Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumamosi, 23 Juni 2018

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI 6 YENYE THAMANI YA BILL.2 WILAYANI NACHINGWEA MKOANI LINDI

Posted by Esta Malibiche on JUNE 23,2018 IN NEWS
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango akikabidhiwa  Mwenge wa Uhuru kutoka kwa  Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi  Joseph Mkirikiti.Makabidhiano hayo yalifanyika jana asubuhi katika kijiji cha Mpiruka mpakani mwa Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea.

Akizungumza na mtandao huu wa habari[KALI YA HABARI BLOG] Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango alisema kuwa jumla ya miradi 6 yenye thamani ya bill.2  imezinduliwa,kukaguliwa na kuwekewa jiwe la msingi.
Mara baada ya kuhitimisha mbio zake wilayani humo,Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa leo wilayani Liwale,ambapo makabidhiano yamefanyika katika kijiji cha Nangano mpakani mwa Nachingwea na Liwale.



Picha ya Pamoja mara baada ya kuzindua mradi wa jengo la shule ya awali na Msingi lililopo kata ya Ugawaji,inayomilikiwa na Masista wa kanisa katoliki Parokia ya Nachingwea.




NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA RODRICK MPOGOLO AIKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE YA SEKONDARI MWEMBETOGWA IRINGA

Posted by Esta Malibiche on JUNE 23,2018 IN SIASA
Naibu katibu mkuu ccm bara Rodrick Mpoholo akikabidhi mifuko ya  saruji kwa uongozi wa shule ya sekondari Mwembetogwa inayomilikiwa na jumuiya ya wazazi ccm,iliyopo Manispaa ya  Iringa,ambapo jumla ya mifuko 100 imekabidhiwa shuleni hapo kwa ajili ya  ujenzi wa nyumba ya mlezi wa wanafunzi wa kike[Matron]

Mifuko ya saruji iliyokabidhiwa na Naibu katribu Mkuu .



 Naibu katibu mkuu ccm bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi mpira kiongozi wa  michezo katika shule ya Sekondari Mwembetogwa .

Naibu katibu mkuu ccm bara Rodrick Mpogolo akisalimiana na walimu wa shule ya sekondari Mwembetogwa mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
 Naibu katibu mkuu ccm bara Rodrick Mpogolo akisalimiana na wanafunzi.


Naibu katibu mkuu ccm bara Rodrick Mpogolo akiendelea kusalimiana na wanafunzi
Naibu katibu mkuu ccm bara Rodrick Mpoholo akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao.






Walimu na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwembetogwa wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu katibu mkuu pamoja na viongozi wa ccm Mkoa wa Iringa.













Ijumaa, 22 Juni 2018

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA RODRICK MPOGOLO AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CCM MKOA WA IRINGA LEO HII

Posted by Esta Malibiche on JUNE 22,2018 IN SIASA

 Naibu katibu mkuu ccm bara Rodrick Mpogolo akizunguymza leo hii na wajumbe wa Halmashauri kuu ccm Mkoa wa Iringa,Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akifuatiwa na Katibu wa ccm Mkoa wa Iringa Christopher Magala ,kulia kwa Naibu katibu mkuu ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ccm Taifa viti 15 tanzania bara Teresia Mtewele pamoja na Mnec wa Mkoa wa Iringa ambae pia ni mjumbe wa Halmshauri kuu ccm Taifa Salim Asas.

 Naibu katibu mkuu ccm bara Rodrick Mpogolo akisalimiana na katibu wa uvccm Wilaya ya Iringa  vijijini,Mkala Mapesa mara baada ya kuwasili katika ofisi za ccm Mkoa wa Iringa.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara,Rodrick Mpogolo  akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM mkoa wa  leo. 
 Naibu katibu mkuu ccm bara Rodrick Mpogolo akizunguymza na wajumbe wa Halmashauri kuu ccm Mkoa wa Iringa,katika kikao kilichofanyika leo hii ofisi za ccm Iringa Mjini.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akifuatiwa na Katibu wa ccm Mkoa wa Iringa Christopher Magala ,kulia kwa Naibu katibu mkuu ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ccm Taifa viti 15 tanzania bara Teresia Mtewele.


 Mbunge wa jimbo la Isimani kupitia chama cha Mapinduzi ccm,ambae pia ni waziri wa Ardhi.Nyumba na makazi Willium Likuvi akizungumza.

 Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Christopher Magala akizungumza.


Mjumbe wa Halmashauri kuu ccm Taifa viti 15 Tanzania bara Teresia Mtewele akizungumza
 Mnec wa Mkoa wa Iringa ambae pia ni mjumbe wa Halamshauri kuu ccm Taifa Salim Asas akizungumza.





  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizunmgumza.


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza.


























Alhamisi, 14 Juni 2018

URUSI YAANZA VIZURI KOMBE LA DUNIA,YAICHAKAZA SAUDI ARABIA 5-0

Posted by Esta Malibiche on JUNE 15,2018 IN MICHEZO
 4D3BF5C300000578-0-image-a-5_1528991066463-950x634
Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Luzhniki kwa wenyeji Urusi kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 5-0 dhidi ya Saudi Arabia katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia.
4D3C2F4700000578-5844851-image-a-18_1528993702196-660x400
Mechi hiyo ya aina yake imeshuhudiwa bao la kwanza likiwekwa kimiani mnamo dakika ya 12 na Ganzizky ambalo limeandika rekodi ya kuwa bao la kwanza katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huu.
4D3BD0C500000578-0-image-a-1_1528990850078-950x614
4D3BE6B000000578-5844851-image-a-2_1528992378569-950x654
Mabao mengine yametiwa kimiani na Cheryshev (43′ minutes, 90’+1), Dzyuba (71′ ) na Golovin (90’+4).
4D3BDDF400000578-5844851-image-a-10_1528991182676-950x608
4D3C506E00000578-5844851-image-m-28_1528993857900-950x624
Baada ya wenyeji kuanza vizuri, mechi zingine za kesho zitakuwa ni Iran itakayowakaribisha Morocco na vilevile Ureno itakuwa inacheza dhidi ya Spain

SALAM MBALIMBALI ZA SIKUKUU YA EID MUBARAK 2018

Posted by Esta Malibiche on JUNE 15,2018 IN NEWS



MTANDAO HUU WA HABARI(KALI YA HABARI BLOG)UNAPENDA KUWATAKIA EID MUBARAK**  NJEMA WAISLAM WOTE.UNAUNGANA NANYI KATIKA TUKIO HILI LA KIIMANI.
TUSHEREKEE KWA AMANI,UTULIVU NA MSHIKAMANO.

TUDUMISHE IMANI YETU NA TUISHI MAISHA MEMA KAMA AMBAVYO MWENYEZI MUNGU ANAVYOTUTAKA TUISHI.
EID MUBARAK.










Add