Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumanne, 28 Agosti 2018

WANANCHI WA VIJIJI VYA IRAMBA KUNUFAIKA NA UMEME WA REA

Posted by Eata Malibiche on Auget   28,2018 IN NEWS.



MENEJA wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kanda ya Kati, Mhandisi Athanasio Nangali amesema watahakikisha vijiji vyote vya Wilaya ya Iramba ambavyo havijapata umeme wa REA mzunguko wa tatu kwa awamu ya kwanza, na awamu ya pili, vinapatiwa umeme huo.

Akizungumza jana katika Kata ya Ndurungu wilayani Iramba mkoani Singida, Eng Nangali alisema watahakikisha kuwa ifikapo mwaka 2021 umeme unaenea katika mkoa wote wa Singida kwa takribani vijiji 150 vilivyoko kwenye mpngo

Alisema kuwa Wilaya ya  Iramba ina vijiji 30 ambavyo vinatakiwa kuwekewa umeme wa REA na kwamba kuna baadhi ya vijiji ambavyo viliachwa kwenye awamu hiyo.
jb
"Kwa kuwa mbunge wenu amekuja kuomba vijiji vya Kata ya Ndurungu ikiwemo Kipuna , Mahola na Mwanduigembe viweze kupatiwa umeme katika awamu hii. Tutasimamia kuhakikisha kila kijiji kinapata umeme kwani ndio chachu ya maendeleo  na ndio fursa nyingi zitapatikana," alisema Eng Nangali.

Kwa upande wake, Mbunge wa Iramba, Dk Mwigulu Nchemba alisema amepeleka maombi hayo kwa sababu baadhi ya vijiji havijapata umeme kwa muda mrefu licha ya kuzungukwa na maeneo mengine yenye umeme.

Dk Nchemba alisema Kata ya Ndurungu imezaliwa kutoka Kata ya Kaselya ambayo ina umeme hivyo wanakijiji wake wanaona kama wametengwa.

"Wanakijiji hawa wanaona wametengwa ili wakose huduma hiyo muhimu au wametengwa ili wapate huduma. Niliona nipeleke maombi maalum ili Kata hii ipate umeme," alisema Dk Mwigulu.

Pia alisema Kijiji cha Sipuka tayari kina umeme na kwenye mpango huo unataka uende kijiji cha Mnere kuzunguka Kata hiyo.

Alisisitiza kuwa kijiografia wananhi wote wanahitaji huduma ya umeme kwani zipo shughuli nyingi za maendeleo zinazofanyika ikiwemo hospitali, shule na viwanda.

Naye, Mwanakijiji wa Mwandujembe Kata ya Ndurungu, Omary Hussein alisema ujio wa umeme utasaidia wajasiriamali, viwanda na shughuli nyingine za maendeleo.

Alisema suala la umeme lilikuwa ni ndoto yao ya muda mrefu kwani sehemu nyingi walizopakana nazo zimepata umeme lakini wenyewe walitelekezwa.

"Hatujapata mbunge mwenye kasi kama hii ya kutusaidia kupata umeme hivyo tunaamini kuwa maendeleo yafakuja kwa kasi," alisema Hussein.


Jumatano, 25 Julai 2018

WANAUME MKOANI IRINGA WATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMA VVU

Posted by Esta Malibiche on Julai 25,2018
Mkuu wa wilaya ya mufindi Jamhuri Wiliam akizindua rasmi kampeni ya 'FURAHA YANGU' pima,jitambue,ishi Mkoani Iringa.Uzinduzi huo ulifanyika jana katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa ikiwa na  lengo la kuhamasisha wannachi hususani wanaume kupima vvu.picha na Esta Malibiche.


WANAUME  mkoani Iringa wametakiwa kujitokeza kwa wingi  kupima ili kujua Afya zao na kuanza dawa mapema  ili  kupimguza maambukizi mapaya.

Iringa ina jumla ya watu wapatao 18,000 wanaoishi na maambukizi ya VVU na wengi wao ni wanaume ambao hadi sasa hawajui hali zao za maambukizi.
Akizungumza jana na wananchi wa mkoa  wa Iringa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘furaha yangu’pima,jitambue,ishi iliyofanyika katika viwanja vya mwembetogwa Manispa ya Iringa, mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Iringa,ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William alisema kuwa takwimu zilizofanyika mwaka 2017 zinaonesha Iringa inakadiriwa kuwa na watu 72,000 wanaoishi na maambukizi ya vvu na kati ya hao hadi kufikia Juni 30 ,2018 watu 54,000 walikuwa wamejiunga na huduma za tiba na matunzo wengi wao wakiwa ni wanawake.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa Christopher Magala akipima maambukizi ya vvu katika Uzinduzi wa kampeni ya" Furaha yangu" pima,jitambue,ishi iliyozinduliwa jana mkoani Iringa.Picha na Esta Malibiche
Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe ambae pia ni Diwani wa kata ya Isakalilo [CHADEMA] akipima maambukizi ya vvu katika Uzinduzi wa kampeni ya" Furaha yangu" pima,jitambue,ishi iliyozinduliwa jana mkoani Iringa.Picha na Esta Malibiche.



WAZIRI JAFO ATEMBELEA UJENZI WA MIRADI MBALIMBALI WILAYANI BAHI, DODOMA

Posted by Esta Malibiche on Julai 25,2018 IN NEWS
jaf (1)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akifanya uhakiki wa vipimo vya upana wa Daraja la Chipanga kama vinaendana
na.
jaf (2)
Daraja
la Chipanga lililo katika hatua za mwisho za umaliziaji wilayani Bahi.
jaf (3)
Viongozi
wakikagua maabara iliyoanza kutoa huduma baada ya kumaliza kwa ujenzi katika
kituo cha afya Bahi.
jaf (4)
Zoezi
la ukaguzi wa miradi likiendelea wilayani Bahi.
jaf (5)
Ujenzi
wa daraja la Chipanga lililopo wilayani Bahi Mkoani Dodoma limeleta faraja kwa
wananchi na viongozi wa wilaya hiyo huku wakimwagia sifa Wakala wa Barabara wa Mijini
na Vijijini (TARURA) kwa usimamizi mzuri.
Hali
hiyo imejidhihirisha leo katika ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipokuwa akikagua miradi.
Akizungumzia
kufurahishwa na ujenzi huo, Mbunge wa Jimbo la Bahi Omary Baduel amewapongeza TARURA
kwa ujenzi wa daraja hilo kubwa na barabara zake kwa ubora wa hali ya juu
ikilinganishwa na siku za nyuma kabla TARURA haijaanza.
ya maendeleo wilayani Bahi.
Daraja
la Chipanga ni daraja kubwa lenye urefu wa mita 45 na limegharimu Sh. bilioni
2.18 na litakuwa mkombozi kwa wananchi wa Chipanga ambao walikuwa wanateseka
kwa miaka yote.
Katika
ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa pia kutembelea ujenzi wa kituo cha Afya
Bahi kinacho karabatiwa na serikali kwa Sh.Milioni 500 ambapo hadi sasa kazi ya
ujenzi imekamilika na wananchi wameanza kupata huduma katika majengo hayo
yaliyojengwa kisasa.

SERIKALI YAAGIZA UANZISHWAJI WA MABARAZA YA WAZEE NCHINI.


  Posted by Esta Malibiche on Julai 25,2018 IN NEWS


Pix 1 (1)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akifungua jengo jipya la Wazee na wasiojiweza  Kolandoto lililopo mkoani Shinyanga.
Pix 2 (1)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi vifaa na mahitaji kwa ajili ya wazee na wasiojiweza mara baada ya kufungua jengo jipya la Makazi hayo ya  Kolandoto lililopo mkoani Shinyanga.
Pix 5
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na Mwenyekiti wa wazee waishio katika makazi ya Kolandoto Mzee Somolo Shija mara baada ya kufungua jengo jipya la Wazee na wasiojiweza  Kolandoto lililopo mkoani Shinyanga.
Pix 3
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wazee na wananchi wa Kolandoto wakati wa uzinduzi wa  jengo jipya la Wazee na wasiojiweza la Kolandoto Mkoani Shinyanga.
Pix 4
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo la wazee na wasiojiweza la Kolandoto lililopo Mkoani Shinyanga kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kabla ya uzinduzi wa jengo hilo .
NA WAMJW, SHNYANGA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezitaka Mamlaka za Mikoa na Wilaya kuanzisha Mabaraza ya Wazee katika mikoa na Halmashauri nchini.
Agizo hilo limetolewa mkoani Shinyanga na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizindua jengo la makazi ya kulea Wazee na wasiojiweza ya Kolandoto yaliyopo mkoani Shinyanga.
Akizungumza na wazee na wanachi wa eneo la Kolandoto Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wazee ni tunu kwa taifa na jamii imeaswa kuwatunza na kuewaenzi kwa utumishi na mambo makubwa waliyofanya katika taifa letu.
Ameongeza kuwa Serikali ipo katika mpango wa kuendelea kukarabati makazi mengine 16 yaliyopo sehemu nyingine nchini.
” Niseme tu Serikali inawajali Wazee kwa kiasi kikubwa na itahakikisha inawatunza wale Wazee wote wasio na ndugu wa kuwalea”.
Dkt Ndugulile amewaasa wazazi na jamii kupambana na mimba na ndoa za utotoni na kuwaomba Wazee nchini wawe washauri na walezi wazuri kwa wajukuu zao katika kuzuia mimba na ndoa za utotoni.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro amesema kuwa Serikali ya Wilaya itaendelea kuwalinda na kuwatunza Wazee kwani ni sehemu pekee ya kuchota busara ili kuwezesha Jamii kuishi katika maadili mema.
“Sisi kama Wilaya tutalisimamia suala la kuwalea Wazee hawa ambao ni tunu ya taifa” alisisitiza Mhe. Josephine.
Akito taarifa ya ujenzi wa jengo hilo Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa makazi hayo yamegharimu jumla ya Tsh . Millioni 138 mpaka kukamilika kwake.
Bibi. Sihaba ameongeza kuwa ujenzi huo umetokana na uchakavu wa majengo yaliyokuwepo hivyo kuwapa mazingira salama Wazee waishio katika makazi hayo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wazee wa Makazi hayo Mwenyekiti wa Makazi Mzee Somolo Shija ameishukuru Serikali ya Awamu ya tano kwa kuwawezesha kupata makazi mapya kwani walikuwa wakiishi katika majengo chakavu.
“Tunaishukuru Serikali yetu kwa kutujali wazee” alisisitiza Mzee Shija.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014 kuna jumla ya wazee 4,14,382 sawa na asilimia 5.6 ya watanzania wote ambapo ndugu na Serikali wanajukumu la kuwalea na kuwatunza katika kaya zao.

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MKOANI SONGWE-ILEJE

Posted by Esta Malibiche on JULY 25,2018 IN KITAIFA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele mara baada ya kuzindua
shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbuge wa Jimbo la Ileje Mhe. Janeth Mbene mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais)



  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya shamba la Misitu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mipango-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais)



 Kikundi cha Ngoma cha Sange kikitumbuiza ngoma ya Ling'oma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia  wakazi wa kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais)

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amezindua shamba la miti katika hifadhi ya Misitu Iyondo Mswima lililopo Katengele wilayani Ileje mkoani Songwe ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.

Shamba hilo lililo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni moja kati ya mashamba mapya yakiwemo Biharamulo (Chato Geita), Buhigwe (Kigoma) na Mpepo (Mbinga, Ruvuma).
Akisoma taarifa ya Shamba hilo kwa Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Mipango –Wakala wa Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo amesema kuwa mpaka shamba la miti la Iyondo Mswima limeweza kutoa ajira kwa wananchi 400 katika msimu wa kupanda miti, pia shamba limetoa ajira zingine 200 wakati huu wa maandalizi ya bustani ya miti, hekta 201 zimepandwa miti kama sehemu ya upanuzi wa mashamba ya miti ya Serikali ambapo bustani yenye jumla ya miche 430,000 kwa ajili ya upandaji miti wa mwaka 2018/2019.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele ambapo shamba la misitu la Serikali Iyondo Mswima limezinduliwa, Makamu wa Rais amewataka wananchi hao kutunza na kuyalinda mazingira kwa kupanda miti kwa wingi ambapo kila mwaka wananchi watapewa miche 50,000 na Wakala wa Huduma za Misitu wa Serikali.
Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Sange ambapo aliwaambia wananchi wa kijiji hicho kuwa Mungu amewapa rasilimali nzuri sana hivyo hawana budi kuyatunza.
Makamu wa Rais amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje kuhakikisha Maafisa Ugani wanashuka kwa wananchi na kutoa ushauri namna ya kufanya shughuli za kilimo vizuri.
Makamu wa Rais amesema Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1.5 katika bajeti mwaka huu iliyopita kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya ya Ileje.

Jumanne, 10 Julai 2018

BANK YA CRDB YAMKABIDHI MIFUKO 724 YA SARUJI MBUNGE WA JIMBO LA DODOMA MJINI ANTHONY MAVUNDE

Posted by Esta Malibiche on July 10,2018 IN NEWS

 Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo amepokea mifuko ya Saruji 724 yenye thamani ya Tsh 10,000,000 kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa,Nyumba za Walimu na matundu ya vyoo katika shule za Msingi na Sekondari katika Jimbo la Dodoma Mjini.

Akikabidhi mifuko hiyo ya Saruji,Mkurugenzi CRDB Tawi la Dodoma Bi Rehema Hamis amesema kwamba Benki ya CRDB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mh Rais Dr John Pombe Magufuli na uchapakazi wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde katika kuboresha miundombinu ya Elimu.

Akipokea mifuko hiyo ya saruji,Mbunge Mavunde ameishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo ambao utalenga kupunguza changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa 1035 katika Jimbo la Dodoma Mjini ambapo kwa hivi sasa anaendesha kampeni maalum ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi na kwa kuanzia mfuko wa Jimbo umetoa matofali 32,000 na mifuko ya Saruji 2,560 kwa kata mbalimbali.







MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM, OFISI NDOGO ZA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA JIINI DAR ESALAAM, LEO

Posted by Esta Malibiche on july 10,2018 IN SIASA

 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akilakiwa na wajumbe alipowasili ukumbini kuogoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jinini Dar es Salaam, leo.

 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akilakiwa na wajumbe alipowasili ukumbini kuogoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jinini Dar es Salaam, leo.

 Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jinini Dar es Salaam, leo.

Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akiogoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jinini Dar es Salaam, leo.