Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumamosi, 28 Oktoba 2017

MKUU WA WILAYA YA MBULU AMEZITAKA KAYA MASIKINI KUTUMIA KWA MALENGO KUSUDIWA FEDHA ZA TASAF

Posted by Esta Malibiche on Oct 28,2017  IN NEWS

Mkuu Wa  wilaya ya  mbulu Chelestino s Mofuga leo ,28/10/2017 atembelea kaya maskini zilizopo katika mpango wa Tasaf na kupata maelezo ya wanufaika jinsi wanavyotumia fedha hizo. Baada ya kutembelea kaya hizo amefanya mkutano na wananchi kuhamasisha uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa, na kupiga vita pombe haramu ya moshi ambaye inasababisha matukio ya uhalifu mbalimbali.
Pia mkuu wa wilaya ameonya vikali wanaopata fadha za Tasaf na kunywa pombe, kuolea wake wa pili badala ya kuanzisha miradi na kusomesha wastoto.


Aidha baadhi ya wanufaika wamekiri na kusema kuwa fedha za Tasaf ni mkombozi katika maisha yao kwani wameweza kusomesha watoto, kujenga nyumba na kuanzisha miradi ufugaji wa Ngo'mbe, mbuzi ,nguruwe na hata kufuga kuku.




VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU MKOANI DODOMA WAMPONGEZA MAVUNDE

 Posted by Esta Malibiche on Oct 28,2017 IN NEWS
Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Anthoyn Mavunde akizungumza na waumini wa dini ya Kiislam mara baada ya dua maalum iliyosomwa leo hii katika Madrasa ya Darual Mustafa_Chang'ombe Dodoma Mjini.PICHA NA OFISI YA MBUNGE

Viongozi mbalimbali na waamini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Ndg Anthony Mavunde kwa utendaji kazi wake wa kuleta maendeleo katika Jimbo la Dodoma Mjini.

Pongezi hizo zimetolewa mapema leo hii wakati akisomewa Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Mjini Dodoma.
 Viongozi hao wamempongeza Mbunge Mavunde kwa kugawa vitabu vya Misahafu 50,Juzuu 400 na Kanzu 300 katika misikiti mbalimbali iliyopo  Dodoma Mjini. 

Wamempongeza pia kwa kusimamia mabadiliko makubwa katika sekta za AFYA,ELIMU,MIUNDOMBINU,MICHEZO na UWEZESHWAJI WANANCHI.

Akitoa maelezo ya awali,Mwalimu wa Madrasa Ustadhi Omar Salum Itara amemshukuru Mavunde kwa msaada mkubwa alioutoa katika Madrasa hiyo ikiwa pamoja na kuwawekea umeme ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza mpaka usiku.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Anthony Mavunde,akizungumza katika Dua hiyo, aliwashukuru Viongozi na waamini wa dini ya kiislamu kwa namna wanavyomuunga mkono katika shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo na kuwaomba waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu atimize majukumu yake vyema.

Mavunde ametoa Msaada kwa Spika moja moja kwa Misikiti 16  zenye thamani ya Tsh 4,000,000 Pia ameahidi kukabidhi Laptop 2 zenye thamani ya Tsh 1,000,000 na milango miwili yenye thamani ya Tsh 500,000 kwa ajili ya madrasa ya Darul Mustafa.



Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Anthoyn Mavunde akizungumza na wau!ini wa dini ya Kiislam mara baada ya dua maalum iliyosomwa leo hii katika Madrasa ya Darual Mustafa_Chang'ombe Dodoma Mjini.PICHA NA OFISI YA MBUNGE
Dua maalum ikiendelea kusomwa katika Maikiti wa Chang'ombe leo Mjini Dodoma.



Dua ikiendelea katika msikiti wa Chang'ombe





Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi CCM Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Dini ya Kiislam mara baada ya Dua maalum iliyosaliwa kwa lengo la kumuombea.PICHA NA OFISI YA MBUNGE.

Ijumaa, 27 Oktoba 2017

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MARY MWANJELWA AWASILI MKOANI ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO WA TFA KESHO

Posted by Esta Malibiche on Oct 27,2017 IN NEWS
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwingine ni Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro 

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza kwa makini maelezo ya hali ya Upatikanaji wa Chakula kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akijadili jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro wakati akiondoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwingine ni Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Rasilimali watu (Utawala) wa Mkoa wa Arusha.

Na Mathias Canal, Arusha

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 27, 2017 aewasili Mkoani Arusha Kwa Ziara ya kikazi ambapo kesho Octoba 28, 2017 atafungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA).

Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha utahudhuriwa na viongozi mbalimbali huku ukitaraji kuhudhuriwa na Wanachama wa Tanganyika Farmers’ Association (TFA).

Pamoja na mambo mengine mkutano huo utabainisha vyema kazi na Huduma zinazotolewa na TFA ambazo ni kuuza Zana bora za kilimo, Pembejeo za kilimo kama Mbolea, Mbegu bora, Viuwatilifu mbalimbali pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa Wakulima, kama juhudi ya kumpunguzia mkulima karaha ya upataji wa huduma hizo,

TFA ni mojawapo ya Taasisi kongwe na muhimu kwenye maendeleo ya Sekta ya Kilimo nchini Tanzania na imekuwa ikihudumia Sekta hiyo kwa miaka zaidi ya 80 sasa, tangu ilipoanzishwa mnamo mwaka 1935.

Aidha, Kampuni ya TFA imekuwa ikifanya kazi na Serikali kwa njia ya kutoa huduma kubwa kwa Wakulima wote nchini pale ambapo TFA ina matawi ambayo husambaza na kuwafikishia Wakulima, pembejeo za kilimo zenye ubora wa hali ya juu, kwa wakati na kwa bei nafuu.

MWISHO.

Waziri Mwakyembe na Naibu Waziri Shonza washiriki Jukwaa la Sanaa

Posted by Esta Malibiche on Oct 27,2017 IN MICHEZO
Pix 1
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wadau wa tasnia ya muziki (hawapo pichani) wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 2
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akifafanua jambo wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 3
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi. Shani Kitogo akijibu hoja wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 4
Baadhi ya wasanii wakifuatilia mada zilizokua zikiendelea wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 5
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akicheza ngoma na wasanii waliokua wakitumbuiza wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 6
Makamu wa Rais Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bibi. Francisca Shirima akichangia mada wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 7
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na viongozi wa mashirikisho mbalimbali ya sanaa baada ya kumalizika kwa jukwaa la sanaa leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto waliokaa ni Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

Bodi Ya Filamu Fanyeni uUtafiti Kuona Takwimu Za Mapato Ya Sekta Ya Filamu – Mhe. Shonza

Posted by Esta Malibiche on Oct 27,2017 IN NWS

Pix 2
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na watendaji wa bodi ya filamu (hawapo pichani) wakati wa ziara yake kutembelea ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam


Pix 1
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kulia) akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) kutembelea ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akiangalia vitambulisho kwa ajili ya wasambazaji wa filamu wa Barazani alipofanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu na kutembelea wadau wa filamu Barazani jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Pix 4
Mkurugenzi wa Barazani Bw. John Kallaghe (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) namna mwananchi anavyoweza kununua kopi ya filamu kupitia simu ya mkononi jana wakati wa ziara yake katika ofisi za Bodi ya Filamu na baadaye kutembelea wadau wa filamu wa Barazani Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Pix 5
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watatu kulia) katika picha ya pamoja na viongozi wa shirikisho la filamu na wadau wa filamu kutoka Barazani baada ya kufanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu na baadaye kutembelea wadau wa Barazani Jana Jijini Dar es Salaam. Wanne kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Pix 6
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiweka sawa kipaza sauti alipotembelea Studio za Wanene Entertainment baada ya kufanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam
Pix 7
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watatu kulia) akiangalia namna kazi za sanaa zinavyoandaliwa alipotembelea Studio za Wanene Entertainment baada ya kufanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Pix 8
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Studio za Wanene Entertainment Bw. Dash Pandit (katikati) alipotembelea Studio hizo baada ya kufanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
…………………
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Tarehe: 27/10/2017
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ameitaka Bodi ya Filamu Tanzania kufanya utafiti na kukusanya takwimu sahihi za mapato yatokanayo na sekta ya filamu nchini ili kuweza kubaini sekta hiyo inavochangia katika pato la taifa.
Hayo ameyasema jana Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania na kuzungumza na watendaji wa bodi hiyo huku akiwataka kuweka mifumo ambayo itasaidia wasanii kuinua, kuboresha na kuendeleza tasnia ya filamu nchini.
Aidha Mhe. Shonza ameitaka bodi ya filamu kuhakikisha kuwa inasimamia maadili katika filamu pamoja na ubora wa filamu ili filamu zinazotengenezwa inchini ziwe na kiwango kitakachowavutia wadau wa filamu ndani na nje ya nchi kupenda filamu zetu.
Mhe. Shonza amesema kuwa katika kukuza vipaji Bodi ya filamu ifanye jitihada za kuwafikia na kutoa elimu kwa wanatasnia ya filamu waliopo mikoani kwani huko nako kuna wasanii wenye uwezo wa hali ya juu lakini vipaji vyao havionekani kutokana na kutofikiwa  kwa wakati.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amemhakikishia Mhe. Naibu Waziri kuwa Bodi ya Filamu itaendelea kukaza kamba na kuhakikisha kuwa haioni haya katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu ya sheria na kanuni zilizopo.
Bibi. Fissoo amesema kuwa kati ya mwaka 2011 hadi sasa bodi ya filamu imesambaza jumla ya nakala elfu thelathini za sheria na kanuni katika Mikoa na Wilaya zote nchini ili shughuli za filamu zinazofanywa mikoani ziweze kuendana na sheria na kanuni zilizopo katika sekta ya filamu.
Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifwamba amemshukuru Naibu Waziri Shonza kwa kuonyesha hari ya kuipigania sekta ya filamu mara tu baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri kwani kwa kufanya hivyo kunawapa moyo wanatasnia ya filamu kuelekea katika mapinduzi ya filamu nchini.

Maaskofu Katoliki wataka hukumu ya kifo itazamwe upya

Posted by Esta Malibiche On Oct27,2017 IN NEWS


MAASKOFU wa Kanisa Katoliki nchini wameiasa serikali kubadili sheria inayoruhusu adhabu ya kifo kwa wahalifu badala yake watoe hukumu ya kifungo cha maisha.
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya ameeleza hayo kwa niaba ya Maaskofu Katoliki Tanzania hivi karibuni huko jimboni TUNDURU-Masasi kwenye ibada ya mazishi ya Askofu wa Jimbo hilo marehemu Castory Msemwa.
“Leo tunapomzika Askofu Msemwa tunakumbuka kuwa mwanadamu anazaliwa na anakufa kupitia vifo mbalimbali ukiwemo uzee na magonjwa. Huo ni mpango wa Mungu kwamba mwanadamu afe ili afike kwenye makao aliyomuandalia.
Lakini kuna vifo ambavyo ni kinyume na mpango wa Mungu ikiwemo sheria inayoruhusu mahakimu kutoa hukumu ya kifo. Aliye na mamlaka ya kuchukua uhai wa mwanadamu ni Mungu peke yake kwani uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Sababu ya vifo vinavyotokea duniani ni sisi wanadamu wenyewe. Maandiko matakatifu yanatuambia Mungu peke yake ndiye ana uwezo na mamlaka ya kuchukua uhai. Uhai ni kitu kitakatifu lakini baadhi yetu tunapuuza.
Tunafahamu kwamba sheria za nchi nyingi duniani zinaruhusu mahakimu kutoa adhabu ya kifo ikiwemo Tanzania. Tunaiomba serikali yetu ione namna ya kubadili sheria hiyo na badala ya kifo, wahalifu wapewe adhabu ya kifungo cha maisha. Kama taifa tusikubali kuridhia mikataba ambayo haiheshimu uhai,” amesisitiza Askofu Mkuu Kinyaiya.
 Aidha maaskofu pia wameisisitiza jamii kuacha kutoa mimba kwani ni namna nyingine ya kutoa uhai wa mwanadamu suala ambalo wamesema ni kosa na ni dhambi kwa anayetoa na yeyote anayeshiriki. Hivyo jamii nzima ina wajibu wa kuheshimu na kutunza uhai ambao ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Wamewaonya vijana ambao ni nguvu ya taifa la Tanzania kuacha kuhatarisha maisha yao kwa kukumbatia utamaduni wa kifo.
“Vijana wanakufa kabla ya wakati wao kwa kudhoofisha miili yao kwa kutumia sumu mbalimbali kama vile mahusiano ya hovyo hovyo, dawa za kulevya nk. Wakidhani ndiyo namna ya kupata starehe kumbe wanajiangamiza.
Tatizo la vijana kujiua wenyewe nalo linaongezeka Tanzania. Kufuatana na ripoti ya Shirika la Afya duniani Tanzania ni kati ya nchi 10 duniani, zinazoongoza kwa watu hasa vijana kujiua.
Wapendwa vijana sisi wazee wenu tunawaasa muachane na huo utamaduni wa kifo, ishini maadili, maadili mliyofundishwa na Askofu Castory MSEMWA, mnayofundishwa na viongozi wenu wa dini mkijua kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu,” amesema.
Katika mazishi hayo Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya amesema kuwa, Maaskofu Katoliki Tanzania pia wametaka jamii itafakari pia kifo cha mazingira katika dunia wanayoishi.
Katika barua yake ya pili inayojulikana kama ' Laudato Si' yaani ‘sifa  iwe kwako’ Baba Mtakatifu Fransisko pamoja na mambo mengine anazungumzia jinsi  wanadamu wanavyoiua dunia kwa vitendo mbalimbali. Wanatumia dunia kwa uroho bila mpango kiasi kwamba wanaiua dunia ambayo ni mama yao.
“Matokeo ya madhara yanaturudia kwa njia ya ukame, ongezeko la hewa ya ukaa ambalo ni mbaya kwa afya zetu nk. Tutakimbilia wapi tukiiharibu dunia?
Tunamuasa kila mmoja wenu asiiumize dunia kwa vitendo visivyofaa, kama vile kukata miti hovyohovyo, kuchoma uoto asilia, kuua wanyama nk.” amesisitiza Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma.
Ameiasa jamii kuacha kulilia kifo kwani jinsi wanavyomuona Marehemu Askofu Castory Msemwa ndivyo kila mmoja atakuwa hivyo kwani kuzaliwa ni bahati na matokeo yake ni kifo ili mwanadamu aende kuishi na Mungu kwenye makao aliyomuandalia.
“Kuna watu wengi hawajapata bahati ya kuzaliwa duniani kwa sababu hawakutungwa mimba kabisa na hawakuja duniani kabisa na kwakuwa hawakuja duniani kabisa hawatakufa kwa sababu hawapo.
Sisi tuliobahatika kuzaliwa duniani hatma yetu ni kufa ili turudi kwa Baba, hivyo tusilalamikie kifo kwani ni sehemu ya hiyo bahati ya kuishi hapa duniani.
Tumeambiwa kuwa  Askofu MSEMWA amefariki kwa ugonjwa ambapo Mwenyezi Mungu ameamua kumchukua. Sisi kama wanadamu jukumu letu ni kupokea mapenzi ya Mungu ijapokuwa ni magumu kama wanadamu. Tuendelee kumuombea.
Ni wakati wetu wa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya Askofu Msemwa hapa duniani kwani aliyoyafanya hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kufanya kwani duniani hakuna watu wawili wanaweza kufanana na kufanya jambo lilelile. Kila mtu ana namna yake ya kutenda, naye alikuwa maalumu.
Tunamshukuru Askofu Msemwa kwa kutumia vipaji vyake kulitumikia Kanisa na jamii kwa ujumla bila kulalamika. Tunaamini kuwa kwakuwa alijitahidi kuishi wito wake kama Padri na Askofu Mwenyezi Mungu atampokea kwake mbinguni.
Suala la msingi ni kuishi ukristo wetu, tuishi maisha ya Sakramenti ili tujitakatifuze, tuwe watu wa toba tujiandae ili siku moja turudi kwa baba yetu Mbinguni,” ameeleza.
Amesema kuwa Maaskofu wanashukuru wote waliojitolea kumuuguza na kujaribu kuokoa maisha ya Askofu Msemwa kuanzia madaktari katika hospitali ya Taifa Muhimbili, India nk.
Pia anashukuru Ubalozi wa Tanzania nchini Oman pamoja na serikali nzima ya Tanzania kwa ushirikiano wa kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Oman hadi Tunduru kwenye maziko.
Amesema Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki wanaungana na wana Tunduru kufarijiana na kutiana moyo katika kipindi hicho kigumu.
Amewataka mapadri wa Jimbo Katoliki TUNDURU-Masasi kuwa na ushirikiano wakati huo ambapo wanasubiria wapewe msimamizi wa muda.
“Ni wazi kiti cha Askofu hapa Tunduru Masasi kipo wazi, sasa ni wajibu wetu kusali na kuomba ili Roho wa Mungu atuchagulie mchungaji mwingine wa Tunduru Masasi.
Tunawaomba mtunge sala maalumu mtakayoisali kila jumapili baada ya Misa kwa lengo hilo.
Na wakati tukisubiri Askofu mwingine, sisi Maaskofu tunawasihi sana mkae kwa amani, upendo na mshikamano,” amesisitiza Askofu Mkuu Kinyaiya.

Watoa huduma za Mahusiano ya Dini mbalimbali Mtwara watiwa hamasa

Posted by Esta Makibichebon Oct 27,2017 IN NEWS
Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara, Mhashamu Titus Mdoe wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya Haki za Binadamu 


Na Dalphina Rubyema, Mtwara
WATU wanaotoa huduma za kijamii kupitia mwamvuli wa Mahusiano ya Dini mbalimbali nchini, wametakiwa kujiona wenye thamani ya pekee kwa kile kilichoelezwa kuwa huduma yao hiyo ina mchango mkubwa katika kumkomboa mwanadamu kiroho na kimwili.
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara, Mhashamu Titus Mdoe wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya Haki za Binadamu yaliyowashirikisha viongozi wa dini na wasaidizi Kisheria mkoani humo iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Masista Mtwara.
Alisema kila anayefanya kazi chini ya mwamvuli wa dini mbalimbali hana budi kutambua kuwa anashiriki utume kwa njia ya pekee ili kuwezesha waja wa Mwenyezi Mungu kufurahia mema aliyowajalia muumbaji wao.
“Hata kule Adeni baada ya dhambi ya kula tunda ndio ulipoingia uhasama na hapo tunaona namna Adam alivyomtupia lawama ya dhambi mama yaani Eva na vile vile huyu mwanamama anamtupia lawama nyoka, hivyo huu unakuwa mwanzo wa  mfarakano hata kwa ndugu mfano mzuri ikiwa ni kwa Kaini na Aberi. Hata hivyo Mungu wetu anatudhihirishia kuwa hakutuumba kwa ajili ya mfarakano na ndio maana alimtuma mwanawe Yesu Kristo atukomboe,” amesema.
Askofu Mdoe amefafanua kuwa uwepo wa Kamati za Mahusiano ya Dini mbalimbali katika ngazi mbalimbali nchini zikiwemo ya Kitaifa, Kimkoa, Kiwilaya na hata ngazi ya Kata ni udhihirisho tosha wa kuviishi kwa matendo amani na upatanisho.
Ameongeza kuwa kupitia mahusiano haya ya dini mbalimbali wanajamii wameweza kuungana pamoja kufanya shughuli zao za kujiinua kiuchumi, kufuatilia rasilimali za umma na kuwa na ubavu wa kuhoji pale wanapoona miradi iliyotekelezwa haiendani na thamani ya fedha iliyotolewa pamoja na kupata fursa ya kupata elimu juu ya haki za binadamu.
“Tunayo sababu ya kufurahia kazi nzuri inayofanywa na wasaidizi wa kisheria katika maeneo mbalimbali ikiwemo hapa Mtwara kwani wamewezesha wanajamii kuelewa juu ya haki za binadamu zikiwemo zile za wanawake, watoto na makundi mengine ya kijamii,” amesisitiza.
Ameongeza “ Jamani hakika Tanzania tunapendwa na Mwenyezi Mungu kwani watu wote bila kujali tofauti zao za kidini wanaweza kukaa pamoja na kuzungumza mambo yanayohusu ustawi wao…Tazama yaliyotokea kwa nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Somalia, Kongo na kwingineko…tujivunie upendeleo huu ambao zaidi unapambwa pia na upatikanaji wa fuvu la mwanadamu wa kwanza lililopatikana kwenye ardhi yetu ya Tanzania eneo la Olduvai Gorge,”.
Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mradi wa Uendelezaji wa Utu wa Mwanadamu inayofanya kazi chini ya Idara ya Haki, Amani na Uadilifu katika Uumbaji ya Kurugenzi ya Human Dignity ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) yalifadhiliwa na Shirika la Misaada la Makanisa ya Norway (NCA) huku wawezeshaji wakuu wakiwa ni Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) cha jijini Dar es Salaam.
Chini ya Mradi huo, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kupitia Kamati ya Mahusiano na Dini mbalimbali mkoani Mtwara inatekeleza shughuli za kuwainua watu kiuchumi kupitia Benki za Kijamii Vijijini (IR-VICOBA), Ufuatiliaji wa fedha za umma zinazotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimali za Maendeleo (PETS) pamojana  Msaada wa Kisheria ambapo kimeanzishwa kituo cha Wasaidizi wa Kisheria katika eneo la Ziwani mkoani humo.
Mbali na Mtwara wilaya nyingine ambazo TEC inatekeleza miradi kama hiyo kwa ufadhili wa NCA ni Mbozi, Ludewa, Njombe, Temeke, Kasulu, Karatu na Babati.