Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Alhamisi, 1 Februari 2018

UVCCM MKOA WA IRINGA YAADHIMISHA MIAKA 41 YA KUZALIWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KWA KUCHANGIA DAMU KATIKA HOSPITALI YA MUFINDI, YAVUNA WANACHAMA WAPYA 120

Posted by Esta Malibiche on Februari 1,2018 IN SIASA
Na Esta Malibiche
Mufindi
JUMUIYA  ya Umoja wa vijana ccm Mkoa wa Iringa imeadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa kufanya usafi katika Hospital ya wilaya ya Mufindi, kuwaona na kuwafariji wagonjwa kwa kutoa vifaa mbalimbali Pamoja na kuchangia damu,ambapo zilipatikana unit 15.

Akizungumza  na mtandao huu wa Habari,[KALI YA HABARI BLOG]Mwenyekiti wa  Jumuiya ya  Umoja wa Vijana  CCM Mkoa wa Iringa, Kenani Kihongosi alisema  kuwa Lengo la kuadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi  kwa kuchangia damu ni kupunguza vifo vinavyokana na ukosefu wa Damu katika Hospital mara Mgonjwa anapohitajika kuongezewa Damu.
Kihongosi alisema kuwa hitaji la Damu salama katika Hospital ni kubwa,kutokana  kuongezeka kwa wananchi wanaohitaji kuongezewa damu kuwa kubwa.

Alisema kutokana na mwammo mdogo wa wananchi wanaojitolea kuchangia damu,hivyo Hospital nyingi zimekuwa zikikabiliwa na uhaba wa damu salama,hivyo aliwataka watanzania kujitokeza kuchangia damu ili kupunguza wimbi kubwa la vifo  vinavyotokana na ukosefu wa damu.

 ‘Hospital zetu zina kabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu salama kutokana na ongezeko la watanzania hasa watoto akina mama wanaopoteza damu wakati wakujifungua,na majeruhi wanaotokana na ajali wapotaka kuongezewa damu lakini inashindikana kutokana na uhaba wa damu hivyo hupoteza maisha.

Tumeshuhudia  matukio mengi ya ndugu zetu wakipoteza maisha yao kwa kukosa damau, na wengine wakifikishwa Hospitalini wanakosa hata chupa moja ya damu na hatimae kupoteza maisha,hivyo jukumu la kuchangia damu ni la kila mtanzania ili kupunguza wimbi hili la ukosefu wa damu katika Hospital zetu na hatimae kupunguza au kumaliza kabisa  vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu,kwa kuchangia damu tutakuwa tumewaokoa watanzania wenzetu’’Alisema Kihongosi na kuongeza kuwa

‘Sisi kama vijana tumaeamua tuadhimishe miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi kwa kuchangia damu ili tuweze kuokoa uhai wa watanzani’’Alisema Kihongosi.
Akizungumza katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi,Kenanai Kihongosi  aliitaka Halmashauri kuhakikisha asilimia 5 ya vijana inyotokana na makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri inawafikia  walengwa kwa wakati na si vinginevyo.

 ‘’Ninakuomba Mkurugenzi  uwasimamie maafisa maendeleo  wa wilaya wa hakikishe  wanatoa Elimu kwa Vijana  juu ya uundaji wa vikundi ili waweze kunufaika na mikopo hiyo.
Pia  aliwataka watumishi wa  kufanya kazi kwa weredi na bidii ili kuendana na kasi ya Seriakali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dakta John Magufuli

‘’Kwa mtumishi ambae anaona hwezi kuendana na kasi ya Serikali hii ya awamu ya tano ni bora akatupisha ili waachie wengine amabao watakuwa tayari kuendana na kasi hii’’Alisema Kihongosi.
Aidha Uvccm Mkoa wa Iringa kwa Pamoja wamempongeza Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Magufuli kwa  kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao,huku akitekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM,huku wakiwaomba watanzania waendelee kumuombea kila iitwapo leo.


Wakati huo huo wanachama wapatao  120 wapya waliojiunga na chama cha Mapinduzi  katika maadhimisho hayo walikabdhiwa kadi na kuapishwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umovja wa Vijana CCM Mkoa wa Iringa Kenanai Khongosi akichangia Damu katika Hospital ya Wila ya Mufindi jana wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm yaliyofanyika,ambapo Uvccm Mkoa wa Iringa Iliadhimisha kimkoa wialayani Mufindi. jana.

Katibu wa Jumuiya ya Umovja wa Vijana CCM Mkoa wa Iringa James Mgego akichangia Damu katika Hospital ya Wila ya Mufindi jana wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm yaliyofanyika,ambapo Uvccm Mkoa wa Iringa Iliadhimisha kimkoa wialayani Mufindi. jana.

Katibu wa Jumuiya ya Umovja wa Vijana CCM Mwialaya ya Mufindi  akichangia Damu katika Hospital ya Wila ya Mufindi jana wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm yaliyofanyika,ambapo Uvccm Mkoa wa Iringa Iliadhimisha kimkoa wialayani Mufindi. jana.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umovja wa Vijana CCM Mkoa wa Iringa Kenanai Khongosi akifyeka katika eneo la Hospital ya wilaya ya Mufindi  wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm yaliyofanyika,ambapo Uvccm Mkoa wa Iringa Iliadhimisha kimkoa wialayani Mufindi. jana.
 Katibu waa Jumuiya ya Umovja wa Vijana CCM Mkoa wa Iringa James Mgego akifyeka katika eneo la Hospital ya wilaya ya Mufindi  wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm yaliyofanyika,ambapo Uvccm Mkoa wa Iringa Iliadhimisha kimkoa wialayani Mufindi. jana.
Mjumbea wa Baraza Kuu Uvccm Taifa anaewakilisha Mkoa wa Iringa, Zawadi akifanya usafi kwa kufyeka katika eneo la Hospital ya wilaya ya Mufindi  wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm yaliyofanyika,ambapo Uvccm Mkoa wa Iringa Iliadhimisha kimkoa wialayani Mufindi. jana.






 








MICHUANO TULIA CUP YAANZA KUTIMUA VUMBI KATA YA KIBAMBA DAR ES SALAAM

Posted by Esta Malibiche on  Februari 1,2018 IN  MICHEZO


MSHAMBULIAJI wa timu ya Kibamba Worious Emmanyel Athanas (kulia) akijitahidi kumtoka beki wa timu ya Mpakani FC, Haruna Ramadhani, timu hizo zilipopambana katika mechi ya fungua dimba ya Tulia Cup, katika uwanja wa Kibwegele, Kibamba Dar es Salaam, juzi.
MSHAMBULIAJI wa timu ya Kibamba Worious (kulia) akijitahidi kumtoka beki wa timu ya Mpakani FC, timu hizo zilipopambana katika mechi ya fungua dimba ya Tulia Cup, katika uwanja wa Kibwegele, Kibamba Dar es Salaam, juzi.
Katibu wa Kamati ya Uratibu wa Michuano ya Tulia Cup Moreen Ngasala akimkaribuisha Diwani wa Kata ya Kibamba (CHADEMA) Ernest Mgawe (kulia) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mpiga wa Kibwegele, katika ufunguzi wa michuano hiyo
Msanii wa kujitegemea akichangamsha Uwanja kabla ya michuano hiyo kuanza
Kibamba Warious na Mpakani FC wakiwa tayari kwa mtanange
MC akitangaza hatua mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika uzinduzi wa michuano hiyo
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Elizabeth Majige aakisalimiana Katibi wa Siasa na Uenezi Kata ya Kibamba Clement Mgabo walipokutana kwenye uzinduzi wa michuano hiyo
Wadau wa friends Of Tulia wakiwa kwenye michuano hiyo
Mgeni rasmi akienda kukagua timu ili mpambano uanze
Mgeni Rasmi akisalimiana na mwamuzi wa mechi hiyo
Mgeni rasmi akisalimia wachezaji wa timu ya Kibamba Warious
Mgeni rasmi akiwa na baadhi ya viongzi baada ya kukagua timu
Timu zikiwa tayari kwa mpambano
Mmoja wa waraibu wa michuano hiyo Moreen akisoma risala
Mwenyekiti wa Friends of Tulia akizungumza kabla ya mpambano kuanza
Wadau wa Friends of Tulia wakiwa kwenye michuano hiyo
Diwani wa Kata ya Kibamba (CHADEMA),  Ernest Mgawe akizungumza kabla ya kipute kuanza. "Michezo siyo siasa, inasaidia sana kuweka jamii pamoja hasa vijana. Napongeza sana uamuzi wa kuanzisha michuano hii", alisema.
Mgeni rasmi akizungumza kufungua michuano hiyo ambayo leo kuu ni kuwaweka vijana pamoja na pia kuchangisha vifaa na fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Hondogo katika Kata hiyo ya Kibamba. Mgeni huyo rasmi aliahidi kuchangia mifuko mia moja ya saruji
Wadau wa Friends Of Tulia
Baadhi ya wadau wakiwa na wachezaji
Mdau wa Friends of Tulia akiwa na baadhi ya wachezaji
Mgeni rasmi akijiandaa kupiga mpira kuanshiria mechi kuanza
Mgeni rasmi akiwa ameshapiga mpira
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na timu zote
mpambano ukaanza
"vipi umenusurika?' refa akimuuliza mchezaji huku akimpapasa baada ya mchezaji wa timu ya Kibamba Warious baada ya  kuchezewa vibaya na mchezaji wa Mpakani FC
Kipa wa Mpakani FC akiuangalia mpira wakati ukiingia kimiani kufuatia penati iliyopigwa na mchezaji wa Kibamba Warious kutokana na mchezaji wa timu hiyo kufanyiwa rafu katika eneo la hatari
Mpambano ukiwa umeiva
Mdau wa Friends of Tulia akiwa na mmoja wa wasanii waliofika kuhangamsha uzinduzi wa Tulia Cup
Mwandishi wa Uhuru FM akiwa na mmoja wa wasanii waliofika kutia chachandu michuano hiyo
"Inaonekana naweza kuwa migapicha mzuri", mdau wa Friends Of Tulia akijaribu kupigapicha baadhi ya matukio kwenye michuano hiyo
Wadau wakitazama picha zao katika Blog ya taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM Blog). PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO