Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumapili, 26 Februari 2017

KERO YA UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA ILIYOKUWA INAWAKABILI WANANCHI WA MTAA WA IGUNGANDEMBWE MANISPAA YA IRINGA YATATULIWA

Posted by Esta Malibiche ob FEB 27,2017 IN NEWS

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akikinga maji kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji kimefunguliwa na kuanza kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa akiwa na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa kujimba visima ambaye pia ndiye aliyechimba kisima hicho. 
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wakitumia wananchi wa mtaa huo
Maji yaliyokuwa yakitumiwa awali na wananchiwa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa kabla ya kujimbiwa kisima 



Wananchi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama.

Wakizungumza na blog hii wananchi hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na tatu (53) hawajawahi pata maji masafi na salama.

“Angalia maji haya machafu ndio tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa anatusaidia tu kutuepusha na magonjwa mbalimbali kiukweli leo tunafuraha sana kuanza kutumia haya maji na ndio maana unaona wananchi wanafuraha nawameanza kunywa maji hapa hapa kwenye kisima hiki kwa kuwa bado hawaamini kilichotokea”,walisema wananchi.

Wananchi wao wamemuomba mbunge Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove kuendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) alisema kuwa wataendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa kuwa yeye ni mbunge wa wananchi wote bila kubagua vyama.

Kabati alisema kuwa ataendelea kuwachimbia visima na kukarabati majengo ya shule zilizochakaa katika mkoa wa Iringa kwa kuwa yeye ni mbunge wa mkoa wa Iringa hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kuiamini serikali ya chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli.

“Hivi hamuoni nimeamua kufika huku ambako hata viongozi wengi hawajafika ila mimi nimekuja nimewaleta kisima na maji safi na nitaendelea kuja kutatua matatizo ya mtaa huu kwa kuwa tumetumwa na Rais kufanya kazi kwa wananchi wa chini ndio maana hata mimi nimeanza kufanya kazi huku mbali japo kuwa ndio jadi yangu kuwatumikia sana wananchi wa chini sasa naombeni mniunge mkono katika juhudi zangu za kuwaletea mandeleo”.alisema Kabati

Aidha Kabati alisema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuleta maendeleo kuanzia huku chini kupanda juu hivyo tufanye kazi kwa kujituma ili tuende sambamba na kasi ya Rais wetu.

Naye Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove alimshukuru mbunge huyo kwa jihada zake za kuleta maendeleo na kumuomba kushugulikia changamoto alizozitoa kwa wananchi ili kuendelea kujijengea imani kwa wananchi wa kata hiyo.Mtove aliongeza kuwa atahakikisha kata yake inamaliza tatizo la maji ambao limetumu kwa miaka mingi hivyo wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa kujituma ili kukuza uchumi wa kata hiyo.

“Angalia hadi saizi tumechimba visima zaidi ya sita kwenye kata yangu japo bado sana kumaliza tatizo hili la maji hivyo naendelea kujituma kutafuta marafiki,wafadhili na kumshirikisha mbunge Kabati kusaidia kutatua tatizo la maji na changamoto nyingi ili wananchi wangu wafanye kazi kwa kujituma bila kuwa na vikwazo vyovyote vile vya kiafya”.alisema Mtove.

UTOAJI TAARIFA ZA MIRADI YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA UMMA UNAVYOSAIDIA KUPAMBANA NA RUSHWA

Posted by Esta Malibiche on FEB 27,2017 IN NEWS

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Serikali imeweka kipaumbele kikubwa katika  ujenzi wa miundombinu ya Umma  kwani ni muhimu kuwa na miundombinu mizuri na bora ili kutoa huduma bora na kurahisisha ufanyaji kazi hivyo kuharakisha maendeleo ya nchi katika nyanja zote muhimu zikiwemo za biashara, utalii na mawasiliano.

Matumizi makubwa ya fedha za Serikali yanatumika katika ujenzi wa miundombinu ya Umma ambapo matumizi hayo yanahusisha karibu asilimia 53 ya Bajeti nzima ya nchi.

Miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Umma inayoelezewa hapa ni ile ambayo inajengwa kwa fedha za Serikali kwa ajili ya matumizi ya wananchi wote ikiwemo ya barabara, hospitali na vituo vya afya,shule na vyuo,nyumba za kuishi pamoja na ofisi mbalimbali. 

Ingawa Serikali inajitahidi kuhakikisha nchi inakuwa na miundombinu bora itakayochochea maendeleo, lakini jitihada hizo zimekuwa zikikwamishwa na changamoto mbalimbali zinazojitokeza pindi mradi husika unavyoanza kwani wahusika hawatumii fedha kama zilivyopangwa na badala yake wanafanya kwa makadirio ya chini na kufanya ujenzi kutokuwa imara.

Hali hiyo inasababisha Serikali kupata hasara kwa kupoteza fedha nyingi na kuambulia kubaki na majengo yasiyo na viwango ambayo mwisho wake hushindwa kutumika na kuilazimu Serikali kuanza upya ujenzi husika. 

Kwa kuwa Serikali hii ni sikivu na imejipanga kuhakikisha nchi inafika katika uchumi wa kati basi mambo hayo hayana nafasi na hayawezi kutokea tena katika nchi hii watu kuachiwa huru kutumia vibaya fedha za Umma zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. 

Kwa kuhakikisha hilo,Serikali kupitia Baraza la Ujenzi la Taifa (NCC) chini ya Mkakati wa Kukuza Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Ujenzi Tanzania (CoST-Tanzania) imejipanga kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta hiyo ili kuondokana na rushwa pamoja na ubadhilifu wowote wa fedha za Umma zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo.

Mkakati huo unalengo la kupambana na rushwa, usimamizi mbaya katika ujenzi pamoja na changamoto zingine zinazopelekea ubadhilifu wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya miundombinu ya Umma kwa kukusanya taarifa za miradi hiyo ya ujenzi ili  kuhakikisha kama thamani ya miundombinu iliyojengwa inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi husika. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,(Ujenzi), Mha. Joseph Nyamuhanga alikaririwa akisema kuwa “Sekta ya Ujenzi ni sekta moja wapo inayoonekana kukithiri kwa rushwa duniani kwa sababu takribani asilimia 10 hadi 30 ya Bajeti yake inapotea kwa njia ya rushwa na usimamizi mbaya hivyo ili kuondoa dhima hii ni lazima kukusanya na kutoa taarifa kwa wananchi juu ya ujenzi wa miundombinu hiyo”.

Mha. Nyamuhanga aliongeza kuwa ni muhimu CoST-Tanzania ikapewa hadhi ya kujitegemea na kuwa na madaraka yake kwani ni kitengo ambacho ni muhimu na kinafanya kazi kubwa ya kuchochea uwepo wa uwazi na uwajibikaji katika miradi ya ujenzi.

Akifungua mkutano wa wadau wa ujenzi kutoka nchi mbalimbali uliofanyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi), Mha. Leonard Chamuriho alisema rushwa inazungumzwa sana katika suala la ujenzi wa miundombinu ya umma hivyo huu ni wakati wa kuweka wazi taarifa za ujenzi wa miundombinu hiyo ili wananchi waelewe kinachoendelea katika miradi inayotumia fedha zao.

Aliongeza kuwa kufanya hivyo kutaisaidia Serikali kupambana na rushwa na hivyo kufuta kabisa taswira ya rushwa katika miradi hiyo kwani msimamo wa Serikali ni kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa.

Maendeleo ya nchi yanachangiwa na wananchi wenyewe kwa njia ya ukusanyaji wa kodi na ushuru mbalimbali hivyo hata miundombinu ya umma inajengwa kwa kutumia fedha za wananchi zinazopatikana kwa njia ya ukusanyaji mapato.

Hivyo, ili kuifanya Serikali kuwa na taswira nzuri kwa wananchi wao pamoja na kuwafanya wananchi kuiamini Serikali yao ni vizuri kuwapa taarifa juu ya matumizi ya fedha hizo wanazozikusanya.

Kuwapa taarifa wananchi juu ya miradi mbalimbali haswa ya ujenzi wa miundombinu kutaamsha ile hali ya watu kuona umuhimu wa kulipa kodi kwa sababu watajua matumizi ya fedha wanazozikusanya.

Taarifa hizo pia zitaendeleza uwajibikaji na uwazi katika ujenzi wa miundombinu hiyo hivyo kupunguza vitendo vya rushwa,kujenga miundombinu inayoendana na thamani ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi husika pamoja na kujenga miundo mbinu bora na imara.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema kuwa shughuli inayofanywa na CoST- Tanzania inalenga kuimarisha uwazi katika sekta ya ujenzi kwa kutoa taarifa juu ya ujenzi wa miundombinu ya Umma kitu ambacho kitasaidia kutambua uwezo, akiba pamoja na ufanisi wa majengo hayo.
"Kazi inayofanywa na CoST- Tanzania ni fursa kwa Serikali na Umma kwa ujumla kufuatilia jinsi fedha za Umma zinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ambapo ukweli na uwazi wa taarifa zinazokusanywa zitasaidia katika kupunguza rushwa na kuboresha usimamizi wa miundombinu hiyo, " alisema Waziri Kairuki.
Nae Mwenyekiti wa CoST-Tanzania, Mha. Kazungu Magili alieleza kuwa utoaji wa taarifa hizo kwa Umma kuhusiana na miradi ya ujenzi ya Umma itaruhusu umma kujua hali ya miradi mbalimbali hivyo kuifanya Serikali kuwa na sifa nzuri mbele ya wananchi.
CoST-Tanzania imejipanga kufanya tathmini ya miradi ya ujenzi isiyopungua kumi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja, majengo yaliyojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) hasa ujenzi mpya wa hosteli  za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia majengo yanayojengwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF ) pamoja na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Ni muhimu kwa Serikali kupitia miradi yote iliyojengwa na inayoendelea kujengwa kwa kutumia fedha za Umma ili kugundua thamani halisi ya majengo hayo na kutoa taarifa kwa wananchi.

Jambo hili pia litasaidia vyombo husika vya kisheria kuwachukulia hatua watu wote walioshiriki kutumia vibaya fedha za wananchi kwa kujenga miundombinu iliyo chini ya kiwango au isiyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi husika.

Alhamisi, 16 Februari 2017

KONGAMANO LA UTAFITI LA KISAYANSI LA BONDE LA ZIWA VICTORIA

Posted by Esta Malibiche on FEB 16,2017 IN NEWS

K1
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leonard Chamuriho (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Bi. Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), katika  maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza.
K2
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leornard Chamurho (kushoto), akifurahia maelezo yanayotolewa na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Bi. Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza.
K3
Mhandisi Diana Munubi (wa kwanza kulia) akitoa maelezo yaliyomfurahisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dtk. Leonard Chamurho (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustine Kamuzora, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo na Afisa Usafirishaji Mkuu wa Uchukuzi, Alphonce Mwingira katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza.
K4
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) kutoka taasisi za TAA, TCAA, TMA na DMI wanaoshiriki kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, linalofanyika Mwanza, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamurho, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Prof. Faustine Kamuzora, na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
K5
Dkt. Frank Mgeta wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure (kulia), akipata maelezo mbalimbali yanayohusu mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, jijini Mwanza.
K6
Raia wa Kenya, John Osodo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi (kulia) alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika Jijini Mwanza.

MBUNGE WA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE AFANYA ZIARA JIMBONI,ATEMBELEA MRADI MKUBWA WA DARAJA LA GALAMBA

Posted by Esta Malibiche on FEB 16,2017 IN NEWS

 Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumatano Februari 15,2017 ameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuangalia miundo mbinu iliyopo katika jimbo hilo.
Siku ya kwanza ya ziara ya mbunge huyo ilikuwa katika kata ya Kolandoto,Ibadakuli,Shinyanga Mjini,Kambarage na Ngokolo. 
 
Mheshimiwa Masele alikuwa ameambatana na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi pamoja na wataalam kutoka idara mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga. 
 
Mheshimiwa Masele ametembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja lililopo katika kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga ambalo lipo kati mto mkubwa maarufu kwa jina la ‘Mto Simba’. 
 
Mbunge huyo pia amejionea jinsi barabara ya kutoka barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza kwenda hospitali ya Kolandoto ilivyokatika na kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Kolandoto. 
 
Ziara ya Mbunge Masele pia ilifika katika masoko makubwa yaliyopo katika jimbo hilo ikiwemo soko la Kambarage lililopo kata ya Kambarage,Nguzo Nane lililopo kata ya Shinyanga mjini,soko kuu la mkoa wa Shinyanga na soko la Mitumba maarufu ‘Ngokolo Mitumbani’ lililopo kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga. 
 
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo katika ziara hiyo ametuletea picha 44 za matukio yaliyojiri kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ziara ya Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele.
Hapa ni katika Barabara ya Kolandoto- Wami ambayo inatoka katika barabara kuu ya Shinyanga- Mwanza-Kushoto ni Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akimuonesha mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele (wa pili kushoto) jinsi barabara hiyo ilivyomong’onyoka hali inayotishia kukatika kwa barabara hiyo inayoelekea katika hospitali ya Kolandoto.
Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akiendelea kutoa maelezo ingawa hata hivyo mbunge Masele aliahidi kutengenezwa/kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango kwa fedha za mfuko wa jimbo la Shinyanga mjini wakati wanafanya utarabu wa kujenga barabara hiyo katika kiwango cha lami.
Hapa ni katika Ofisi ya CCM Kata ya Kolandoto-Aliyesimama ni Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akizungumza wakati akimkaribisha mheshimiwa Masele aweze kuzungumza na baadhi ya wananchi wa kata hiyo huku akibainisha kuwa ziara hiyo inalenga kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
Diwani wa Kata ya Kolandoto mheshimiwa Agnes Machiya ambaye pia ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga akielezea changamoto ya gharama kubwa za matibabu katika hospitali ya Kolandoto hali inayosababisha wananchi wa eneo hilo wakose huduma ya afya kama inavyotakiwa matokeo yake kulazimika kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma hiyo katika kituo cha Afya Kambarage au Zahanati ya Galamba.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi wa kata ya Kolandoto ambapo alisema ziara hiyo siyo ya siasa bali ni kiutendaji.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) alieleza kukerwa na changamoto ya gharama kubwa ya matibabu katika hospitali ya Kolandoto na kuahidi kuzungumza na mamlaka zinazohusika ili kumaliza tatizo hilo.Mheshimiwa Masele pia alisema serikali/Chama Cha Mapinduzi kinafanya jitihada zote ili kuhakikisha kuwa wananchi wa kata ya Kolandoto wanapata huduma ya maji safi na salama.
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya akimwelezea Mheshimiwa Masele changamoto zilizopo katika kata hiyo
Mkazi wa Kolandoto Kadesha Noniyaza akielezea kero ya maji katika kijiji cha Wami na Mwanubi 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi katika Senta ya kijiji cha Galamba kilichopo katika kata ya Kolandoto baada ya kumuomba asimame wamwelezee changamoto zinazowakabili ambazo ni maji na uhitaji wa daraja katika mto Simba
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wananchi hao na kuwaeleza namna serikali inavyojitahidi kuhakikisha kuwa kero zao zinamalizika
Hapa ni katika Mto Simba ambapo mradi wa Ujenzi wa Daraja lililopo katika kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga unaendelea.Pichani ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akiangalia upande wa pili wa daraja linalojengwa na Mkandarasi M/S Pasons Co.Ltd tangu mwezi Juni mwaka 2016 na unatarajia kukamilika mwezi Machi mwaka 2017.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akiangalia daraja hilo ambalo mpaka kukamilika kwake jumla ya shilingi milioni 429.8 zinatarajiwa kutumika. 
Mmoja wa wataalam katika ujenzi huo akimwelezea mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele namna ujenzi huo unavyoendelea. 
Daraja hilo lina urefu wa mita 26 na upana wa mita 8
Ujenzi wa daraja ukiendelea
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishindilia zege kwa kutumia mashine kwenye daraja hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza kwenye daraja la Galamba ambapo alisema ujenzi huo wa daraja ambalo litaboresha mawasiliano katika kata ya Kolandoto na manispaa ya Shinyanga kwa ujumla ni miongoni mwa ahadi ambazo aliahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya (CCM) akizungumza ambapo alisema mradi huo unatekelezwa kupitia mfuko wa barabara ‘Road Fund’ huku akiongeza kuwa daraja hilo litaunganisha wilaya ya Shinyanga,Wilaya ya Kishapu na Meatu na kwamba kabla ya ujenzi huo eneo hilo lilikuwa kero hasa wakati wa masika
Mkandarasi George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd akielezea mradi huo wa daraja ambapo alisema mpaka sasa ameshakamilisha ujenzi wa vitako vyote vya daraja na ujenzi wa kuta/nguzo zote za daraja na kwamba anaendelea kutengeneza kindanda cha daraja ya upande mmoja na kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 75.
Muonekano wa daraja hilo
Ujenzi unaendelea
Muonekano wa daraja na eneo ambapo mto Simba unapita
Mheshimiwa Masele akiteta jambo na Mkandarasi George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd
Hapa ni katika Shule ya Msingi Bugweto iliyopo kata ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga-Wanafunzi na walimu wakimpokea mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akimtambulisha Diwani wa viti maalum (CCM) kata ya Ibadakuli mheshimiwa Zuhura Waziri (katikati) na diwani wa kata ya Kolandoto mheshimiwa Agnes Machiya (CCM) ambaye pia naibu meya wa manispaa ya Shinyanga
Mheshimiwa Masele akizungumza katika shule ya msingi Bugweto na kuwataarifu wanafunzi na walimu wa shule hiyo kuwa ametoa mifuko 100 ya saraji kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo ambayo yamechakaa na hayana sakafu sambamba na ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Bugweto
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa ndani ya darasa la saba katika shule ya msingi Bugweto
Darasa likiwa lina kokoto na vumbi sakafuni
Hapa ni katika Soko la Kambarage kata ya Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga.Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasili katika soko hilo kwa ajili ya kuzungumza na wafanyabiashara 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akisalimiana na mfanyabiashara katika soko la Kambarage katika manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko la Kambarage na kuwaeleza kuwa serikali ina mpango wa kujenga upya soko hilo hivyo kuwaomba wafanyabiashara wakae na viongozi wao na manispaa ya Shinyanga waangalie eneo ambalo litatumika wakati wakipisha ujenzi wa soko hilo pia kuangalia mazingira mazuri ya wafanyabishara hao kurudi na kuendelea na biashara katika soko hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiteta jambo na katibu wa soko la Kambarage Daudi Kitila( wa kwanza kulia)
Hapa ni katika eneo la Stendi Mpya ya Mabasi Mjini Shinyanga ambapo ujenzi wa choo cha stendi hiyo unaendelea.Katikati ni Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akielezea ujenzi wa mfumo wa majitaka unaoendelea katika eneo hilo
Hapa ni katika soko la Nguzo Nane kata ya Shinyanga Mjini-Mheshimiwa Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akisikiliza na kujibu kero za wafanyabishara katika soko hilo.Kero kubwa iliyotolewa ni ushuru mkubwa kwa mazao ambapo Masele aliahidi kukutana na uongozi wa manispaa ya Shinyanga kufuatilia kero hiyo na namna ya kuitatua
Ndani ya Soko Kuu la Mkoa wa Shinyanga.Mheshimiwa Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo,kero kubwa ikiwa ni soko hilo kukosa wateja kutokana wafanyabiashara na wateja kukimbilia katika soko la Nguzo Nane na Kambarage
Hapa ni Ngokolo Mitumbani,kwenye soko la Mitumba lililopo kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga.Mheshimiwa Mbunge akishangaa namna mabanda yalivyo wazi kutokana na wafanyabiashara kukimbia soko hilo na kufanyia biashara zao katika maeneo mengine mjini Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wafanyabiashara wa nguo za mitumba katika soko la Mitumba,maarufu Ngokolo Mitumbani katika kata ya Ngokolo.
Mfanyabiashara wa Mitumba akielezea jinsi soko hilo lilivyokosa wafanyabiashara kutokana serikali kuruhusu masoko kila mahali mjini Shinyanga
Vibanda vikiwa havina nguo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akijadiliana na wafanyabiashara hao namna ya kurudisha wafanyabiashara waliokimbia 
 
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog