia Julai 6-9 mwaka huu.
Tunaamini wakirudi wataendelea kuwa waalimu wazuri kwa wale chipukizi, ambao nao watapata fursa kama hiyo siku za usoni.
Ahsanteni,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
01/06/2016
Hifadhi ya Selous yapoteza asilimia 90 ya Tembo wake
04:47
No comments
Hifadhi ya Taifa ya wanyamapori
ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania imepoteza asilimia 90 ya Tembo
waliopo katika hifadhi hiyo kutokana na ujangili uliokithiri.
Ripoti ya mfuko wa hifadhi ya
wanyapori na mazingira duniani (WWF) imesema kufikia mwaka 2022 kama
hakutakuwa na hatua zozote kali zitakazochukuliwa kuwalinda tembo
kutokana na ujangili basi watatoweka kabisa.
Ripoti hiyo imeendelea kusema
kuwa kwa miaka ya nyuma mbuga ya Selous ilikuwa mojawapo ya mbuga kubwa
kabisa katika bara la afrika yenye tembo wengi ambapo kulikuwa na tembo
zaidi ya 110000 lakini kutokana na ujangili uliokithiri katika miaka 40
iliyopita tembo hao wamepungua na kubakia 15000 tu uku mahitaji makubwa
ya pembe za ndovu katika nchi ya china yakitajwa na ripoti hiyo kuwa
kichocheo kikubwa cha ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo hao.
Aidha ripoti hiyo inaonyesha
hathari kubwa kiuchumi itakayotokea kutokana na kwamba Tanzania
kupitia Mbuga ya Selous inaingiza dola milioni 6 kwa mwaka
ikilinganishwa na Sekta ya Viwanda inayochangia dola bilioni 5 katika
pato la Taifa.
Pamoja na Hayo Serikali ya awamu
ya tano kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka mikakati
madhubuti ikiwemo kuunda kitengo chake cha intelijensia na kuunda kanda
nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya mbuga ya
Selous ambayo imeanza kuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kushirikiana
na wadau wa uhifadhi kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa
ajili ya doria.
Mwaka 2014 Shirika la Kimataifa
la Sayansi,Elimu na Utamaduni la umoja wa mataifa(UNESCO) liliiweka
Mbuga ya Selous katika Urithi wa asili ulio hatarini Duniani.





