Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumanne, 4 Aprili 2017

Posted by Esta Malibiche on APRIL 4,2017 INBIASHARA

bbb
Kwa sasa, juhudi za Rais Dkt. Magufuli kufufua huduma bora na za uhakika katika Mashirika na Makampuni ya Umma zinazidi kuleta *Matokeo chanyA+*
Kampuni Simu ya TANZANIA -TTCL ndiyo kampuni pekee inaongoza kwa sasa kwa kutoa huduma za intanet bora na za uhakika.
Rais wangu… *mzalendo na mchapakazi..* Nchi yangu…

UCHAGUZI TAFCA KINONDONI KUFANYIKA MEI 7

Posted by Esta Malibiche on APRIL 4,2017 IN MICHEZO

football_0
Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu (TAFCA) Mkoa wa Kinondoni unatarajiwa kufanyika Mei 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Tarehe ya uchaguzi huo imetangazwa na Kamati ya Utendaji ya TAFCA Kinondoni inayomaliza muda wake iliyokutana Jumapili, Aprili 2 mwaka huu chini ya Mwenyekiti Eliutery Mholery (0715 621 667) na Katibu Mkuu wake Mbwana Makata (0655 520 129).
Fomu kwa ajili ya wagombea zimeanza kutolewa Jumatatu, Aprili 3 mwaka huu kwenye ofisi za Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA). Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea ni Ijumaa, Aprili 7 mwaka huu.
Ada ya fomu kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TAFCA ni sh. 50,000 wakati Mhazini, Mhazini Msaidizi na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni sh. 30,000.
Ajenda ya uchaguzi itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa Kawaida ambao mbali ya taarifa ya utendaji, Kamati ya Utendaji inayomaliza muda wake pia itawasilisha ripoti ya mapato na matumizi.
Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA Kinondoni inaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa TAFCA, Ramadhan Mambosasa.
IMETOLEWA NA TAFCA KINONDONI 

USHAURI WA KUANZISHA KOZI YA UKALIMANI NI FURSA MPYA YA AJIRA KWA WATANZANIA.

Posted by Esta Malibiche on APRIL 4,2017 IN NEWS

Coat_of_arms_of_Tanzania.svg
Jovina Bujulu –MAELEZO
Ubora na thamani ya lugha ya Kiswahili duniani unadhihirika kwa kukubalika kwake,  hali hii inayopelekea lugha adhimu ya Kiswahili kuendelea kukua na kutumika katika nchi mbalimbali duniani kijamii, kiuchumi na hasa kibiashara na ushirikiano wa kimataifa.
Mchango wa lugha hii inaipa hadhi kubwa nchi yetu ambayo ni kitovu cha lugha hii inayotumika kama lugha rasmi ya mawasiliano katika nyanja mbalimbali na pia ndiyo lugha unganishi inayotumiwa na watu wengi nchini.
Kihistoria, lugha ya Kiswahili imekuwa na mchango mkubwa kutokana na kutumika katika harakati za ukombozi  na pia kuwaunganisha Watanzania na kuwafanya wawe wamoja.
Mara baada ya Uhuru Tanzania ilianzisha Baraza la Kiswahili (BAKITA) na kupewa jukumu la kuimarisha na kueneza lugha hii , pia kuhakikisha inatumika kwa ufasaha pamoja na kukuza msamiati wake ili iweze kukidhi matumizi yake.
Mwaka 1968, lugha hii ilianza kutumika  kufundishia katika shule za msingi hapa nchini. Hatua hii ilimaanisha kila mwanafunzi wa shule ya msingi kuifahamu vizuri kwa kuiandika, kuisoma na kuielewa.
Aidha, historia ya kuikuza na kuieneza lugha hii imeanzia mbali, mwaka 1962 hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliitumia kuhutubia Bunge la Tanganyika, baada ya utawala wake, Rais aliyemfuatia, Ali Hassan Mwinyi aliendeleza matumizi ya Kiswahili katika shughuli mbalimbali za mawasiliano.
Naye Rais wa Awamu ya Tatu, Mhe.Benjamin Mkapa na Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete walifanikisha maendeleo ya lugha hii kwa kuhimiza matumizi fasaha katika nyanja za elimu, shughuli zote za Serikali, katika shughuli au mikusanyiko rasmi pamoja na matumizi mengine ya mawasiliano.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakikuwa nyuma katika kuhakikisha kinakuza, kinaeneza na kinakifanya Kiswahili kitambulike zaidi duniani.
Miongoni mwa jitihada hizi ni pamoja na kuanza kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano chuoni hapo ili kuipa msukumo kwa wananchi wa mataifa mengine yanayohitaji kujifunza lugha hii.
Katika kutambua juhudi hizi za Chuo, Balozi wa kwanza wa Kiswahili Barani Afrika, Mama Salma Kikwete, hivi karibuni alimkabidhi tuzo ya Kiswahili  Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa  Rwekaza Mkandara, ikiwa ni utambuzi wa mchango wake  kwa kurasimisha lugha hiyo  kutumika katika shughuli zote za Chuo na kitaaluma ikiwemo mikutano ya Baraza la chuo.
Aidha, Mama Salma alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kuwekeza katika kuendeleza lugha Kiswahili ili kuieneza kibiashara ndani na nje ya Bara la Afrika.
Kutokana na umuhimu wake katika mawasiliano hivi karibuni Bunge la Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki limeidhinisha lugha Kiswahili itumike katika mikutano yake ya Bunge.
Bunge hilo linajumuisha Wabunge kutoka katika nchi sita za jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini zimepitisha lugha hiyo kutumika katika nchi zao. Hatua hiyo ni mwanzo mzuri wa kukipaisha Kiswahili kimataifa.
Ni kutokana na muktadha huo, baadhi ya wataalamu wa lugha wameishauri Serikali kuanzisha kozi ya ukalimani katika vyuo vyake ili kuongeza idadi ya wakalimani hapa nchini hatua ambayo itawaongezea ajira wahitimu wa kozi hiyo.
Hadi sasa inakadiriwa kuwa idadi ya wakalimani nchini haizidi 20 mbao ndio wanaotoa huduma katika mikutano mbalimbali ya kimataifa.
Akizungumza jijini Dar es Saaam hivi karibuni Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili (BAKITA), Dkt. Selemani Sewangi alisema kuwa huu ni wakati muafaka kwa Tanzania kuanzisha kozi hiyo ili kupata wakalimani wa kutosha na wenye weledi, uwezo na maarifa katika kukalimani lugha ya Kiswahili kwenda lugha nyingine mbalimbali duniani.
Aliendelea kusema kuwa Tanzania haina kozi hiyo nyuoni, hivyo uwepo wa wataalamu hao hasa kipindi hiki ambacho nchi inapokuwa kiuchumi kwa kasi, kazi hiyo itoe mchngo wake ikizingatiwa sekta ya utalii inaendelea kuimarika na kuwa na ongezeko la wageni mbalimbali wakiwemo watalii, wawekezaji na wengine hatua ambayo itakuwa fursa ya kutangaza utajiri na maliasili zilizoko nchini mwetu.
 “Kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanatafsiri lugha ya Kiswahili wakidhani wanafanya taaluma ya ukalimani, jambo ambalo si sahihi kitaaluma, watu hawa hawawezi kupata ajira kutokana na kukosa vigezo vya elimu rasmi ya ukalimani” alisema Dkt. Sewangi.
Akifafanua juu ya maana hasa ya ukalimani Dkt. Sewangi alisema kuna mkanganyiko  kati ya kutafsiri na kukalimani, ambapo alisema kuwa kutafsiri kunaweza kufanywa na mtu yoyote, lakini kukalimani ni lazima mtu asomee kozi maalumu  ili aweze kutambulika kimataifa.
Katika kuonyesha msisistizo wa kuhakikisha kuwa Kiswahili kinapaa kimataifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa Kiswahili ni lugha ya Waafrika na inazungumzwa katika nchi nyingi na imekubalika kutumika katika mikutano ya Umoja wa Afrika, hivyo aliwashauri Watanzania kuipenda lugha hiyo.
Hivi karibuni Tanzania ilitembelewa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Haile Mariam Dessalegn ambapo alisema kuwa nchi yake imekubali kuchagua Chuo Kikuu kimoja ili lugha ya Kiswahili ifundishwe nchini mwake kwa kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Aidha, Rais Dkt. Magufuli aliahidi kupeleka wataalamu wa lugha ya Kiswahili ili wafundishe katika chuo kitakachoteuliwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia kufundisha lugha hiyo.
Kwa kuzingatia umuhimu wa lugha ya Kiswahili huu ni wakati muafaka kwa watunga Sera, Mamlaka husika na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuanzisha kozi ya ukalimani katika vyuo vyetu ili wahitimu wapate fursa za ajira katika nchi mbalimbali  na hivyo kuzidi kuipa hadhi  na kuieneza lugha ya Kiswahili ambayo inakisiwa kuwa ni lugha ya 10 miongoni mwa lugha 600 zinazozungumzwa duniani.

SHULE YA SONGAMBELE YA MJI MDOGO WA MIRERANI KUJENGEWE MADARASA SABA

Posted by Esta Malibiche on APRIL 4,2017

A
Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Faisal Shabhai akizungumza kwenye viwanja vya shule ya msingi Songambele Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, alipoahidi wananchi kuwajengea vyumba saba vya madarasa.
A 1
Mkazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Japhary Matimbwa akiushukuru uongozi wa kampuni ya TanzaniteOne baada ya kuahidi kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele. A 2
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Jackson Sipitieck akiushukuru uongozi wa kampuni ya TanzaniteOne baada ya kuahidi kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele.
…………….
Kampuni ya TanzaniteOne kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Faisal Juma Shabhai ameahidi kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele ya mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambayo yameweka ufa.
Tangu mwaka 2013 madarasa hayo yaliweka ufa kutokana na kupitiwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kwenye eneo hilo.
Kutokana na hali hiyo uongozi wa shule hiyo uliamua kuyafunga madarasa hayo na ofisi ya walimu, wakihofia kupaata madhara kutokana na hitilafu hiyo iliyotokana na tatizo hilo.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Shabhai alisema yeye binafsi atajenga madarasa matatu na wakurugenzi wenzake wa kampuni hiyo Hussein Gonga na Riziwani nao watajenga mengine manne yaliyobakia.
Alisema kampuni hiyo imeamua kujenga madarasa hayo ili kusaidia jamii inayozunguka maeneo hayo ambayo wao wamewekeza kwenye madini ya Tanzanite.
“Pamoja na hayo jamii ya eneo hili nanyi mnapaswa kutuunga mkono kwa kutumia nguvu zenu ikiwemo kubeba majabali, matofali na kusogeza mchanga ili tushiriki pamoja,” alisema Shabhai.
Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Simanjiro Jackson Leskar Sipitieck aliipongeza kampuni ya TanzaniteOne kwa kufikia uamuzi huo kwani utasaidia watoto wa eneo hilo kupata elimu.
“Mwezi huu kutakuwa na baraza la madiwani na kupitia nafasi hiyo tutatoa shukurani zetu rasmi kwa kutuunga mkono baada ya kujenga madarasa hayo saba ya shule hiii ya Songambele,” alisema Sipitieck.

MASHABIKI WAJITOKEZA KUIPOKEA TIMU YA SIMBA MKOANI GEITA

Posted by Esta Malibiche on APRIL 4,2017 IN MICHEZO

Timu ya Simba imetua Mkoani Geita  ikitokea Kagera  kwaajili ya kuweka kambi ya siku nne kujiandaa na mchezo Dhidi ya Mbao Fc na Toto zote za Jijini Mwanza Mchezo ambayo itapigwa kwenye Dimba la CCM Kirumba.
 
Ikiwa Mkoani Geita Simba inatarajia kucheza mchezo wa Kirafiki na timu ya Geita Gold Sport Siku ya Jumatano mechi ambayo itachezwa kwenye  uwanja wa shule ya msingi  Waja.
 
Kwa Mujibu wa Nahodha wa Kikosi cha Simba Jonas Mkude amewataka mashabiki kuendelea kuhishabikia timu hiyo na kwamba wataakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo  ambayo imebakia.
Hata Hivyo kwa upande wake Mussa Hassan Mgosi ameelezea kuwa wamejipanga vizuri kukutana na Mbao Fc siku ya Jumatatu na kwamba hawatawaangusha mashabiki wao na ni vyema wakasahau ambayo yamepita na  mashabiki wakashikamana na timu ili kuweza kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.



IMEANDALIWA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE BLOG.

KAIMU MKURUGENZI MKUU NIDA AFANYA ZIARA KUKAGUA SHUGHULI ZA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOANI IRINGA

Posted by Esta Malibiche on APRIL 4,2017 IN NEWS

 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida Ndugu Andrew W. Massawe wakati alipofanya ziara Wilaya ya Mufindi 
 
 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ndugu Andrew W. Massawe yuko mkoani Iringa kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu; ambapo pamoja na mambo mengine anatazamiwa kushuhudia sherehe za uzinduzi wa utoaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilaya ya Mufindi na kuzinduliwa kwa kampeni ya Usajili wa wananchi na wageni wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wanaoishi mkoani humo.
Katika ziara yake; leo amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ambaye amemweleza Mkurugenzi huyo hatua kubwa ambayo Wilaya yake imefikia mpaka sasa katika kuwasajili wananchi, ambapo takribani asilimia 60 ya wananchi wameshasajiliwa, kuchukuliwa alama za vidole na baadhi Vitambulisho vyao kuzalishwa, mbali na kukamilika kwa zoezi la kuwasajiliwa Watumishi wa Umma.
Akiwa Wilayani Mufindi Mkurugenzi huyo ametembelea na kukagua shughuli katika ofisi ya Usajili na kukagua vifaa vinavyotumika katika Usajili. Aidha; amefanya mazungumzo na wadau wakubwa wa NIDA likiwemo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Mafinga namba 841, kinachoongozwa na Kanali Hamisi Maiga; ambaye amehakikishia NIDA ushirikiano zaidi katika kufanikisha zoezi la kuwasajiliwa wananchi.
Mkurugenzi huyo pia alitembelea Kata za Boma na Upendo na kukutana na watendaji wa Kata hizo pamoja na kufanya mazungumzo na Diwani wa Kata ya Boma Mhe. Julist Kisoma (Chadema) ambaye ameishukuru NIDA kwa kufanikisha zoezi la kuwasajili wa wananchi.
Mbali na kukagua shughuli za Usajili Wilaya ya Mufindi; pia amekutana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa bwana Joseph Meshacky Chitnka ambaye alieleza mikakati ya Wilaya yake katika kuhakikisha watu wote wanafikiwa kwa wakati kusajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ilianza utekelezaji wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa mara ya kwanza mkoa wa Iringa mwezi Septemba, 2016 kwa kuanza na kuwasajili Watumishi wa Umma zoezi lililomalizika hivi karibuni na kuanza mikakati ya kuwasajili wananchi na Wageni.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndugu Andrew W. Massawe (katikati kulia), wengine wa kwanza kushoto ni ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na wa kwanza  kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu Bernard.
 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Mufindi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA; Ndugu Andrew W. Massawe
 Ndugu George Mushi Afisa Usajili Mkoa wa Iringa (RRO), akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, kuhusu vifaa vinavyotumika kwenye usajili wa wananchi alipotembelea ghala la kuhifadhi vifaa wilayani Mufindi
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA akiwa na Kanali Hamisi Maiga Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Mafinga namba 841, wakati alipotembelea kambi hiyo.
 Mtendaji wa Kata ya Boma; Joseph Kiwele akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la usajili wananchi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndugu Andrew W. Massawe akisalimiana na Diwani wa Kata ya Boma Mhe. Julist Kisoma (Chadema).
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Andrew W. Massawe akiweka saini kwenye ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa bwana Joseph Meshacky Chitinka wakati alipofanya ziara.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA (Katikati) akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa bwana Joseph Meshacky Chitinka (katikati kulia). Wengine ni Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho (wa kwanza kushoto) na  wa kwanza kulia ni ndugu George Mushi, Afisa Usajili Mkoa wa Iringa.

EALA SPEAKER ADDRESSES IPU ASSEMBLY IN BANGLADESH

Posted by Esta Malibiche on APRIL 4,2017 IN NEWS

 Speaker of the Senate of Kenya, Rt Hon Ekwe Ethuro addresses the Assembly where he called for urgent international action to save millions of people from famine and drought 
 The EALA Speaker, Rt Hon Daniel F. Kidega consults with Hon Dora Byamukama at the 136th Inter-Parliamentary Union Assembly in Dhaka, Bangladesh 
  Rt Hon Daniel F. Kidega, Speaker of EALA addresses the IPU Assembly. 
 A section of the delegates in attendance at the global Parliamentarians meet.
…tells Parliamentarians to take “bull by the horns” in redressing inequalities

East African Legislative Assembly, Dhaka, Bangladesh: 3rd April 2017: EALA Speaker, Rt Hon Daniel Fred Kidega is calling on global Parliamentarians to pay more attention in ensuring promotion of economic stimulus programmes that address social challenges and support local value chains in a bid to narrow the widening poverty gaps and redress inequalities. 

At the same time, Rt Hon Kidega says Parliaments should appropriate more resources in the States’ budgets to check on rising inequalities and hold Executive accountable on the same. 

The Speaker was addressing the 136th Inter-Parliamentary Union Assembly (IPU) taking place in Dhaka, Bangladesh.    The annual event which is themed: Redressing inequalities: Delivering on dignity and well-being for all” brings together over 50 Speakers and 1400 legislators from the globe.

In his remarks, Rt Hon Kidega maintained that despite the emergence of BRIC countries and other economies as well as attempts to generate wealth, much more was needed to reduce the inequality and to raise the standards of living.

He said the East African Community region had similarly been gravely affected by inequalities. “The State of East Africa Report 2016 depicts not all citizens have seen or felt the benefits of increasing national GDP figures at the individual/family front. If anything, life continues to be harsher and harder. The economic boom has not generated the jobs as was expected, while levels of poverty and malnutrition remain high”, the Speaker said, while remaining optimistic the trend could be reversed.

The Speaker cited issues contributing to inequality as disparity in income levels throughout the world, uncertain political environments, the gender norms and stereotypes and the imbalance of economic power.

In many countries, Rt Hon Kidega said, fruits of economic development increasingly failed to reach those who deserve the same – instead benefitting companies, financial services and vested interests. He said the rate of unemployment in the globe was similarly high.

“Statistics in East Africa reveals that 7 out of the 10 persons you see walking in the streets are jobless, while another 6 out of 10 live in informal settlements. Yet, the largest population, the youth, constitute about 8 out of 10 persons and their age range is below 30 years”, Such is replicable in many parts of the globe”, he noted.

The Speaker called on Parliaments to enact relevant legislation to make greater impact.   He informed the convention that EALA had legislated a number of pieces that protect society and address inequalities including; the EAC Persons with Disabilities Bill, 2016, the EAC Gender, Equity and Equality Bill, 2016, the EAC Conflict Management Bill, 2011 and the EAC Human and Peoples Rights Act 2011.

“He further called for dialogue to resolve political issues saying politically instigated inequalities more often than not arise from disputed elections and uncertainties which result into conflicts and sometimes wars.    The ramifications are sometimes too much to bear leading to refugee crises and instabilities in the nations”, Rt Hon Kidega said.

Analysts contend that Poverty reduction is often compromised by income inequality. The International Monetary Fund (IMF) urges poor and resource rich nations to simultaneously explore reduction of inequality and bolster long-term economic growth.  However, inequality correlates to shorter spells of economic expansion and volatility to crises.  

The 136th IPU was opened by the Prime Minister of the Republic of Bangladesh, Hon Sheikh Hasina at the Parliament of Bangladesh yesterday. The Prime minister thanked delegates for electing Bangladesh as the chair of both Inter Parliamentary Union (IPU) and Commonwealth Parliamentary Association (CPA). The Prime minister mentioned her government’s short, medium and long-term initiatives for the development of the country and said the government is making stride to build the country in a planned way.

“The 100 Million young people are prepared to make the world a better place. Let us not make them frustrated. They are the face of change and let us globalise human compassion”, he said.

The Emergency items include a call for urgent international action to save millions of people from famine and drought in parts of Africa and the Yemen jointly presented by the Republic of Kenya together with Belgium and the United Kingdom. Speaker of the Senate of Kenya, Rt Hon Ekwe Ethuro, presented the merged proposal to the Assembly yesterday.

“We need to request for international organisations to come to the aid of the affected nations.  Without global action, people will simply starve to death”, the Speaker remarked.The Speaker of the Parliament of Uganda, Rt Hon Rebecca Kadaga and the Speaker of the Burundi National Assembly, Rt Hon Pascal Nyabenda also addressed the Assembly.

In attendance also are a delegation of the Parliament of Rwanda led by the Deputy Speaker and legislators from the Transitional Assembly of the Republic of South Sudan.

The Inter-Parliamentary Union (IPU) is the global organization of national Parliaments. It works to safeguard peace and drives positive democratic change through political dialogue and concrete action. To that end, IPU fosters contacts, co-ordination, and the exchange of experience among Parliaments and Parliamentarians of all countries. IPU also contributes to the defence and promotion of human rights - an essential factor of Parliamentary democracy and development.  EALA is an Associate Member of the IPU.