Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumamosi, 27 Januari 2018

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KINONDONI CHAANDIKA HISTORIA MPYA UZINDUZI WA KAMPENI YA UBUNGE

Posted by Esta Malibiche on JAN 28,2018 IN SIASA


Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,katika viwanja vya Biafra Kinondoni jioni ya leo.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akiwasalimia wananchi mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza mambo mbalimbali mbele ya Wanachama wa chama hicho na Wananchi kwa ujumla mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akiwasalimia wananchi wa Kinondoni jioni ya leo alipokuwa akitambulishwa kwao na kurudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,pichani kati ni Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba na kulia kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Stephen Wasira
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akirudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akiitazama kadi hiyo kwa makini
Aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassaanal ambaye hivi karibuni alihamia CCM,akimwombea kura za ushindi Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni ,Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa watu waliofika kuhudhuria uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la uzinduzi wa kampeni Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Kinondoni,mapema leo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.

WAZIRI WA TAMISEMI SELEMAN JAFO AWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KILOSA NA KUIPONGEZA KAMATI YA MAAFA MKOANI MOROGORO

Posted by Esta Malibiche ON JAN 27,2018 IN NEWS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na waathirika wa mafuriko
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa mkoa wa morogoro Dk.Stephen Kebwe wakimtembelea mmoja wa waathirika wa mafuriko ambaye pia ni mlemavu ambaye kwasasa anaishi katika hema.

Baadhi ya madaraja yaliyosombwa na mafuriko wilayani Kilosa.

Wananchi wa Kilosa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu athari za mafuriko Kilosa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akikagua maeneo yaliyoathirika mafuriko.

.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuangalia maafa za mafuriko yaliyo tokea wilayani Kilosa.

     ..................................................................

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo ameipongeza kamati ya maafa ya mkoa morogoro na ya wilaya ya Kilosa kwa juhudi kubwa wanayo ifanya katika zoezi la kuwaokoa wananchi walikumbwa na mafuriko.

Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea wilayani Kilosa leo ili kujionea athari za mafuriko na kuwapa pole waathirika hao. 

Waziri Jafo amewahakikishia waathirika hao wa mafuriko kwamba serikali itajitahidi kufanya mambo ya msingi ili kunusuru maisha ya watu wote.

Amesema serikali itajitahidi kurekebisha miundombinu iliyoathirika ikiwemo barabara, madaraja, shule, Reli, vyanzo vya maji, na huduma mbalimbali za kijamii.  

Katika ukaguzi wake,Jafo amesema kutokana na eneo la tuta la kuzuia maji kubomoka pamoja na mfereji wa kuchepushia maji yaliyozidi ameagiza wataalam wa mradi wa mabadiliko ya tabia nchi wafanye tathmini ili kuona cha kufanya ili kuepusha maafa makubwa kwa siku za usoni kwa maeneo ya mji wa Kilosa na viunga vyake.

Kwasasa wanaendelea kuhamishiwa sehemu ya ukanda wa juu wa Kilosa ambapo serikali imeamua kutenga eneo maalum na kuwapimia viwanja bure ili wananchi wajenge makazi ya kudumu na kuachana na tabia ya kukaa maeneo hatarishi ya mabondeni. 

Aidha serikali kwa kushirikiana na  wadau mbalimbali  inaendelea kuwasaidia mahema, madawa, maji, na chakula ili kukidhi hali ya maisha. 

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUSIMAMIA FEDHA ZA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA AFYA

Posted by Esta Malibiche on JAN 27,2018 IN NEWS
Waziri Ummy akikagua ramani ya kituo cha afya kilichojengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Shirika la SEDA Foundation, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Subi na kushoto ni mmoja wa viongozi wa Shirika hilo.

Na.WAMJW,Mwanza

Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kusimamia Fedha za kuboresha huduma za dharura zinazotolewa na Serikali zitumike ipasavyo na si kwa matumizi mengine

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  jijini hapa wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za utoaji huduma za afya pamoja na ujenzi wa huduma za dharura za Uzazi kwenye kituo cha afya cha Karume kilichopo kata ya Igombe Wilayani Ilemela
Waziri Ummy alimpongeza Mkurugenzi wa Ilemela kwa matumizi mazuri ya fedha hizo ambapo alijionea kazi nzuri inayoendelea katika kituo hicho ambapo wametumia wajenzi wa kawaida na ujenzi huo unaenda vizuri na kwa kiwango kinachoridhisha

Aidha,alisema Fedha za kuboresha miundombinu ya huduma za uzazi wa dharura zitumike kama haya angalau kujengwe chumba cha upasuaji,maabara ya damu na tunamataka wodi ya wazazi na nyumba moja ya mtumishi kuliko kujenga masuala mengine
“kama fedha zitabaki unaweza kufikiri kujenga vitu vingine,kuliko kqenda kutumika kwa masuala mengine kama baadhi ya sehemu nyingine wanavyofanya, kama fedha zimebaki nipo tayari kukuruhusu kujenga kitu kingine Mkurugenzi,hongera sana Mkurugenzi na viongozi wengine”.

Hata hivyo alisema Tanzania ni moja ya nchi yenye vifo vingi vya akina mama wajawazito na watoto”leo hii toka saa sita usiku tuanze siku hadi saa sita usiku wanawake 30 wa kitanzania wanafariki kwa sababu tu ya kutimiza wajibu wao wa kuleta kiumbe duniani”
“Kwahiyo Mhe.Rais alichokifanya  kwa kushirikiana na wadau tunaboresha huduma za uzazi zikiwepo za upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni,hivyo tumefurahi kuona hapa zile zshilingi milioni mia tano zimetumika ipasavyo,binafsi nimedhirika  na kazi iliyofanywa hapa karume hivyo naahidi kuleta fedha kwa ajili ya   kuboresha miundombinu ya kituo cha afya Buzurugwa”alime Waziri Ummy

Wakati huo huo nae naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi na Mbunge wa Jimbo la Ilemele Dkt.Angela Mabula alisema wao kama viongozi watahakikisha fedha zote zitakazoenda kwa ajili ya afya itatumika ipasavyo na wataisimamia ili kuweza kuboresha miundombinu ya sekta ya afya

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amewataka wananchi wa    Igombe kuendeleza mshikamano wanaouonyesha ili kuendelea kufanya makubwa zaaidi kwa kujiletea maendeleo”mchakato wa maendeleo chini ya Jemedari wetu rais Magufunli ndo kwanza umeanza.

1 of 1,377 ZIARA YA NAIBU WAZIRI MASAUNI KUKAGUA MAKAZI YA ASKARI NA MAENEO YA POLISI WALIYOUZIWA WANANCHI KINYUME NA UTARATIBU MKOA WA KUSINI UNGUJA

Posted by Esta Malibiche on JAN 27,2018 IN NEWS
pix 1
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA (kushoto), alipotembelea eneo la Tunguu lililovamiwa na wananchi, ambalo mmiliki halali ni jeshi la Polisi. Wakwanza kulia ni  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja,Makarani Khamis  na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan.Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
pix 2
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Makarani Khamis , akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, juu ya eneo la Tunguu lililoko Mkoa wa Kusini Unguja  ambalo ni mali ya Jeshi la Polisi, hivi sasa likimilikiwa na wananchi kinyume cha sheria.Kushoto ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
pix 3
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyeshwa  na Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA, ramani ya moja ya maeneo yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa ziara ya naibu waziri kukagua maeneo yanayotarajiwa  kujengwa vituo vya polisi mkoani hapo.Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo,Hassan Khatib Hassan. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
pix 4
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua makazi ya askari polisi yanayoonekana pichani, yaliyopo eneo la Machui, lililopo Mkoa wa Kusini Unguja.Naibu Waziri yupo Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
pix 5
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua eneo yalipojengwa maduka ya biashara ambayo wamiliki wamenunua viwanja hivyo vya Jeshi la Polisi kinyume na utaratibu. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
pix 6
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Mkoa Kusini Unguja alipowasili leo  mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Ijumaa, 26 Januari 2018

RAIS MSTAAFU KIKWETE AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI

Posted by Esta Malibiche ON JAN 27,2018 IN NEWS
 Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete akifurahi kuona papai alililopelekewa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen) walipokwenda kumpa elimu kuhusu kilimo bora cha zao hilo nyumbani kwake Msoga, Chalinze mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange.
 Dk. Kikwete akishukuru kwa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mwanachama wa Mkikita  Mtaalamu wa Kilimo cha Papai kutoka Kampuni ya Awino Farm, Ezra Machogu. Kulia ni Adam NGAMANGE


Na Richard Mwaikenda, Msoga.

.RAIS mstaafu Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)

Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani  kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu  Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.

Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa wakati wa mauzo.

Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.

Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.

Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo kuweka majagi mawili badala ya debe moja.Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne.

Alisema kuwa pia wamejipanga kimasoko kwa kuutumia mtandao wa Mkikita ambao tayari una watalaam wa masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na watalaamu wa kufungasha (Packaging) bidhaa kwa teknolojia ya kisasa.

Baada ya kuridhika na maelezo hayo, Rais mstaafu, alifurahi na kuishukuru Mkikita kwa kumpelekea watalaam hao kutoka Kampuni ya Awino Farm.Ezra alizidi kumfurahisha, Dk. Kikwete kuwa kwa heka moja akiuza papai anaweza kupata hadi sh. mil. 80,000,000 kwa mchanganuo ufuatao; 

Heka moja inaweza kupandwa mipapai 1000 hadi 1200 na kwamba mpapai mmoja unaweza kuzaa papai 100 hadi 1300 na endapo kila papai lenye uzito wa kilo 2 likiuzwa kwa bei ya jumla sh. 800 ukizidisha na wastani wa papai 100 kila mche halafu zidisha kwa miche 1000 tu unapata kiasi hicho cha fedha kwa msimu wa kwanza.

Pia alimueleza kuwa uzuri wa miche ya papai huishi miaka mitatu ambapo kila wiki utakuwa unavuna na kuuza, hivyo kukupatia faida kubwa tofauti na mazao mengine ambayo ukivuna mara moja tu.

"Laiti kama ungekuwa mchungaji, padri au sheikh anayehubiri kutafuta waumini, basi bila shaka mimi mmenipata nimekuwa muumini wenu." Alisema Dk. Kikwete huku akicheka kwa furaha."Kubwa mlilonifurahisha ni jinsi mlivyopunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya kuzalisha papai 
na faida kubwa nitakayoipata, nipo tayari kutoa heka 10 za kuanzia."Aliahidi Dk. Kikwete ambaye alisema kazi ya kilimo anaipenda na kwamba iko kwenye damu yake. 

Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita Adam Ngamange, ambaye akabla y yote alimshukuru Dk. Kikwete kwa kuwaalika na kumuomba ajiunge na mtandao, jambo ambalo alilikubali.

Ujumbe alioongozana nao ni Ezra Machogu, Martine  Wamaya wa Kampuni ya Awino Farm, Khalid Tamim, Hassan Tamim na Ali Said ambao ni Wawekezaji wa zao la muhogo,  Mkurugenzi  Betl Worldwide Ltd, Murtaza Bharmal ambaye ni mtaalamu wa masoko na uongezaji thamani mazao na Richard Mwaikenda ambaye ni Mshauri wa Habari wa mtandao huo.
 Meneja  Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikwete, Justine (kushoto) akiwa na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino, Martine Wamaya (kulia) na Mtalaamu wa kilimo cha Papai,  Ezra Machogu walipokuwa wakitoka kuchuma papai kutoka kwenye shamba darasa la Kampuni ya Awino eneo la Msata tayari kumpelekea Rais mstaafu, Dk. Kikwete. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Dk. Kikwete akisalimiana na Adam Ngamange wa Mkikita
 Dk. Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Awino Farm, Wamaya.
 Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra
 Dk. Kikwete akisalimiana na wanachama wa Mkikita wawekezaji katika shamba la Muhogo. Kushoto ni Khalid Tamim na Hassan Tamim.
 Meneja wa Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikiwete, Justine akiutambulisha ujumbe wa Mkikita nyumbani kwa Kikwete, Msoga
 Ngamange akielezea mbele ya Dk Kikwete kuhusu utendaji wa mtandao huo
 Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra (kulia) akitoa elimu kwa Dk. Kikwete kuhusu kilimo bora cha zao hilo kwa gharama nafuu
 Ngamange akimkabihi Dk. Kikwete mafuta yaliyotengenezwa kwa kutumia mchaichai
 Dk. JK akinusa mafuta hayo ya mchaichai

 Dk. Kikwete akifungua kasha la mchaichai
 Mtaalamu wa Masoko na Ufungashaji wa bidhaa mshirika wa Mkikita, Murtaza Bharmal (kulia) akitoa maelezo jinsi anavyoweza kutafuta masoko kirahisi kwa kutengeneza makasha mazuri ya kuhifadhia bidhaa ili kuongeza thamani.
 J akiwa na ujumbe wa Mkikita pamoja maofisa wasaidizi wake
 Dk. Kikiwete akizungumza Ngamange (kulia) pamona na Murtaza
 JK akiagana na kiongozi wa ujumbe wa Mkikita, Ngamange baada ya ziara yao kumalizika

JK akiagana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Octor