Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumatatu, 6 Machi 2017

WAZIRI NAPE NNAUYE AFUNGA FAINALI ZA KOMBE LA ULEGA CUP MKURANGA MKOANI PWANI

Posted by Esta Malibiche on MARCH 6,2017 IN MICHEZO

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwasalimia Waamuzi wa mpira wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.

Baadhi wa Wakazi wa Mkuranga Mkoani pwani wakishiriki zoezi la uchangiaji damu 05/03/2017 wakati wa fainali za Kombe la Ulega lililoandaliwa na Mbunge wa Wilaya hiyo, Mhe. Abdallah Ulega.

Baadhi wa Wakazi wa Mkuranga Mkoani pwani walioshiriki zoezi la uchangiaji damu 05/03/2017 wakati wa fainali za Kombe la Ulega lililoandaliwa na Mbunge wa Wilaya hiyo, Mhe. Abdallah Ulega wakipokea zawadi za jezi na doti za khanga ikiwa ni sehemu za motisha.

Mbunge wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega (aliyevaa tisheti la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakazi wa Mkuranga Mkoani pwani walioshiriki zoezi la uchangiaji damu 05/03/2017 wakati wa fainali za Kombe la Ulega lililoandaliwa na Mbunge wa Wilaya hiyo

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwasalimia wachezaji wa timu ya mpira ya Kisiju wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akimpongeza Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega kwa juhudi zake za muleta maendeleo kaaika jimbo lake na udahmini wake wa kuanzisha Kombe la Ulega ambapo fainali za kombe hilo zimefanyika jana 05/03/2017 Wilayani hapo.

Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na wageni waalikwa pamoja na wakazi wa wilayani hapo kuhusu maendeleo ya jimbo lake na lingo la kuanzisha Kombe la Ulega ambapo fainali za kombe hilo zimefanyika jana 05/03/2017 Wilayani hapo.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kisiju Wilayani Mkuranga wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Tengelea Wilayani Mkuranga wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Timu za moira za Kisiju na Tengelea wakichuana kuwania kombe la Ulega lililoandaliwa na Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega ambapo fainali hiyo imechezwa jana 05/03/2017 Wilayani hapo.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye pamoja na wageni engine walioalikwa wakifuatilia mpambano kati ya Timu ya mpira ya Kisiju na Tengelea wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

VIVUTIO VYA UTALII TANGU ENZI ZA MKOLONI VILIVYOPO SHULE YA SEKONDARI YA IYUNGA JIJINI MBEYA

Posted by Esta Malibiche on MARCH 06,2017 IN NEWS

Kamati ya Utalii ya Jiji la Mbeya iliyopo chini ya Halmashauri ya Jiji kupitia kwa Afisa Utalii Bi.Levina Modest jana ilifanya ziara ya kuitembelea Shule ya Sekondari Iyunga iliyopo Mkoani hapo kwa kushirikiana na wadau wakubwa wa masuala ya Utalii Jijini Mbeya, Uyole Cultural Tourism Enterprises chini ya Mratibu wake Amos Mwamugobole na Asasi nyingine isiyo ya kiserikali iitwayo ELIMISHA chini ya Mkurugenzi wake Bw.Festo Sikagonamo.
Katika Ziara hiyo wajumbe wa Kamati walionyeshwa Vitu mbalimbali vilivyotengenezwa toka enzi za  Mkoloni Mjerumani. Akiongea kwa bashasha kuu Mwalimu mwandamizi wa Michezo,Habari na Utamaduni Sekondari ya Iyunga, Mwalimu Emmanuel Michael ameelezea kwa marefu kuhusu kumbukumbu za kale zilizopo shuleni hapo ikiwemo kengere ya kale,birika,bwawa la kuogelea,mahandaki kwa ajili ya ulinzi,kiti cha kukaa cha kale,matanki ya maji pamoja na majengo vyote vikiwa vilitengenezwa mnamo mwaka 1925.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Utalii ,ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sisimba Mhe.Geofrey Kajigili amemuomba Mwalimu Michael kwa niaba ya Uongozi wa Shule hiyo kushirikiana na Kamati hiyo ili kupata Wazee wa zamani waiishio maeneo hayo ili waweze kupata historia nyingine nyingi kuhusu Utawala wa Kikoloni na taarifa zingine za kina.
Naye Afisa Utalii Bi.Levina amesema kuna kila sababu ya kuboresha mazingira ya Shule hiyo ili yawe ya Kitalii zaidi kwani yataisaidia Halmashauri kujitangaza na kujiingizia mapato huku Shule na wanajamii wa Sekondari ya Iyunga watanufaika pia kwa kuwa na Vivutio hivyo.
Mwishowe,Mwalimu Emmanuel Michael aliushukuru Uongozi wa Halmashauri ,Kamati ya Utalii kwa kuliona suala la Utalii kuwa ni jema na kuamua kulishupalia na kuiahidi Kamati hiyo kushirikiana nayo bega kwa bega katika kufanikisha suala hilo zuri huku akiiomba Kamati utekelezaji mwema wa majukumu yake.

Kiti hiki cha kukalia ni moja ya kivutio shuleni hapo kilitengenezwa zaidi ya miaka 90 iliyopita enzi za Utawala wa Kikoloni wa Kijerumani

Ukuta huu ulijengwa na Wajerumani pembezoni mwa Mto Nzovwe kwa ajili ya Ulinzi na Usalama kwani chini ya Ukuta huu kuna Handaki kubwa linalounganisha maeneo ya ndani ya shule na nje ya eneo hilo

Hili ni birika la kale lililokuwa likitumika na Utawala wa Kijerumani kwa ajili ya kuhifadhia maji na vitu vingine vinavyofanana na hivyo ambalo Uongozi wa Shule ya Sekondari Iyunga wamelitunza vizuri hadi hivi sasa

Hiki ni kifaa kitumikacho Kuratibu masuala mbalimbali kuhusu Hali ya Hewa (Stevenson Screen) kilichojengwa na kutumika tangu enzi za mkoloni Mjerumani

Jengo hili ni Ukumbi uliojengwa na Mkoloni ambao ndani yake kuna Handaki linalotoka mpaka nje ya maeneo ya Shule hiyo, Juu kulia karibu na dirisha ni Kengere ya Mkoloni inayotumia umeme iliyokuwa ikitumika kutoa taarifa mbalimbali kama kuna hatari au kuita watu mkutanoni kwa ajili ya kujuzwa yanayojiri

Kamati ya Utalii ya Jiji, Waandishi wa Habari pamoja na Mwalimu mwenyeji Mwl Emmanuel Michael wakiwa eneo lilipo Bwawa la Kuogelea lililojengwa na Enzi za Mkoloni

Afisa Habari wa Halmshauri ya Jiji la Mbeya Bi.Jacqueline Msuya akitoka ndani ya Handaki pamoja na wajumbe wengine waliokuwa wakizungukia maeneo ya utalii ndani ya Shule ya Sekondari ya Iyunga,Jijini Mbeya

Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii na Diwani wa Kata ya Sisimba Mhe.Geofrey Kajigili (wa kwanza kushoto) akiwa na Afisa Utalii wa Jiji Bi.Levina Modest wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa mwenyeji wao Mwalimu Emmanuel Michael wa Sekondari ya Iyunga

Mwalimu Emmanuel Michael ,Mwalimu mwandamizi wa Michezo,Habari na Utamaduni akielekeza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Utalii ndani ya Handaki lililopo shuleni hapo
PICHA YA PAMOJA: Wajumbe wa Kamati, Waandishi wa Habari na Mwalimu mwenyeji kwenye viunga vya Shule ya Sekondari Iyunga

Wajumbe wa Kamati ya Utalii wakifurahia mara baada ya Kuelezwa mambo mbalimbali na kuyatembelea, hapa wakiwa kwenye pozi la kuruka juu ndani ya Bwawa la Kuogelea lillilojengwa tangu Enzi za Mkoloni miaka 90 iliyopita
FADHIRI ATICK 01:36 (2 hours ago) to me
Kamati ya Utalii ya Jiji la Mbeya iliyopo chini ya Halmashauri ya Jiji kupitia kwa Afisa Utalii Bi.Levina Modest jana ilifanya ziara ya kitalii kuitembelea Shule ya Sekondari Iyunga iliyopo Mkoani hapo kwa kushirikiana na wadau wakubwa wa masuala ya Utalii Jijini Mbeya, Uyole Cultural Tourism Enterprises chini ya Mratibu wake Amos Mwamugobole na Asasi nyingine isiyo ya kiserikali iitwayo ELIMISHA chini ya Mkurugenzi wake Bw.Festo Sikagonamo.
Katika Ziara hiyo wajumbe wa Kamati walionyeshwa Vitu mbalimbali vilivyotengenezwa toka enzi za  Mkoloni Mjerumani. Akiongea kwa bashasha kuu Mwalimu mwandamizi wa Michezo,Habari na Utamaduni Sekondari ya Iyunga, Mwalimu Emmanuel Michael ameelezea kwa marefu kuhusu kumbukumbu za kale zilizopo shuleni hapo ikiwemo kengere ya kale,birika,bwawa la kuogelea,mahandaki kwa ajili ya ulinzi,kiti cha kukaa cha kale,matanki ya maji pamoja na majengo vyote vikiwa vilitengenezwa mnamo mwaka 1925.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Utalii ,ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sisimba Mhe.Geofrey Kajigili amemuomba Mwalimu Michael kwa niaba ya Uongozi wa Shule hiyo kushirikiana na Kamati hiyo ili kupata Wazee wa zamani waiishio maeneo hayo ili waweze kupata historia nyingine nyingi kuhusu Utawala wa Kikoloni na taarifa zingine za kina.
Naye Afisa Utalii Bi.Levina amesema kuna kila sababu ya kuboresha mazingira ya Shule hiyo ili yawe ya Kitalii zaidi kwani yataisaidia Halmashauri kujitangaza na kujiingizia mapato huku Shule na wanajamii wa Sekondari ya Iyunga watanufaika pia kwa kuwa na Vivutio hivyo.
Mwishowe,Mwalimu Emmanuel Michael aliushukuru Uongozi wa Halmashauri ,Kamati ya Utalii kwa kuliona suala la Utalii kuwa ni jema na kuamua kulishupalia na kuiahidi Kamati hiyo kushirikiana nayo bega kwa bega katika kufanikisha suala hilo zuri huku akiiomba Kamati utekelezaji mwema wa majukumu yake.

Kiti hiki cha kukalia ni moja ya kivutio shuleni hapo kilitengenezwa zaidi ya miaka 90 iliyopita enzi za Utawala wa Kikoloni wa Kijerumani

Ukuta huu ulijengwa na Wajerumani pembezoni mwa Mto Nzovwe kwa ajili ya Ulinzi na Usalama kwani chini ya Ukuta huu kuna Handaki kubwa linalounganisha maeneo ya ndani ya shule na nje ya eneo hilo

Hili ni birika la kale lililokuwa likitumika na Utawala wa Kijerumani kwa ajili ya kuhifadhia maji na vitu vingine vinavyofanana na hivyo ambalo Uongozi wa Shule ya Sekondari Iyunga wamelitunza vizuri hadi hivi sasa

Alhamisi, 2 Machi 2017

WAZIRI WA AFYA AZINDUA RIPOTI YA HALI YA NDOA ZA UTOTONI

Posted by Esta Malibiche on MARCH 2,2017 IN NEWS

HER1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akiwa tayari kwa uzinduzi wa Ripoti ya hali ya ndoa za utotoni Nchini.
HER2
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akionesha Ripoti ya hali ya ndoa za utotoni Nchini.
HER3
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akionesha Ripoti ya hali ya ndoa za utotoni Nchini.
HER4
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akiwa na viongozi wa dini katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua  Ripoti ya hali ya ndoa za utotoni Nchini
……………………………………………………………………..
Na Anthony Ishengoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Ally Mwalimu ameagiza walimu wakuu wote wa shule za msingi chini kutekeleza marekebisho ya sheria ya elimu ya mwaka 2016 kwa vitendo kwa kuwataka kuwasilisha taarifa za wasichana waliopata mimba shuleni kwa kila kamishina wa elimu kama ilivyo agizo la sheria hiyo.
Aidha amewaagiza watendaji wa Wizara yake kufuatilia taarifa za wanafunzi wakike walioacha shule kutoka kwa kila Afisa Maendeleo wa Jamii katika ngazi ya Wilaya kuwapatia mrejesho wa kina kuhusu agizo lake kwa walimu wakuu kama hatua muhimu ya kutekeleza agizo la sheria ya elimu kama ilivyofanyiwa marekebisho na bunge mwaka 2016.
Amesema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa ripoti ya hali ya mimba za utotoni hapa nchini iliyofanyika kote nchini chini ya mtandao wa mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali ikiongozwa na shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto Tanzania, ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Ummy amewambia wajumbe walioshiriki ufunguzi huo kuwa kwa kuwa mabadiliko ya sheria ya ndoa hususani kifungu namba kumi na tatu cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 hayajafanyika ni bora kwenda mbele zaidi kutekeleza sheria ya elimu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 ili kutekeleza kwa vitendo hatua za kupinga ndoa za utotoni.
Amesema kuwa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kimsingi inahalalisha uwepo wa vitendo vya ndoa za utotoni na kuahidi kuwa ataendelea kupigania marekebisho katika ndoa hiyo mara baada yakuwasiliana na waziri wa sheria na mambo ya katiba.
Katika kuhakikisha Serikali na Mashirika yasiyo ya kiserikali yanapambana na tatizo la ndoa za utotoni ameyataka mashirika hayo kuweka nguvu zake katika maeneo ya vijijini kwani ofisi nyingi za mashirika hayo zimejikita maeneo ya mjini hasa katika jiji la Dar es Salaam.
Aidha amehaidi kuwa serikali itaboresha mazingira ya mtoto wa kike kusoma ikiwemo ujenzi bora wa vyoo pamoja na uendelezaji wa sera rafiki na sheria kwa mtoto wa kike kujipatia elimu bila vikwazo ikiwemo elimu ya Afya na uzazi ili mtoto wa kike aweze kutambua thamani yake katika jamii na taifa kwa ujumla.
Ufunguzi huo umefanyika wakati serikali na mashirika ya yasiyo ya kiserikali wakiendelea kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake ambayo kilele chake ni Machi 8, mawaka huu.

MKUU WA MKOA WA IRINGA AMINA MASENZA AZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI

Posted by Esta Malibiche on MARCH 2,2017 IN NEWS
 Katika kuelekea maadhimisho ya  siku ya wanawake Duniani,Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza,leo hii amezindua jukwaa la uwezeshaji wanawake mkoa wa IRINGA.Akizindua jukwaa hilo mkuu wa mkoa amewasihi wanawake kuitumia vizuri mikopo wanayoichukua katika Taasisi cha fedha wahakikishe inatumika katika lengo mahususi na si vinginevyo ili waweze kurejesha bila tatizo lolote.

 Meneja wa Bank ya posta mkoa wa Iringa Athony Kayanda akitoa Taarifa.
Meneja wa SIDO Mkoa wa Iringa Neserian Laiza akiwasilisha Taarifa

 Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa Ritha Kabati akizungumza katika uzinduzi wa jukwaa la wanawake,lililofa leo hii katika ukumbi wa siasa ni kilimo Iringa    Afisa Elimu na huduma kwa walipa kodi TRA Kefa Mwambene akitoa Taarifa juu ya ulipaji kodi

Wajumbe  wa jukwaa  la wanawake wakiwa katika  uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa siasa ni kilimo Iringa

Mstahiki meya wa Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe wa pili  kulia  akiwa katika  uzinduzi wa  jukwaa la  wanawake kiuchumi

 Wajumbe  wa jukwaa  la wanawake wakiwa katika  uzinduziuliofanyika katika ukumbi wa siasa ni kilimo Iringa