Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumatano, 23 Machi 2016

SALIM ASAS AJITOLEA KUMUUNGA MKONO RAIS DK. MAGUFULI VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA ,ASAIDIA KUHUDUMIA WAATHIRIKA


Baadhi ya  vijana  walikuwa  wakitumia dawa  za  kulevya kwa  sasa  wameacha
 
Mlezi  wa kituo  hicho  cha Iringa Sober Hous Bw Godwin Msillu  kushoto  akiwa na baadhi ya  vijana  waliokuwa  watumiaji wa dawa za kulevya ambao  wanaishi  kituoni hapo
 
Shadrack
John ambae ni  anaishi  kituo  cha Iringa  Sober House aliyetoka  mkoa  wa Arusha  akijisomea Biblia baada  ya  kuachana na matumizi ya  dawa  za kulevya 
 
 Na MatukiodaimaBlog.
KAMANDA  wa  umoja  wa vijana  wa chama  cha mapinduzi (UVCCM)  mkoa  wa  Iringa Bw Salim Asas ameunga  mkono  kwa vitendo mapambano ya vita  dhidi ya madawa ya kulevya  nchini  yaliyoanzishwa na  Rais Dr  John Magufuli kwa kusaidia uanzishwaji  wa   kituo  cha kusaidia waathirika  wa madawa ya kulevya  mkoani hapa.
 
Bw Asas  ambae  wakati  wa kampeni   za uchaguzi  mkuu alipata  kuweka bayana  mkakati  wake  wa kusaidia vijana   walioathiriwa na matumizi ya madawa  ya  kulevya  ameungana na  kituo  cha Iringa Sober  House kilichopo Semtema katika Manispaa ya  Iringa  kuwasaidia  vijana  hao ambao  afya  zao zimeathiriwa na madawa ya  kulevya kwa kuwakusana na kuwapatia  tiba.
 
Akizungumza na mtandao  wa Kali ya Habari   Dr Alli Ngalla ambae ni Mkurugenzi  wa NGOs  ya Foundation for ellevition of drug eddiction anda sufferings (FADAS) wameanzisha kituo cha  kutoa  huduma kwa waathirika wa madawa ya  kulevya  cha  Iringa Sober House ambacho  kimeanza kufanya kazi chini ya  ufadhili mkubwa  wa Bw  Asas .
  
Alisema kuwa kituo  kituo  hicho   toka  kimefunguliwa  kina  zaidi ya  mwezi mmoja  ambapo  jumla ya  wategemezi 7 ambao  wanahudumiwa katika  kituo hicho pamoja na  wasimamizi  watatu ambao pia  walikuwa ni  watumiaji wa dawa  za kulevya ambao kwa sasa  waliacha .
 
Kwa  kweli  kuendelea  kwa  kituo  hiki  kumechangiwa kwa karibu na Salim Asas ambae amekuwa bega kwa  bega  kuona  vijana  walioathirika na madawa ya kulevya    wanasaidiwa na anachofanya  salim pia ni  kumuunga mkono Rais Dr Magufuli  ambae ametangaza  vita   dhidi ya madawa ya kulevya ……hivyo bado  tunaomba   wadau  wengine   kujitokeza kusaidia mapambano haya  ya  kunusuru afya  za  vijana  wetu “alisema Dr Ngalla.
 
Kuwa  lengo la  kituo  kuweza  kuwahudumia   waathirika  wa madawa ya  kulevya  kutoka  mikoa mbali mbali nchini hasa  wamelenga  kuwafikia vijana wa mkoa  wa Mbeya, Njombe , Ruvuma na Iringa japo  tafiti zinaonyesha  mkoa  wa Mbeya  ndio  unaongoza kwa matumizi ya madawa ya  kulevya 
 
Msimamizi  wa  kituo   hicho Bw Godwin Msillu alisema  kuwa mkakati  wa  kuanzisha  kituo   hicho  ulitokana na  mkakati  wa NGOS  ya  FADAS ambao  walikuja na mpango  wa kuanzisha kituo hicho .
 
Alisema  kuwa kati ya  waathirika  wa dawa za kulevya ambao  wapo  kituoni  hapo  baadhi yao ni kutoka  mkoa  wa Arusha na  kuwa  kumekuwepo  na mafanikio makubwa kwa  walengwa hao afya  zao  kuanza  kuimarika na  hivyo kuwataka   vijana  wengine  walioathirika  na  dawa  za  kulevya  kutosita  kufika   kituoni hapo  ili  kusaidiwa zaidi.
 
Akizungumza  kwa niaba  ya  wenzake walioathirika na madawa ya kulevya Bw  Shadrack John alisema  kuwa amepata  kufika  mkoani Arusha  kuja  kupatiwa  huduma  hiyo  na kuwa kwa sasa hali  yake  inaendelea  vizuri  zaidi.
 

Msaada wa Matibabu ya Mtoto EBENEZA PEMBE anasumbuliwa na Kansa ya Ngozi

Msaada wa Matibabu ya Mtoto EBENEZA PEMBE anasumbuliwa na Kansa ya Ngozi

Mama ROIDA MUHAMA mkazi wa Mkimbizi mjini Iringa, anamuuguza mwanaye aitwaye EBENEZA PEMBE anayesumbuliwa na saratani ya ngozi kwa miaka sita sasa.
 
Anaomba msaada wa hali na mali ili aendelee kumtibia mwanaye, Anahitaji kiasi cha fedha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuendelea na matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
 
Kwayeyote atakayeguswa tuma mchango wako kwa njia ya M-pesa 0767834377 au Tigo pesa 0717353529 kwa SILVANUS KIGOMBA au 0762 174 573 ROIDA MUHAMA (Mama wa Ebeneza)
Mtoto EBENEZA PEMBE anayesumbuliwa na Kansa ya Ngozi kwa zaidi ya Miaka 6 anahitaji Msaada wa fedha zitakazo muwezesha kwenda kupatiwa Matibabu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mtoto EBENEZA PEMBE aliyevaa shati la Bluu akiwa amebebwa na Mama yake Mzazi Bi ROIDA MUHAMA mkazi wa eneo la  MKIMBIZI manispaa ya Iringa, kushoto ni mtoto mwingine wa Bi ROIDA wakiwa katika Picha ya Pamoja.
……………….

Nimeguswa na maumivu na mateso anayoyapata mtoto Ebeneza kwa zaidi ya miaka 6 nimejitolea kusaidia kusambaza taarifa za Ugonjwa wake ili kukusanya michango kwaajili ya matibabu yake. 
 
                     Naomba ushirikiano wenu rafiki zangu na Mungu awabariki sana.

MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU CHINI YA UNESCO YAZINDULIWA CHUO KIKUU HURIA, DAR

MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU CHINI YA UNESCO YAZINDULIWA CHUO KIKUU HURIA, DAR

Faith Shayo - Unesco, Tanzania
Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (hayupo pichani) kufungua rasmi mafunzo ya Tehama kwa walimu nchini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
MAFUNZO kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yamefunguliwa katika maabara za Chuo Kikuu Huria jijini Dar es salaam.
Mafunzo hayo yanayohusisha walimu kutoka Vyuo vya Monduli, Tabora na Morogoro yamelenga kuoanisha ufundishaji na matumizi ya Tehama katika program ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya kuboresha elimu Tanzania kupitia ufadhili wa taifa la China.
Programu hiyo inayotoa ushirikiano mpya kati ya China na shirika hilo la Umoja wa Mataifa inafanyakazi katika mataifa manane ya kusini mwa jangwa la sahara inatekelezwa kwa lengo la kuwezesha mafanikio kwa malengo ya 2030.
Nchi zinaozhusika na mpango huo ni Tanzania Kongo ya Kinshasa (DRC), Congo, Liberia, Uganda, Côte d’Ivoire, Ethiopia na Namibia.
Mpango huo ambao kwa ujumla wake , awamu ya kwanza na ya pili unachukua miaka minne umelenga kuwezesha vyuo vya walimu kutoa walimu wa kufunza wenzao kwenye stadi za kufundisha kwa kutumia Tehama.
Mradi huo unaojulikana kama UNESCO-China Funds-in-Trust (CFIT) wenye lengo la kuziba pengo la ubora wa elimu wa kuwawezesha walimu kufundisha kwa kutumia Tehama ulizinduliwa Novemba 22,2012 kwa nchi tatu za kwanza na baadae kuongezwa nchi nyingine tano kufikia nane mwaka 2013.
Mpango huo ni wa dola za Marekani milioni 8 kutoka China mahususi kwa mataifa ya Afrika kuboresha elimu kupitia Unesco.
Prof. Elifas Bisanda
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yanayoendelea katika maabara za Chuo Kikuu Huria (out) jijini Dar es salaam. Walioketi kutoka kushoto ni Basiliana Caroli Mrimi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo pamoja na Kiongozi wa kitaifa wa timu ya mradi wa CFIT kit, Prof. Ralph Masenge.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku 10 katika Chuo Kikuu Huria, Mtaalamu wa program za elimu kutoka makao makuu ya Shirika la Unesco mjini Paris, Ufaransa, Gabriel El Khili alisema kwamba program hiyo imelenga kutatua chnagamoto zinazokabili elimu ili elimu iwe ileinayotakiwa kuwezesha maendeleo ya kasi katika sayansi.
Alisema ni lengo la Unesco kupitia ufadhili huo kuhakikisha kwamba kunapatikana walimu bora watakaowezesha matumizi ya Tehama katika kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu ili kutengeneza wataalamu wa baadae katika taifa hili.
Alisema kuna pengo kubwa kuhusiana na ubora wa elimu na kwamba baada ya kumaliza program ya elimu kwa wote mwaka jana nguvu sasa inastahili kuelekezwa katika ubora wa elimu ili kufikia malengo ya 2030.
Alisema changamoto kubwa ni kuleta karibu matumizi ya digitali kwa kuzingatia ukweli wa sasa kwamba matumizi yake ni madogo ukizingatia na haja kubwa inayoambatana na haja ya kuwa na elimu bora.
Alisema ni vyema kuiga mfano wa China kwamba kuna tatizo la kidunia la kielimu lakini linalohitaji suluhu ya eneo la husika kwa kuzingatia rasilimali zilizopo eneo hilo.
Gabriel El Khili - Unesco, Paris
Mtaalamu wa program za elimu kutoka makao makuu ya Shirika la Unesco mjini Paris, Ufaransa, Gabriel El Khili (kulia) akizungumzia madhumuni ya programu hiyo inayoratibiwa na UNESCO wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya wiki mbili kwa walimu yanayoendelea katika maabara ya Tehama Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Alisema mapinduzi ya kitamaduni ya China baada ya kujikomboa yalizingatia elimu na kwa kutumia rasilimali za nyumbani waliweza kusonga mbele na nia yao ya sasa ni kufikiri shida ya elimu na maendeleo kimataifa lakini kupata suluhu ya tatizo hilo kwa nchi husika kwa kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika kuboresha elimu.
Anasema mafunzo kwa Tehama maana yake kusambaza elimu bora kwa kutumia nyenzo za Tehama zilizopo kuanzia redio televisheni, CD na kadhalika.
Alisema ni matumzi ya Unesco kwamba mafunzo yanayotolewa yatasaidia kuboresha elimu ya walimu na wanafunzi wao kwa kutumia Tehama, matumizi yake yaliyotukuka ambayo yatasaidia kuimarisha na kutoa ubora wa elimu pamoja na kuwa na walimu wachache.
Naye Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akifungua mafunzo hayo aliwataka walimu hao kutambua umuhimu wao katika kusukuma mbele lengo la mafunzo hayo na wala si kujipatia cheti cha mahudhurio.
Prof. Ralph Masenge
Kiongozi wa kitaifa wa timu ya mradi wa CFIT kit, Prof. Ralph Masenge akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo katika hafla fupi ya ufunguzi.
Alisema ulimwengu wa sasa ni wa walimu kutoa mwongozo wa namna ya kujifunza kwa kumuelekeza mwanafunzi kwa kuwa ulimwengu wa digitali umerahisisha mambo mengi.
Alisema wasishangae wakigundua kwamba wanafunzi wao ni weledi zaidi kuliko wao ila wasaidie kuhakikisha kwamba Tehama inatoa nafasi ya wanafunzi wengi kujifunza na kupata elimu wanayohitaji katika kubadili maisha na uchumi katika jamii.
Alisema kwamba ni matumaini yake kwamba kwa mafunzo hayo elimu ya Tanzania itapaa hasa kutokana na ukweli kuwa China imesema wazi kuwa haitapenda Tanzania kushindwa katika mradi huu wa kuleta maboresho makubwa katika elimu ya Tanzania ili iweze kutumika kutengeneza maarifa.
Profesa Bisanda alisema kwamba kwa sasa Tanzania ina shida kubwa katika masomo ya sayansi (bayolijia,kemia na fizikia ) pamoja na hesabu na kwamba uwapo wa program hiyo kutasaidia kufikisha mafunzo kwa wanafunzi kwa namna bora na yenye uhakika zaidi hata kama walimu wapo wachache.
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
Pichani juu na chini walimu kutoka Vyuo vya Monduli, Tabora na Morogoro wakishiriki mafunzo ya matumizi ya Tehama kwa vitendo katika program ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya kuboresha elimu Tanzania kupitia ufadhili wa taifa la China.
Alisema ni vyema walimu wakajifunza namna ya kufanya na kutafuta majawabu ya matatizo kwa kutumia tehama na kuambukiza mwenendo huo kwa wenzao na kwa wanafunzi.
Alisema ni kweli kuwa Tanzania ipo gizani katika ICT kutokana na matumizi yake madogo na hivyo walimu wakielewa na kuwafunza wengine taifa hili litaondoka katika giza hilo na kupata mapinduzi makubwa ya fikira na elimu.
Aidha alisema kwa kutumia ICT wanaweza kupunguza gharama za uendeshaji na uzalishaji hasa katika masomo na mafunzo.
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
Alitolea mfano kwamba kama wakipata softwea ya mitihani ambayo ipo wanaweza kuokoa zaidi ya shilingi milioni 700 wanazotumia kwa ajili ya mitihani na michakato yake.
“Fikiria unaweka program ambayo mwanafunzi anafanya mitihani moja kwa moja na hii inawezekana, utafanya nini na fedha hizo ambazo unazitumia sasa kwa ajili ya uandazi wa mitihani kuifanya na kuisahihisha” aliuliza na kusema kwamba zingelisaidia vitu vingine.
Alisema kihistoria walikuwa wanakazi kubwa ya kuandaa mitihani na kusambaza lakini mwanzo wa kuwafanya wanafunzi wajieleze kama wanataka kufanya mitihani kwa kutumia Tehama sasa wanatengeneza mitihani kwa kadiri ya maombi na kupunguza gharama.
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
Picha ya pamoja ya wakufunzi na washiriki.
Faith Shayo - Unesco, Dar es Salaam
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (kushoto), Mtaalamu wa program za elimu kutoka makao makuu ya Shirika la Unesco mjini Paris, Ufaransa, Gabriel El Khili (katikati) pamoja na Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.

Jumanne, 22 Machi 2016

MAJALIWA ATEMBELEA SOKO LA FERI DAR ES SALAAM




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielkea kwenye soko la samaki la Feri  akitokea ofisini kwake  Magogoni  jijini Dar es salaam kukagua hali ya soko hilo Machi 22, 2016. Kushoto kwake  ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  eneo la kukaangia samaki kwenye soko la samaki Feri la jijini Dar es salaam Machi 22, 2016, Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Raymond Mushi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mama Lishe wakati alipotembelea  soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam Machi 22, 2016.






Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia  Mama Lishe wakati alipotembelea  soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam Machi 22, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DARAJA LA KIGAMBONI KUFUNGULIWA RASMI APRILI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni Eng. Karim Mattaka alipokagua daraja hilo leo jijini Dar es salaam.


 Mwonekano wa lango la kuingilia daraja la Kigamboni kwa upande wa Kigamboni, linavyoonekana pamoja na vyumba vya kukatia tiketi.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja miradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Eng. John Msemo wakati alipotembelea daraja la Kigamboni kuangalia ujenzi wa daraja la Kigamboni leo jijini Dar es salaam.
 Mwonekano wa lango la kuingilia daraja la Kigamboni  kwa upande wa Kigamboni, linavyoonekana pamoja na vyumba vya kukatia tiketi.
 Mwonekano wa vyumba vya ofisi zitakazotumiwa na wasimamizi wa Daraja la Kigamboni.
 Barabara za maingilio (inter change) ya Daraja la Kigamboni upande wa Kurasini.

WAZIRI NAPE KUREJESHA HADHI YA MUZIKI WA DANSI NCHINI

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wasanii wa Muziki wa Dansi alipokutana nao jana jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mungereza akizungumza wakati wa mkutano baina ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) na wasanii wa muziki wa Dansi nchini jana jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) Bw.Juma Ubao akizungumza wakati wa mkutano baina ya wasanii wa muziki wa Dansi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) jana jijini Dar es Salaam.
 Mdau wa Muziki wa Dansi nchini Asha Baraka akichangia mada wakati wa mkutano baina ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) na wasanii wa muziki wa Dansi jana jijini Dar es Salaam.


Mwanamuziki wa Dansi nchini,Muumini Mwijuma akichangia mada wakati wa mkutano baina ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) na wasanii wa muziki wa Dansi jana jijini Dar es Salaam.




Mdau wa Muziki wa Dansi nchini ambaye pia ni raia wa Italia Bibi.Maria akichangia mada wakati wa mkutano baina ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) na wasanii wa muziki wa Dansi jana jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea CD yenye nyimbo ya kumsifu Mwl. Nyerere kutoka kwa mwanamuziki nguli Mzee Makassy (mwenye kofia). Katikati ni Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Hassan Msumari.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea zawadi ya CD yenye nyimbo za Bendi ya Twanga Pepeta kutoka kwa mmiliki wa Bendi hiyo Bibi. Asha Baraka mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Waziri na wasanii wa muziki wa Dansi nchini jana jijini Dar es Salaam.

 Mwanamuziki mkongwe wa Muziki wa Dansi nchini Komandoo Hamza Kalala akichangia mada wakati wa mkutano baina ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) na wasanii wa muziki wa Dansi jana jijini Dar es Salaam.

MBUNGE VITI MAALUMU ASAIDIA AKINA MAMA WAJASILIAMALI.



  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve




Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve akiwana baadhi ya wananchama wa chama ch mapinduzi.
            

Na Sebastian Emmanuel jr. Mafinga.
 
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve ameendelea kukutana na makundi mbalimbali katika mkoa
huo, mwishoni mwa wiki hili amekutana na wajasiliamali wanawake katika makundi
mawili tofauti. Kundi la kwanza alilokutana nalo ni lile la umoja wa wanawake
wa ccm Iringa mjini, waliounda vicoba kwa ajili ya kukopeshana na kuendeleza
miradi kadhaa ya kijasiliamali.
Aidha wanawake hao wakati wakisoma risala kwa mbunge huyo wamesema kuwa wanakabiliana na changamoto kadhaa hasa
ukosefu wa mtaji utakao wafanya waendeleze vicoba hivyo ambavyo imekuwa
kimbilio la makundi mbalimbali mijini na vijijini.
Pia wanawake wao wamemwomba mbunge huyo kuhakikisha kuwa wanawake wa mkoa wa Iringa wanakuwa mfano wa kuigwa
katika kuanzisha, kukilinda na kukitetea chama chao hicho cha vicoba kwa kuwa
vinaonesha nia ya kuwasaidia kujikimu kimaisha, mpaka sasa wameanza kutafuta
wataalamu wa kufundisha namna ya kufuga kuku ili wapate elimu sahihi na kasha kuanza
kutekeleza mladi huo.
Kwa upande wake mbunge huyo kijana ametoa milioni moja taslimu kama mkopo usiokuwa na riba ili uweze kuwasaidia
kuendeleza mtaji wao pia akatumia fursa hiyo kuwaomba mkopo huo wauzungushe
katika miradi mbalimbali kama ya ufugaji kuku n.k. pia ameonesha nia ya
kuwasaidia wanawake hao na kuwaahidi kuwa wakiwa na uaminifu wa kulinda mtaji
wao hata kama ni mdogo atahakikisha kuwa vicoba hiyo inakuwa ya mfano wa kuigwa
mkoani Iringa. 
Mbunge huyo amewaomba wanawake wote wa mkoa wa Iringa wasikate tamaa badala yake wapende kujifunza na kutaka
kupata nafasi ambayo itawapeleka kwenye mwanga wa  mafanikio. Amesema kuwa hata yeye amekuwa
akithubutu kujituma kwa bidii ili aweze kufikia lengo la kuwasaidia wanawake
wote bila kujali itikadi, kabila wala dini zao.
Aidha kundi jingine la pili ni lilela wanawake wanaoishi na ulevu Mjini Iringa, wametumia fursa hiyo kuongea
na mbunge huyo na kumweleza changamoto wanazokumbana nazo, ikiwa ni pamoja na
kutokuwa na mtu wa kuwasaidia kwa mda mrefu kulingana na changamoto zinazo
wakabili na kuonesha imani kwa mbunge huyo kuwa sasa wanamatumaini mapya kuwa
wamepata mtu muafaka wa kuwasaidia.
Wanawake hao wanaoishi na ulemavu wameomba pia kupatiwa mtaji ili uweze kuwasaidia katika umoja wao wa kazi za
mikono ikiwa ni ususi wa shanga za kimasai, mikoba ya kimasai na mikoba ya
kisasa kwa kutumia shanga mbalimbali za asili, ambapo mbunge huyo licha ya
kuwapa kiasi cha pesa kwa ajili ya kuendeleza mtaji wao pia amewaomba waanzishe
mladi wa utengenezaji wa batiki utakao wanufaisha kwa kiwango kikubwa kwani
unaonesha kuwa na soko la uhakika.