Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Ijumaa, 2 Desemba 2016

IGA yatoa mafunzo ya Usimamizi wa Miradi ya Jotoardhi

Posted by Esta Malibiche on Dec 2,2016 in NEWS

Mtaalamu wa Nishati kutoka Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) Dkt. Thrainn Fridrikson aliwapongeza TGDC kwa jitihada walizofikia na kuahidi kuendeleza ushirikiano na TGDC pamoja na IGA wakati wote wa mchakato wa kuwajengea uwezo wataalamu wa jotoardhi nchini.

Mhandisi Uchorongaji, Amani Christopher kutoka TGDC alishukuru wakufunzi na wafadhili kwa niaba ya TGDC “mafunzo haya yana tija sana kwetu hasa waandisi tuliotoka katika mufunzo ya vitendo nchini Kenya kwa kuwa sasa tunaweza kuowanisha utekelezaji na usimamizi wa miradi ya jotoardhi, hasa kipengele cha uchorongaji” alisema Amani.

Mafuzo hayo yalihusu usimamizi katika manunuzi, taratibu za kisheria, uchorongaji na fedha za kugharamia miradi.
Kaimu Meneja Mkuu Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Kato Kabaka akizungumza na wataalamu wa nishati ya jotoardhi kutoka TGDC, Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) na Chama cha Kimataifa cha Jotoardhi (IGA) wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wataalamu wa jotoardhi nchini.
Mtaalamu kutoka Chama cha Kimataifa cha Jotoardhi (IGA) Mhandisi Cristian Scanzoni akiwasilisha mada kuhusu usimamizi wa uchorongaji visima vya jotoardhi wakati wa miradi. Mafunzo hayo maalum yalifadhiliwa na ESMAP na yalilenga kuwajengea uwezo wataalamu wa Jotoardhi Tanzania.
Wataalamu wa nishati ya jotoardhi kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) na Chama cha Kimataifa cha Jotoardhi (IGA) katika majadiliano wakati wa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo  yaliyafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki ya Dunia Tanzania.
Mtaalamu wa Nishati kutoka Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) Dkt. Thrainn Fridrikson akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa nishati ya jotoardhi nchini, mafunzo hayo yamedhaminiwa na ESMAP na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Banki ya Dunia Tanzania.






Na Johary Kachwamba - TGDC

Wataalamu kutoka Chama cha Kimataifa cha Jotoardhi (International Geothermal Association-IGA) wametoa mafunzo ya usimamizi wa miradi ya jotoardhi kwa wataalamu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC).

Mafunzo haya yanafadhiliwa na Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) katika jitihada za kuijengea uwezo TGDC ili iweze kusimamia miradi ya jotoardhi ambayo bado ni teknolojia ngeni nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Meneja Mkuu TGDC, Mhandisi Kato Kabaka alitoa shukrani kwa ESMAP na kusema “ni fursa muhimu kwetu kama kampuni katika maandalizi ya kuendeleza nishati ya jotoardhi inayolenga kusaidia taifa kufikia malengo yaliyo katika dira ya 2025”.

CHAMA CHA AFYA YA JAMII TANZANIA (TPHA) CHAPATA VIONGOZI WAPYA

Posted by Esta Malibiche on Dec 2,2016 in NEWS
 Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (wa nne kushoto), akiwa na viongozi wenzake wateule waliochaguliwa katika mkutano mkuu wa chama hicho 2016 jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Dismas Vyagusa, Violeth Shirima, Dk. Godfrey Swai, Dk.Nderineia Swai, Dk. Feliciana Mmasi,  Dk. Mwanahamisi Hassan na Dk.Elihuruma Nangawe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho aliyemaliza muda wake.
Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), aliyemaliza muda wake Dk.Elihuruma Mangawe (katikati), akiongoza kikao cha mkutano mkuu wa chama hicho. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TPHA, Fabian Magoma na kulia ni Ofisa Utawala wa chama hicho, Erick Goodluck.
 Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (kulia) akiwaelekeza jambo wajumbe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi uliompa nafasi hiyo.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wa mkutano huo.
Usikivu katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Afya ya Jamii (TPHA) kimepata viongozi wapya ambapo kimemchagua Dk. Shaibu Mashombo kuwa Mwenyekiti.
Mashombo alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 35 na kumbwaga Feliciana Mmassy aliyepata kura 10 na kura moja ikiharibika.
Katika nafasi ya Mhariri Mkuu Dk.Godfrey Swai aliibuka kidedea dhidi ya Ndeniria Swai aliyepata kura 15 na kura tisa zilikataa ambapo katika nafasi ya Katibu Mwenezi wagombea walikuwa wawili Elizabeth Nchimbi aliyepata kura 15 na Ndeniria Swai ambaye aliibuka mshindi kwa kupata kura 29 huku kukiwa hakuna kura iliyopotea.
Katika nafasi ya Mtunza Fedha licha ya kuwepo na ushindani makali aliyeibuka mshindi ni Mwanahamisi Hassan ambaye alipata kura kura 20 dhidi ya mgombea mwenzake Violeth Shirima aliyepata kura 24.
Nafasi ya Katibu wa Mipango ilikwenda kwa Dk. Mwanahamisi Hassan aliyepata kura 38 dhidi ya Othman Shem aliyeambulia kura tano huku Feliciana Mmasi na Dismas Vyagusa wakishinda nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji.

ULEGA AENDELEA NA ZIARA YA KUWASHUKURU WANANCHI JIMBONI KWAKE

Posted by Esta Malibiche on Dec 2,2016 in MICHEZO

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibuyuni Kata Panzuo, alipokuwa katika ziara yake ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua, pia kusikiliza kero zao, hususani ile ya Mifugo kuharibu vyanzo vya maji pamoja na mazao yao.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkuruwili, alipokuwa katika ziara yake ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua, pia kusikiliza kero zao.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Mbulali FC inayo shiriki kombe la Ulega.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Nyatanga FC.





LUKUVI ATATUA MIGOGO YA ARDHI YA WANANCHI WA KASULU NA KIBONDO MKOANI KIGOMA

Posted by Esta Malibiche on Dec 2,2016 in NEWS

luku-4

Wakazi wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wenye migogoro ya ardhi wakimsikiliza Mh. William Lukuvi wakati akitatua migogoro yao ya ardhi.

luku
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akipokelewa kwa maandamano na mabango na mamia ya wananchi wa kata ya Nyarubanda katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma ambao kwa muda mrefu wamekuwa na kero ya ardhi baada ya mmoja wa wakazi wa kijiji hicho kujimilikisha eneo la serikali ya kijiji.
luku-1
Wananchi wa kata ya Nyarubanda wakimpeleka kumuonesha eneo la mgogoro Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akiwa na Mbunge wa Kigoma Vijijini Mhed. Peter Serukamba (mwenye shati jeupe).
luku-2
 Wakazi wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wakiwa na nyaraka za migogoro ya ardhi walizo zileta ili kumpatia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi aweze kuitatua migogoro yao.
luku-3
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akitatua migogoro ya ardhi ya wakazi wa Kasulu mara baada ya kupokea malalamiko hayo.


Hassan I. Mabuye
Information Officer
The Ministry of Lands, Housing
and Human Settlements Development

Dar es salaam, Tanzania

MWENYEKITI WA BODI YA TANAPA KUONGOZA WANANCHI NA WAANDISHI WA HABARI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA MAATHIMISHO YA MIAKA 55 YA UHURU

Posted by Esta Malibiche on Dec 2,2016 in NEWS
 
 picha wa kwanza  kushoto ni meneja  Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi  wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa kampuni ya Zara  Zainabu  Ansell wakati wa mkutano wao na waandisi wa habari juu ya   maandalizi ya miaka 55 ya uhuru ambayo yanatarajiwa kufanyika december 9
 

 Mkurugenzi wa mamlaka ya hifadhi za taifa (Tanapa) Allen Kijazi akiongea na waandishi wa habari
meneja  Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi  wa kwanza kushoto ni Afisa uhusiano wa Tanapa Paschal Shelutete
 
 Habari  Picha na Woinde Shizza,Arusha
Aliyekuwa mkuu wa majeshi na mwenyekiti wa bodi ya tanapa jenerali msataafu geogre waitara anatarajiwa kuongoza  msafara wa zoezi la kupanda mlima kilimanjaro desemba 5 hadi kumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya  uhuru wa tanzania,
Aidha katika msafara huo wa kupanda mlima kilimanjaro watakuwepo pia wanajeshi kutoka jeshi la wananchi tanzania pamoja na wanahabari ambao watakuwa wanahabarisha jamii kuhusiana na tukio hilo.
 
Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa tanapa allan kijazi alisema kuwa mwaka huu tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru na hivyo shrikia hilo imeshirikiana na kampuni ya utalii ya zara pamoja na bodi ya utalii (ttb) kuandaa zoezi la kupanda mlima kilimnajro ili kuweza kuhamasisha  watanzania kuvifahamu vifutio vya utalii.
 
Alisema kuwa zoezi hilo la upandaji mlima litahusissha baadhi ya viongozi mashuhuri  wa jeshi awastaafu akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi ili kuhamasisha watanzania waweze kupanda mlima ambapo tukio hilo litajulikana kama Uhuru Epedition .
 
Kijazi alifafanua kuwa pamoja na kuadhimisha uhuru wa nchi ,lakini madhumuni mengine ya zoezi hilo ni kuhamasisha utalii na kuhimiza uhifadhi wa mazingira kwani bado watanzania wengi hawana muamko wa kutembelea vufutio vya utalii hivyo kujikuta asilimia kubwa ya watalii ni kutoka nje ya nchi.
 
“Katika maadhimisho haya tuna malengo ya kuhamasisha watanzania ili wajitokoze kupanda mlima kilimanajaro pamoja na kutembela hifadhi mbali mbaki kwani tunavyo vivutio 16 ambavyo vipo ndani ya tanzania na vinahitaji watanzania wote wanufaike navyo sio tu wageni kutoka nje ya nchi bali hata wa hapa wajue wanazo fursa “aliongeza kijazi.
 
Kwa upande wake mkurugenzi wa zara Zainabu Ansell alisema kuwa watanzania wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kihistoria kwani  wengi wao wamekuwa na mawazo potofu ya kufikiria wanaopaswa kupanda mlima na kutembelea hifadhi ni wazungu tu na wageni kutoka nje ya nchi hali inayowafanya watanzania kupoteza haki yao.
 
Kauli mbiu ya zoezi la kupanda mlima kilimanjaro mwaka huu ni endelea kuweka mazingira safi na salama ya fahari ya afrika.

RIDHIWANI – WENYE MAAMBUKIZI YA UKIMWI WASIJINYANYAPAE

Posted by Esta Malibiche on Dec2,2016 in NEWS
img_7115
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WATU wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi wameaswa kuacha kujinyanyapaa ama kukata tamaa na badala yake wahakikishe wanajilinda na kuepuka maambukizi mapya ya ukimwi.
Aidha wametakiwa kutumia madawa ya kufubaza makali ya virusi vya ukimwi ARVs kiuhakika.
Rai hiyo imetolewa na mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, huko Mdaula, wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi dunia katika kituo cha kupima na kutoa elimu juu ya masuala ya ugonjwa wa ukimwi.
Alisema kuwa watu wengi wanaopima na kujikuta na maambukizi hukata tamaa na wengine kuamua hata kujidhuru.
Ridhiwani aliwapa moyo wasijinyanyapae bali wafuate maelekezo ya wataalumu ili kukinga maambukizi mapya.
Hata hivyo alisema pia ni wajibu wa jamii kuwaheshimu,kuwapa ushirikiano na kuwasaidia inapobidi ili nao wajione ni sehemu muhimu katika jamii.
Ridhiwani alitoa wito kwa wananchi jimboni humo kupiga vita maambukizi mapya ya ukimwi kwa kujilinda na kuwa waaminifu katika mahusiano yao .
“Jukumu la kujilinda ni la watu wote, tuachane na matamanio ambayo mwisho wake ni majuto “” alisema Ridhiwani.
Mbunge huyo alitumia maadhimisho hayo kuungana na wananchi wa Mdaula na baadhi ya wananchi jimbo la Chalinze kupima afya yake.
Katika maadhimisho hayo watu 81 walijitokeza kupima afya zao ambapo watu watatu kati yao waligundulika kuwa wana maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
Ridhiwani alianza ziara yake jimboni hapo yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kutolea majibu baadhi ya hatua ambazo zinachukuliwa katika baadhi ya kero ambapo alianza na kupima afya yake kwenye maadhimisho hayo.

KITISI FC MABINGWA SPANEST CUP 2016

Posted by Esta Malibiche on Dec 2,2016 in MICHEZO

KLABU ya Kitisi imeshinda Kombe la SPANEST linalodhaminiwa na Mradi wa Kuboresha Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania baada ya kuwashinda Kinyika FC kwa mikwaju ya penati 4-2.

Dakika 90 za mchezo huo uliopigwa katika uwanja maarufu wa Kimande Pawaga, Iringa Vijijini ulishuhudia wababe hao waliovuka vihunzi dhidi ya timu nyingine 22 zinazozunguka hifadhi ya Taifa ya Ruaha, wakitoka sara ya 1-1 mbele ya mashabiki waliokadiriwa kuwa zaidi ya 3,000.

Kwa ushindi huo, Kitisi FC iliondoka na kombe, medali za dhahabu, seti moja ya jezi, cheti na Sh Milioni moja taslimu huku wakiahidiwa kutembelea hifadhi ya Ruaha.

Watakapofanya ziara katika hifadhi hiyo, Kitisi FC watapata pia fursa ya kumenyana na timu kali ya waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa inayoundwa na wachezaji mahiri 20.

Pamoja na kwamba Kinyika FC waliokuwa na matumaini makubwa ya kutwaa kombe hilo baada ya kuongoza kwa muda mrefu katika dakika 90 za mchezo, kulizwa kwa mikwaju ya penati, wameondoka na medali za shaba, cheti, mipira miwili na Sh 700,000 taslimu.

Nafasi ya tatu ya ligi hiyo ilikwenda kwa Itunundu FC, waliofanikiwa kumlaza kwa mabao 3-2 Mapogolo FC ambao pia walipata zawadi mbalimbali kutoka kwa waandaji wa mashindano hayo ya kila mwaka yanayolenga kuwaokoa Tembo dhidi ya majangili.

Akikabidhi zawadi kwa washindi, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliahidi kusaidia kuyatafutiwa wadhamini zaidi kwa kuwa yana mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya majangili.

Mratibu wa SPANEST inayoratibu mashindano hayo, Godwell Ole Meing’ataki alisema fainali ya ligi hiyo inalenga kuoa Tembo kwa kupitia kauli mbiu yake ya “Piga Vita Ujangili, Piga Mpira Okoa Tembo.”
 

Meing’ataki alisema wazo la kuunganisha vijana katika vita ya ujangili linaonekana kuwa njia muafaka ya kutokomeza ujangili kutokana na ukweli kwamba vijana ndiyo walengwa wakubwa katika kushawishika kuingia kwenye maeneo yaliyohifadhiwa na kufanya ujangili.

Timu ya Kitisi Fc ndio mabingwa wa kombe La spanest 2016 baada ya kuifungwa kwa penati timu ya Kinyika FC leo  katika michezo wa fainali