Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumanne, 10 Julai 2018

BANK YA CRDB YAMKABIDHI MIFUKO 724 YA SARUJI MBUNGE WA JIMBO LA DODOMA MJINI ANTHONY MAVUNDE

Posted by Esta Malibiche on July 10,2018 IN NEWS

 Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo amepokea mifuko ya Saruji 724 yenye thamani ya Tsh 10,000,000 kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa,Nyumba za Walimu na matundu ya vyoo katika shule za Msingi na Sekondari katika Jimbo la Dodoma Mjini.

Akikabidhi mifuko hiyo ya Saruji,Mkurugenzi CRDB Tawi la Dodoma Bi Rehema Hamis amesema kwamba Benki ya CRDB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mh Rais Dr John Pombe Magufuli na uchapakazi wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde katika kuboresha miundombinu ya Elimu.

Akipokea mifuko hiyo ya saruji,Mbunge Mavunde ameishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo ambao utalenga kupunguza changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa 1035 katika Jimbo la Dodoma Mjini ambapo kwa hivi sasa anaendesha kampeni maalum ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi na kwa kuanzia mfuko wa Jimbo umetoa matofali 32,000 na mifuko ya Saruji 2,560 kwa kata mbalimbali.







MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM, OFISI NDOGO ZA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA JIINI DAR ESALAAM, LEO

Posted by Esta Malibiche on july 10,2018 IN SIASA

 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akilakiwa na wajumbe alipowasili ukumbini kuogoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jinini Dar es Salaam, leo.

 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akilakiwa na wajumbe alipowasili ukumbini kuogoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jinini Dar es Salaam, leo.

 Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jinini Dar es Salaam, leo.

Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akiogoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jinini Dar es Salaam, leo.

MKUU WA WILAYA ARUSHA AIPONGEZA SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW KWA KUHAMASISHA ELIMU




Posted by Esta Malibiche on july 10,2018 IN NEWS

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro aipongeza Taasisi ya  Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhamasisha maswala ya elimu katika Mkoa wa Arusha awataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo’ aliyasema hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini hapa, ambapo Taasisi hiyo iliandaa Tuzo maalumu kwa mwalimu bora(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)


Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo ,iliyofanyika hivi karibuni katika shule ya Levolosi jijini hapa,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa wameaanda Tuzo hiyo kwa shule za msingi jiji la Arusha na Meru kwa walimu 20

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya sombetini,Caroline Kiyoja cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Sinoni,Dorice Mhina cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow 

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Levolosi,Elizabeth Minja cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Uhuru,Jane Mkomwa  cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Lucky Vicent Julius Saunyi  cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Daraja  mbili Leah Mshana  cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow


Waalimu kutoka shule za msingi jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja Tuzo hiyo maalumu iliandaliwa na shirika la Foundation For Tomorrow kwaajili ya waalimu waliobainika kufanya kazi zao kwa umahiri mkubwa
Na Pamela Mollel,Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro ameipongeza Taasisi ya  Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika  kuhamasisha maswala ya elimu katika Mkoa wa Arusha .
 Aliyasema  hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini hapa ambapo alisema shirika hilo limekuwa bega kwa bega katika kuhamasisha maswala mbalimbali ya Elimu na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo
 “Foundation for Tomorrow wamekuwa mstari wa mbele sana katika maswala ya elimu mfano mzuri leo wameanda Tuzo maalumu kwa mwalimu bora ambaye amekuwa akifanya kazi zake kwa umahiri mkubwa”alisema Daqarro
Kwa upande wake Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa lengo la Tuzo hiyo ni kutia hamasa miongoni mwa walimu waliobainika kufanya kazi zao kwa bidii na umahiri mkubwa
Alisema kuwa katika zoezi hilo la kumsaka mwalimu bora limezingatia vigezo vyote ikiwemo uwezo wa kuhamasisha ufikiri wa kina miongoni mwa wanafunzi,uwezo wa kutengeneza mazingira ya kushiriki na mazingira rafiki ya kujifunza,uvumbuzi na ubunifu katika swala zima la ufundishaji na utekelezaji wa mtaala
Kayanda aliongeza kuwa vigezo vingine ni pamoja na kujikita katika kusaidia watoto wenye changamoto za kujifunza pamoja na uzoefu wa kujifunza
Alisema kuwa katika Tuzo hiyo ya mwalimu bora kila mwalimu atapewa zawadi ya cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI REAIII WILAYANI KILOSA, VIJIJI 180 MKOANI MOROGORO KUNUFAIKA

Posted by Esta Malibiche on July 10,2018 IN NEWS
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, na viongozi wengine wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini REA Awamu ya Tatu (REAIII), kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro Julai 9, 2018. Mhe. Naibu Waziri pia alitumia fursa hiyo kusikilzia kero za wnanchi kuhusu upatikanaji umeme kwenye vijiji vyao.




 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mafulu kata ya Kitete wilaya ya Kilosa wakati wa ziara yake kusikiliza kero nakuzipatia ufumbuzi kuhusiana na mradi wa umeme vijijini (REA) REA Awamu ya Tatu(REAIII) mzunguko wa tatu mkoa wa Morogoro.
 Wananchi wakimsikilzia Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, wakayti akihutubia
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akizungumza na wananchi wakijiji cha Mafulu kata ya Kitete wilaya ya Kilosa
 Diwaniwa kata ya Kimamba A, Upendo Mpoto akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri waNishati, Mhe. Subira Mgalu wakati akisikiliza kero zinazohusiana na mradi waumeme vijijijini.
Diwani wa Kata ya Kimamba akizungumza kwenye mkutano huo.
  NaibuWaziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (Mwenye Kilemba chekundu kichwani)akimsikiliza Diwani wa kata ya Kitete wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Bw. StephenLukobe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Maful. Wakwanza
kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Maganga.
NaibuWaziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu kulia akizungumza jambo na Diwani wa kataya Kitete wilaya ya Kilosa, Stephen Lukobe katika ofisi ya kijiji cha Maduduwakati wa ziara ya naibu waziri huyo ya kutembelea vijiji vitavyonufaika namradi wa umeme wa REA Awamu ya tatu (REAIII), mzunguko wa tatu mkoa wa MorogoroJulai 9, 2018
Makzi wa kijiji cha Mandera, Wilayani Kilosa, akizungumza mbele ya Naibu Waziri
NA
K-VIS BLOG, MOROGORO


NAIBU
Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, amezindua mradi wa usambazaji umemevijini REA awamu ya tatu (REAIII), ambapo jumla ya vijiji 180 vya Mkoa waMorogoro vitanufaika.

NaibuWaziri alifanya uzinduzi huo kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoanihumo Jumatatu Julai 9, 2018 kwa kukata utepe na kuwasha swichi ya umeme na hivyo kuibua shangwe, nderemo na vifijo kutokakwa wananchi waliojawa na furaha.
Akizungumzabaada ya uzinduzi huo Mhe. Naibu Waziri Subira Mgalu, alisema, Serikali yaAwamu ya Tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John Pombe Magufuli inayo dhamira ya kweli ya kuhakikisha ahadi zote
ilizotoa kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wote wa Tanzania mijinina vijijini inatekelezwa kwa kasi.
“Tayari umeme umefika sasa utumieni kikamilifu kujiletea maendeleo yenu na taifa kwa ujumla.” Alisema Mhe. Naibu
Waziri.
 
Gharama za kuunganishiwa umeme huo ninafuu sana kiasi cha shilinbgi Elfu Ishoirini na Saba tu (27,000) 

DR.MWIGULU NCHEMBA AKABIDHI RASMI OFISI LEO HII

Posted by Esta Malibiche on july 10,2018 NEWS

PIX 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo. Hata hivyo, Waziri Lugola alisema aliwahi kua mwanariadha, hivyo atahakikisha anasonga mbele kuendelea na safari, hata angalia nyuma.

PIX 2

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akipongeza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba mara baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo. Hata hivyo, Waziri Lugola alisema aliwahi kua mwanariadha, hivyo atahakikisha anasonga mbele kuendelea na safari, hata angalia nyuma.

PIX 3

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Katibu wa Waziri Nelson Kaminyoge, alipokua anataka kumkabidhi taarifa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba ilia aweze kukabidhiwa taarifa hizo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisi ya Waziri huyo, jijini Dodoma leo. Hata hivyo, Waziri Lugola alisema aliwahi kua mwanariadha, hivyo atahakikisha anasonga mbele kuendelea na safari, hata angalia nyuma.

PIX 4

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuaga aliyekua Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba, mara baada ya kukabidhiwa taarifa kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo. Hata hivyo, Waziri Lugola alisema aliwahi kua mwanariadha kipindi cha nyuma, hivyo atahakikisha anasonga mbele kuendelea na safari, hata angalia nyuma. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  

WANANCHI WA MIKUMI WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI

Posted by Esta Malibiche on july 10,2018 IN NEWS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Selemani Jafo akiongea viongozi wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
 Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Mikumi juu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais Magufuli ya ujenzi wa Kituo cha Afya.
 Ukaguzi wa jengo la zahanati inayotumika kwasasa eneo la Mikumi.

Wananchi wa Mikumi walipokuwa katika mkutano wa hadhara.
..................................
WANANACHI wa Mikumi wamemwagia sifa Rais Dk.John Magufuli kwa kusikia kilio chao cha kukosa huduma za afya.
 Wananchi hao wamemwaga sifa kwa Rais Magufuli wakati Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipombelea zahanati ya Mikumi na kuzungumza na wananchi wa mikumi.
 Katika ziara hiyo,Waziri Jafo amewataarifu wananchi hao kwamba serikali inaanza ujenzi wa kituo cha afya Mikumi ambacho kiliahidiwa na Rais Magufuli alipokuwa katika ziara mkoani Morogoro. 
 Kituo hicho kimeshapokea shilingi milioni 400 ambapo ujenzi wa majengo muhimu unatarajiwa kuanza ndani ya wiki moja kuanzia sasa kwa kutumia utaratibu wa force account. 
 Kufuatia habari hiyo, Wananchi wa Mikumi wameishukuru Sana serikali ya awamu ya tano kwamba Rais Magufuli na serikali yake imejipambanua katika kuwahudumia wananchi wanyonge.

TAASISI YA MO DEWJI YAIKABIDHI HOSPITAL YA MUHIMBILI MILL 125

Posted by Esta Malibiche on July 10,2018 IN NEWS

Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula akikabidhi mfano wa hundi ya Tsh. 125 Milioni kwa wawakilishi wa kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Fedha hizo zitatumika kugharamia matibabu ya watoto wenye saratani.


Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa Tsh. 125 Milioni kwa kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambazo zitatumika kugharamia matibabu ya watoto wenye saratani.


Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa Tsh. 125 Milioni kwa kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambazo zitatumika kugharamia matibabu ya watoto wenye saratani.



Meneja wa Wafadhili wa kituo cha Tumaini la Maisha, Alex Kaijage akitoa neon la shukrani baada ya kupokea msaada wa Tsh. 125 Milioni kutoka kwa Taasisi ya Mo Dewji ambazo zitatumika kugharamia matibabu ya watoto wenye saratani.


Baadhi ya watoto ambao wanapatiwa matibabu katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Baadhi ya watoto ambao wanapatiwa matibabu katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


NAMWANDISHI WETU

TAASISI ya Mo Dewji imetoa msaada wa Tsh. 125 Milioni kwa kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili kusaida kugharamia matibabu ya magonjwa ya saratani kwa watoto wanaopatiwa huduma katika kituo hicho.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo imekuwa ikitolewa na taasisi kwa kituo hicho.

Alisema wanatambua hali ngumu ambayo wanapitia watoto hao wanapouguza magonjwa ya saratani, hivyo wanaamini msaada huo utasaidia kuboresha huduma kwa watoto waliopo kituoni hapo na kuwezesha watoto waliopo mikoani kusafirishwa ili kufikishwa hospitalini na wao wapatiwe matibabu.

“Kama upo hai na mwanao anapumua, mshukuru Mungu kuwa ana makusudi na wewe na ana makusudi na mtoto wako. Usikatishwe tamaa na magonjwa, tunaamini kwamba watoto hawa watapona na kurudi nyumbani, watasoma na watalitumikia Taifa letu,

“Kama mnavyofahamu Mohammed Dewji amekuwa akifanya kazi na Tumaini la Maisha tangu mwaka 2012 ili kusaidia watoto kupatiwa matibabu, na kupitia taasisi yake tutaendelea kushirikiana ili kusaidia watoto wetu wapatiwe matibabu,” alisema Chengula.

Naye Meneja wa Wafadhili wa kituo cha Tumaini la Maisha, Alex Kaijage aliishukuru Taasisi ya Mo Dewji kwa msaada ambao wamekuwa wakiwapatia na kuwaomba kuendelea kuwa na moyo huo wa kusaidia matibabu ya watoto wenye saratani ili warejee katika hali ya kawaida na kuendelea na shughuli zingine ikiwepo kusoma.

“Tunajua kwamba tunahitaji sana sana hizi fedha kufanikisha matibabu ya hawa watoto, sio tu usafiri wa kutoka huko wanakotoka na kuja bali hata dawa ambazo tunazipata kwa sababu ya huu mchango ambao Mohammed Dewji ametuwezesha. Kwa sababu yenu watoto hawa wanapata matibabu, kwa sababu yenu wanapona kwahiyo tunawashukuru sana,” alisema Kaijage.

Kwa upande wa mmoja wa wazazi ambao mtoto wake anapatiwa matibabu katika hicho, Hamisi Samweli aliwataka wadau wengine wenye uwezo wa kifedha kuwa na moyo wa kusaidia kama anavyofanya Mohammed Dewji ili watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kifedha wapatiwe matibabu.