Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Alhamisi, 21 Desemba 2017

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAMISEMI SELEMANI JAFO AAGIZAA DED WA MOROGORO VIJIJINI ACHUNGUZWE HARAKA

Posted by Esta Malibiche on DEC 21,2017 IN NEWS
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Morogoro vijijini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya morogoro Vijijini Sudi Mussa Mpiri kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Pia ameshindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani kutoka kampuni ya Dimond ambapo matumizi ya fedha hiyo zaidi ya asilimia 90 hayafahamiki kilichofanyika.
Kadhalika, Mkurugenzi huyo anadaiwa kuwa na mahusiano mabovu kati yake na watumishi wa Halmashauri hiyo.
Jafo alitoa agizo hilo akiwa Kijijini Mvuha kwenye makao makuu ya Halmashauri ya morogoro vijijini.
Kutokana na hali hiyo,Jafo ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa mkurugenzi huyo kwa lengo la kuchukua hatua stahiki endapo itabainika kuna ufisadi na mapungufu ya kiuongozi kwa mkurugenzi huyo.
Katika hatua nyingine, Waziri Jafo hajarishishwa kabisa na miradi aliyo itembelea wilayani humo kutokana na miradi hiyo imeonyesha wazi kwamba Halmashauri hiyo imefanywa kama shamba la bibi.
Jafo amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa niaba ya wananchi wanyonge hivyo wanapaswa kulinda na kusimamia rasilimali za Halmashauri hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya morogoro vijijini katika ukaguzi wa miradi.



 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya morogoro vijijini akiwemo Mbunge wa Morogoro vijijini Omary Mgumba katika ukaguzi wa miradi.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya  Morogoro vijijin

.....................................................................

MAVUNDE ATEMBELEA UJENZI WA DARAJA LA CHIHANGA-GAWAYE NA ZAHANATI YA ZEPISA,HOMBOLO MAKULU-DODOMA MJINI

Posted by Esta Malibiche on DEC 21,2017 IN NEWS
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,Mh Anthony Peter Mavunde leo ametembelea ujenzi wa Daraja linalounganisha vijiji vya Chihanga na Gawaye kata ya Chihanga Jimbo la Dodoma Mjini na kupongeza kasi ya ujenzi inayofanywa na Mkandarasi katika kuhakikisha daraja hilo linakamilika mapema ili wananchi waondokane na adha kubwa ya kutokupitika eneo hilo kipindi cha masika.

Daraja hilo lenye thamani ya Tsh 49m linatarajiwa kukamilika mapema January 2018 na hivyo kuondoa kero ya muda mrefu ya kutopitika kwa eneo hilo.

Aidha Mh Mavunde pia ametembelea ujenzi wa Zahanati ya Zepisa akiongozana na Mkurugenzi wa Global Space East Africa Ltd Ndg Gaston M. Francis aliyeoongozana na Mhandisi Malcom kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Mbunge Mavunde katika kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo ambapo Mavunde ameahidi kuchangia matofali 1000 na saruji mifuko 100,Manispaa ya Dodoma 10m na Ndg Gaston M. Francis kwa niaba ya Kampuni ya Global Space East Africa Ltd ameahidi kuchangia mifuko 50 ya saruji na vifaa vya ndani vya Zahanati baada ya kukamilika.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Hombolo Ndg Jacob Lemanya kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa anazofanya za kuwasaidia katika ujenzi wa Zahanati kwa kutafuta wafadhili mbalimbali ili kufanikisha ujenzi huu wa zahanati na kuahidi kuunga mkono jitihada hizo kwa wao kujitolea katika shughuli mbalimbali za ukamilishwaji wa zahanati hiyo










MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI KUIFANYA DODOMA KUWA YA KIJANI KWA KUPANDA MITI

Posted by Esta Malibiche on DEC 21,2017 IN NEWS
21
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma.
14
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akitoa maelezo ya kampeni ya kupanda miti  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjni kupitia chama cha Mapinduzi CCM Anthony Mavunde akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni ya   kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani iliyofanyika  kwenye chanzo cha Maji bonde la Makutupora Dodoma.

24
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiandaa mti wake kabla ya kuupanda mara baada ya kuzinduzi  kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma.
25
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti  mara baada ya kuzinduzi  kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjni kupitia chama cha Mapinduzi CCM Anthony Mavunde akipanda mti mara baa ya uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani.







Picha na ofisi ya Makamu wa Rais
………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa kampeni ya kupanda na ustawishaji miti isiishie Dodoma mjini tu bali ienee katika Wilaya zote za mkoa wa huo na hatimaye nchi nzima.
Makamu wa Rais aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani.
Makamu wa Rais alisema upandaji miti si kwa ajili ya kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi  ambapo alitolea mfano mti mmoja uliokomaa unaweza kunyonya hadi kiasi cha kilo 150 za gesi ya hewa ya ukaa kwa mwaka,husaidia kupunguza joto, kusaidia kuboresha afya zetu za mwili na akili kama tafiti zinavyoonyesha .
“Ni dhahiri, kampeni hii ya kuifanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kwa vitendo.” Alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Wana Dodoma kuipokea kampeni hii kwa mikono miwili na kutoa kila aina ya ushirikiano ili kufikia lengo zuri lililokusudiwa.
Makamu wa Rais ambaye alihamia rasmi mjini Dodoma siku ya ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 alitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Ofisi yake kwa kuja na wazo zuri .
Makamu wa Rais alisisitiza kuwa hategemei kuona zoezi la upandaji miti lianze na kuisha leo, na badala yake liwe la kudumu, pia alizitaka manisapaa zitunge sheria ndogo zitakazoelekeza shule, chuo, taasisi na familia kuanzisha bustani ndogo  za miti zitakayomudu mazingira husika,Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa ni vyema kupunguza ukataji wa miti kiholela ambapo alizitaka sheria, kanuni na taratibu zizingatiwe kabla ya kukata miti na kusema tupandemiti kabla ya kukata mti.
Makamu wa Rais alimalizia kwa kutoa shukrani kwa kampuni ya TATU Mzuka kwa kujitoa na kuhakikisha kampeni hii inatekelezwa na kutoa wito kwa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania iige mfano na kuelekeza makampuni mengine ya bahati nasibu yaweze kutoa mchango wake katika shughuli za kijamii hususan kwenye suala la hifadhi ya mazingira.
Pia Makamu wa Rais alitoa shukrani kwa Jeshi la Kujenga Taifa Makotopora, DUWASA, Magereza na Tanzania Forest Services (TFS) kwa kujitoa na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hili.
Mwisho, Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wa mkoa wa Dodoma kuanzisha vikundi mbali mbali vya upandaji .

Jumatano, 20 Desemba 2017

SOMA YALIYOJILI KATIKA MAGAZETI YA LEO DECEMBER 21,2017

Posted by Esta Malibiche on DEC 21,2017 IN NEWS