Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumamosi, 2 Desemba 2017

DEOGRATIUS NDEJEMBI;UVCCM MKOA WA IRINGA KUWENI WAZALENDO KWA KUTANGULIZA MASLAI YA CHAMA MBELE

Posted by Esta Malibiche on DEC 2,2017 IN SIASA
Deogratiuas Ndejembi mkuu wa wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma akizungumza na wajumbe wa umoja wa uvccm mkoa wa Iringa katika mkutano mkuu wa 9 wa uvccm mkoa,akitangaza matokeo ya wasshindi wa ngazi mbalimbali ikiwemo ya uenyekiti wa uvccm mkoa wa iringa,aliwasihi washindi  kuwa wazalendo kwa kutanguliza maslai ya chama na jumuiya ya vijana mbele pamoja na kukipigania chama ili kiendelee kushika hatamu.PICHA ZOTE NA ESTA  MALIBICHE.
Na Esta Malibiche
Iringa
UMOJA wa vijana ccm mkoa wa Iringa umeandika historia mpya kumpata Mwenyekiti wa jumuiya hiyo mara baada ya kukaa takribani miaka 4 bila Mwenyekiti wa Uvccm mkoa.

Akitangaza matokeo ya kura za Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa katika mkutano mkuu wa 9,Msimamizi mkuu wa uchaguzi Deogratius Ndejembi ,ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma,aliwasihi washindi wa umoja wa vijana ccm walioshinda katika ngazi mbalimbali za jumuiya hiyo i kuwa wazalendo kwa kutanguliza maslai ya chama na jumuiya ya vijana mbele pamoja na kukipigania chama ili kiendelee kushika hatamu.

Ndejembi alisema hakuna Taifa linalosonga mbele kimaendeleo pasipo kumtegemea kijana,hivyo aliwataka kuweka maslai ya chama mbele na wasikubali kutumika na watu kwa maslai yao binafsi hivyo kukivuruga chama na jumuiya ya Vijana.

"Kura zilizopigwa ni 294,halali 193 iliyoharibika ni kura 1.Amoni..kapata kura 7,Jafari kikoti kapata kura 45 na Kenani Kihongosi kapata kura 235.Hivyo basi kutokana na matokeo haya ninamtangaza Kenani Kihongosi kuwa ndiye Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Iringa.Uchaguzi umeisha kikichobaki ni kumpa ushirikiano,tuwe na sauti moja  juu ya maslai mapana ya jumuiya na chama"" Alisema Ndejembi.

Kwa upande wa Msimamizi msaidizi ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wawe viongozi wenye kuleta mabadiliko katika jumuiya,kujiepusha na makundi ambayo yanaweza kuwagawa vijana.

‘Msikubali kubezwa na vyama vya upinzani,tembeeni kifua mbele kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mwenyekiti wetu wa ccm Taifa Rais Magufuli’’Alisema Asiah na kuongeza kuwa

 ‘’Uongozi wa jumuiya ya vijana siyo ajira bali ni uzalendovijana  moja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umempata mwenyekiti mpya bwana Kenani Kihongosi alichaguliwa kwa kura nyingi za kishindo na kurudisha matumaini mapya ya kuanza safari ya kuijenga CCM mpya kwa vijana wa mkoa huu wa Iringa’’Alisema Asia

Nae katibu wa jumuiya ya umoja wa vijana ccm mkoa wa Iringa,Jemsi Mgego akitoa pongezi kwa washindi walioshinda katika ngazi mbalimbali za uongozi wa umoja huo alisema kazi kubwa ya uvccm ni kuwapika vijana  kwa imani na itikadi ya ccm,na kwa mtu yeyote atakae hubiri utengano na kuleta mpasuko ndani ya umoja wa vijana wa ccm basi hastahili kuwa kiongozi na kuwa mwanaccm.
""Huu sasa ni wakati wakujenga jumuiya imara na madhubuti ikiwa nipamoja na  kuvujna makundi ya uchaguzi na kuwa kitu kimoja  ili kuiletea hedhima jumuiya hii iliyopotoea  kwa miaka minne bila juwa na Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Iringa"" Alisema Mgego na kuingeza kuwa

""Mbele yetu tuna kazi kubwa ya kulikomboa jimbo la Iringa mjini,tukishirikiana kwa pamoja kama tulivyoshirikiana katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya kitwiru hakika tutafanikiwa na hatimae jimbo kurudi katika mikono ya chama cha Mapinduzi"" Alisema Mgego

Akiwashukuru kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Vijana ccm MKOA WA Iringa,Kenani Kihongosi alisema kuwa atahakikisha jumuiya zote za umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi zinarudi na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha wanapata wanachama wapya ambao itakuja kuwa nguzo ya chama hicho hapo baadae.

“Ninawashukuru wajumbe kwa kuniona kuwa ninafaa,ni miaka mine tumekaa kwa unyonge bila kuwa na Mwenyekiti,ninawaomba tushirikiane kwa pamoja katika kufanya kazi na kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyokusubiwa na kuhakikisha chama kinapata matokeo chanya kutoka kwetu vijana hivyo naomba mniunge mkono kuhikikisha tunakuwa wamoja” alisema Kihongosi

Kihongosi aliwataka vijana kufanya kazi na kuhakikisha wanaendelea kumuunga mkono Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuijenga CCM na Tanzania mpya.


“Sisi ndio vijana ambao tunatakiwa kuonyesha mfano kwa kufanya kazi na kuonyesha wapinzani wa mkoa wa Iringa kuwa sasa kuna UVCCM ambavyo inania ya kuhaikisha inaumaliza upinzani uliopo hapa mkoana na CCM ikachukua jimbo la Iringa Mjini” alisema Kihongosi
Deogratiua Ndujembi mkuu wa wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma akizungumza na wajumbe wa umoja wa uvccm mkoa wa Iringa katika mkutano mkuu wa 9 wa uvccm mkoa, alisema hakuna Taifa linalosonga mbele kimaendeleo pasipo kumtegemea kijana,hivyo aliwataka kuweka maslai ya chama mbele na wasikubali kutumika na watu kwa maslai yao binafsi hivyo kukivuruga chama na jumuiya ya Vijana.
Msimamizi msaidizi ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akizungumza alisema kuwa Uongozi wa jumuiya ya vijana siyo ajira bali ni uzalendovijana  moja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umempata mwenyekiti mpya bwana Kenani Kihongosi alichaguliwa kwa kura nyingi za kishindo na kurudisha matumaini mapya ya kuanza safari ya kuijenga CCM mpya kwa vijana wa mkoa  wa Iringa.

Msimamizi msaidizi ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akizungumza aliwataka viongozi waliochaguliwa kuwa wenye kuleta mabadiliko katika jumuiya,kujiepusha na makundi ambayo yanaweza kuwagawa vijana.
Katibu wa chama cha mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa Christopher Magala,akizungumza alisema,sasa ni wakati wakujenga jumuiya imara na madhubuti ikiwa nipamoja na  kuvujna makundi ya uchaguzi na kuwa kitu kimoja  ili kuiletea hedhima jumuiya hii iliyopotoea  kwa miaka minne bila juwa na Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Iringa.

katibu wa jumuiya ya umoja wa vijana ccm mkoa wa Iringa,Jemsi Mgego akitoa pongezi kwa washindi walioshinda katika ngazi mbalimbali za uongozi wa umoja huo alisema kazi kubwa ya uvccm ni kuwapika vijana  kwa imani na itikadi ya ccm,na kwa mtu yeyote atakae hubiri utengano na kuleta mpasuko ndani ya umoja wa vijana wa ccm basi hastahili kuwa kiongozi na kuwa mwanaccm.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa vijana ccm Mkoa wa Iringa,Kenani Kihongosi aliyechaguliwa  kwa kura 235 kati ya kura 294 kuiongoza jumuiya hiyo.










 




Ijumaa, 1 Desemba 2017

WAKAZI WA MTAA WA MJIMWEMA MAFINGA MJINI WAKO HATARINI KUKUMBWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Posted by Esta Malibiche on DEC 1,2017 IN NEWS

 Na Esta Malibiche
Mafinga

WANANCHI wakazi wa kitongoji cha Mbigili mtaa wa mji mwemakata ya Boma  Halmashauri ya mji wa  Mfinga ,Mkoani Iringa wameitaka Seriakali  kunusuru Afya zao ambazo ziko hatarini kukumbwa na  magonjwa ya mlipuko yakiwemo kuhara,kupindupindu kutokana na dampo kubwa la taka lililopo katika makazi yao Mjini Mafinga.

Akizungumza leo na blog hii ya KALI YA HABARI huku akitokwa na machozi Moi Mgoda  ambaye ni mkazi wa eneo huilo alisema Afya zao ziko hatarini kutokana na Halmashauri kushindwa kutoa hizo taka kwa wakati,huku wakazi hao wakikabiliwa na harufu mbaya,kuzagaa kwa taka hadi katika makazi yao Pamoja na nzi.


‘’Moja ya kero tunayoipata hapa ni kuzagaa kwa taka hadi mlangoni kwetu,harufu mbaya na kuja kwa nzi katika makzi yetu.Tunashindwa kuhimili hali hii inayohatarisha Afya ya familia yangu Pamoja na familia za weakazi wa eneo hili,pia watoto wadogo wanacheza katika dampo hili’’Alisema Mgoda

Aliongeza kuwa Pamoja na familia zao kuathirika kiafya pia dampo hilo lipo katika vyanzo vya Maji,maji yanayotumiwa na  wakazi wa Halmashauri hiyo,hali inayoweza kuleta athari kwa wakazi wa mji wa Mafinga kukumbwa na  magonjwa kutokana na  matumizi ya maji.

‘’Asilimia kubwa ya wananachi wamji wa Mafinga wanatumia haya maji,tena wengine hata hawachemshi na dampo lipo katika vyanzo vya maji pia kipindi hiki mvua zinanyesha na kila aina ya taka zinatupwa hapa.Tunaomba dampo hili liondolewe katika makazi ya watu na itafutwe eneo amabalo halina makazi ya watu ili kunusuru Afya za watanzania’’’Alisema Mgoda

Kwa upande wake Beatrice Nestory nae alisema,kero hii ya kulundikana kwa taka kunatokana na Halmashauri hiyo kukosa Gari la kuzolea taka,hata hivyo gazri inatosomba toaka kutoka majumbani au katika mitaa ni toyo dogo ambalo halikidhi mahitaji ya wakazi waHalmashauri ya Mji wa Mafinga.

‘’Sisi tumekuwa na kazi ya kuwafukuza watoto ambao wamekuwa akija na kucheza katika dampo hili, na kuokota vitu mbalimbali,kwa kweli ni sehemu hatari sana si kwa watoto tu bali pia kwa sisi watuwazima afya zetu zipo hatarini’’Alisema Beatrice
Jitihada za kumtafuta  Diwani wa Kata hiyo Julius Pius  ili kujua ni hatua gani alizozichukua kuhakikisha ananusuru maisha ya wakazi wa eneo hilo,zilifanikiwa nae alisema kuwa alifikishaa tarifa kwa Halmashauri ya Mji wa Mafinga,kuondoa dampo hilo eneo la makazi ya watu lakini mpaka sasa hakuna mafanikio yeyote.

Julius aliitaka Halmashauri ya Mji wa Mafinga kuchukua hatuia za haraka za kulihamisha dambp hilo kwa kuwa wananchi wake wakiwemo watoto wadogo wapo hatarini kukumbwa na magonjwa.

Ndugu Mwandishi wa habari kwa upendo kabisa ninaiomba Halmashauri ichukue hatua kulihamisha dampo hilo,ukiangalia lipo mjini kabisa na lipo katikakatik ya makazi ya watu ni hatari sana.Pia lipo kwenye vyanzo vya maji , na wananchi wanalima vinyungu ambavyo mboga za majani tunazokula hapa Mafinga zinazalishwa hapo,hali hii nimbaya sana,si nzuri kwa na nimejaribu kulalamika sana bila mafanikio’’Alisea Diwani
Alisema  kwa  aliwaita watu wa afya
  ambao huwa  anapenda sana  kuwashirikisha katika mambo mbalimbali ingawa majibu yao hayaridhishi.

‘’Siku moja wananchi walikuwa wameipigia simu wakinitaarifu juuya kero wanayoipata kutokana na dampo hilo,kwa bahati nzuri nilipoongea na mtu wa afya na mtendaji wangu wa kata akiwepo alinijibu dampo hilo limewekwa kwa muda  lakini cha ajabu mpaka leo hii bado lipo na linaendelea kuwepo bila kuangalia athari wanazozipata wakazi wa eneo hilo ‘’Alisema Diwani huyo na kuongeza kuwa

Mimi ni kiongozi si mwanasiasa na shughuli zangu napenda ziende kama kiongozi mahali ninapotetea umma ninapenda kuona hatua zinachukuliwa haraka.Kilio change hakijasilikizwa na mwenywe umeshuhudia  atahari kubwa kwa watoto wa shule na wananchi amabao wanaingia kule kuchambua vitu.

Huwa ninaumia sana ninapopeleka kilio kwa Hamashauri ambayo ndiyo Serikali yenyewe lakini inashindwa kuchukua hatua,ni vema sauti yetu ikapaa zaidi katika nagzi za juu uli hatua za haraka ziweze kuchukuliwa kuzoa taka na kuliondoa dampo ili kunusuru uhai wa wananchi  amabao wapo katika mazingira hatarishi,ambapo hali hii ikiendelea maafa makubwa yanaweza kutokea ya mlipuko wa magonjwa ya kuhara na kipindupindu.Alisema Diwani Julius Pius



BALOZI SEIF ALI IDDI AWATAKA WAISLAM KUIMARISHA IMANI

posted by Esta Malibiche on DEC 1,2017 IN NEWS
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewataka Waislam nchini kote kuwa waadilifu kama alivyokuwa Mtume Muhammad (S.A.W).
Amesema ni vema wakatumia wakati huu wa Maulid kutathmini mienendo ya maisha yao kwa kujiuliza kama maisha wanayoishi  yanafanana na yale aliyoishi Mtume Muhammad.
Balozi Seif ameyasema hayo leo (Ijumaa, Desemba Mosi, 2017) alipokuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) lililofanyika kitaifa wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi.
“Kuna vigezo vingi mja anaweza kuvitumia wakati anapojitathmini, ambavyo ni pamoja na tabia ya Bw Mtume ya uadilifu na  wake. Tujiulize kati yetu hapa ni wangapi waadilifu na waaminifu kama alivyokuwa Bw. Mtume.”
Amesema kupungua kwa uaminifu na uadilifu ndiko kulikomfanya Rais Dkt. John Magufuli mara baada ya kuingia madarakani kuanzisha vita dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi, hivyo wanatakiwa kumuunga mkono.
 “Mtume (S.A.W) aliikemea sana rushwa na akasema kuwa amelaaniwa na Mwenyezi Mungu mwenye kutoa na kupokea rushwa na hata Yule mpiga debe. Pia tunaamini kuwa dini zote duniani zinapinga rushwa, hivyo tuiiepuke” 
Awali, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Bin Zubeiry alisema aliwaasa Watanzania wote waendelee kuidumisha na kuitunza amani kwa sababu hakuna maendeleo yoyote yatakayopatikana bila ya kuwepo kwa amani.
Alisema suala la kudumisha amani, kuheshimiana na kushirikiana miongoni mwa waislamu na wasiokuwa waislam limehimizwa sana katika dini ya kiislam na dini nyingine, hivyo wananchi hawana budi kuendeleza.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimpongeza Sheikh Mkuu kwa uongozi wake mzuri wa  Baraza la WaislamTanzani (BAKWATA) ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na dini zote bila Ubaguzi.
Alisema serikali itaendelea kufanya kazi na dini zote na kwamba Rais Dkt. Magufuli amezipa kipaumbele shughuli za dini zote ziendelee kufanyika nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika Baraza la Maulidi ya  Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika kwenye  uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani Rungwa Desemba 1, 2017. Mgeni Rasmi katika Maulidi hayo alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Baraza la Maulidi ya  Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika kwenye  uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani Rungwa Desemba 1, 2017. Mgeni Rasmi katika Maulidi hayo alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Mufti Mkuu wa Tanzania,  Sheikh Aboubakar Zubeiry akizungumza katika Baraza la Maulidi ya  Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika kwenye  uwanja wa Shule ya Msingi ya Likangala wilayani Rungwa Desemba 1, 2017. 
Baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati alipohutubia   kwenye uwanja wa  Shule ya Msingi ya  Likangala wilayani   Ruangwa Desemba 1, 2017.

RITTA KABATI AKABIDHI MIFUKO 50 YA SARUJI KWA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA IRINGA

Posted by Esta Malibiche on DEC 1,2017 IN NEWS


MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi  CCM Ritta Kabati akikabidhi mifuko ya sumenti kwa wanafunzi wa shule ya Iringa Girls akiwa sambamba na diwani wa Kata ya Nduli Bashir Mtove



MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati amechangia kiasi cha mifuko ya saruji 50 kwa shule ya sekondari ya Iringa Girls iliyoko katika manispaa ya Iringa kutokana na uhaba wa baadhi ya majengo ya shule hiyo.

Akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iringa Girls Kabati alisema kuwa ameamua kujitolea kutoka kwenye posho yake kuhakikisha elimu kwa wanafunzi wa shule zilizopo mkoani Iringa wanasoma na wanapa elimu iliyo bora kutokana na ubora wa miundombinu iliyopo.

“ Nimetembelea shule nyingi mkoani kwetu hasa za msingi kuweza kuangalia miundo mbinu na majengo yake kwa kweli hali inatisha na majengo mengi yamekuwa chakavu hivyo nitajitahidi kwa kushirikiana na wadau wa elimu kuweza kukarabati yaendane na hali ya sasa ya kuwa bora zaidi” alisema Kabati

Hadi sasa Kabati amekwisha fanya ukarabati kwa shule za msingi za Azimio, Kihesa,Mtwivira na shule ya Kibwabwa ambazo alizitembelea na kubaini uchakavu mkubwa wa majengo na miundo mbinu mibaya na shule nyingine alizoahidi kuzifanyia ukarabati ni shule ya msingi Gangilonga.

Kwa upande wake mwalimu wa shule hiyo Bazila Kondo alimushukuru mbunge huyo kwa msaada wake alioutoa kwa kuwa utawasidia kujenga majengo ya mabweni ya wanafunzi hapa ambayo imekuwa ikiwasumbua na kuongeza mlundikano kwa wanafunzi mabwenini.

“Tulikuwa tunasherekea jubilee ya shule hivyo mgeni rasmi alikuwaMheshimiwa Joyce Ndalichako  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi  na Katika ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe  Amina Masenza, Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Bi wamoja Ayoub, Wakuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Jamhuri David na Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela,Pia wabunge waheshimiwa, Ritta Kabati, Zainab Mwamwindi na Mch Peter Msigwa hivyo mbunge kabati ametimiza ahadi yake”alisema Kondo

Kondo alisema lengo la shule ni kuhakikisha wanajenga jingo la bweni jipya la wanafunzi pamoja na kujenga vyoo viwili vya wanafunzi wenye mahitaji maalum

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI-DESEMBA 1, 2017

Posted by Esta Malibiche on DEC 1,2017 IN NEWS

 Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa serikali wakipokea maandamo (hayapo pichani) wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam
 Wananchi wakiwa  kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi wa Uragibishi na Habari kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Jumanne Issango.
 Wanachi wakipima shinizo la Damu wakati wa maadhimisho hayo.
 Mratibu kutoka Shirika lisilo la kiserikali Voice of African Mothers Tanzania (VAM-TZ), Bi Mary Makinda akimuelezea  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan huduma wanazotoa za mapambano ya Ukimwi alipotembelea mabanda katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Richardi Ngirwa akimuelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kuhusiana elimu wanazotoa kwa wanachi  dhidi ya maambukizi Ukimwi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) alipotembelea banda hilo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Msanii wa nyimbo za uswahilini, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu  akitoa burudani katika maadhimisho hayo.

SALAM MBALIMBALI ZA SIKUKUU YA MAULID

Posted by Esta Malibiche on DEC.1,2017 IN NEWS

Naitwa Esta Malibiche,ambae ni mmiliki wa blog hii ya KALI YA HABARI,ninaungana na watanazania wote,kuwatakia heri  waislam wote katika kusherekea  sikukuu ya Maulid Al-Nabi Tusherekee kwa Amani na Utulivu huku tukiwakumbuka wahitaji,upendo utawale katika famili na Taifa kwa ujumla.Pia tuiombee Amani nchi yetu ya Tanzania na tuwaombee viongozi wetu wa vyama na Serikali.Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania.AHSANTENI