Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumatatu, 27 Machi 2017

DKT. NCHIMBI AWAAGIZA WATENDAJI KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI MKOANI SINGIDA, AAHIDI KUWASHUGHULIKIA WASIOSIMAMIA.

Posted by Esta Malibiche on MARCH 27,2017 IN NEWS

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akijitwisha ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama ikiwa ni maadhimishi ya kilele cha wiki ya maji yaliyofanyika katika kijiji hicho cha Iguguno, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya Mkalama Injinia Jakson Masaka.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaagiza watendaji wa serikali kuanzia ngazi ya kitongoji hadi Mkoa kusimamia na kuwa walinzi wa kwanza wa miundombinu ya miradi yote inayotekelezwa na serikali pamoja na wahisani hasa miundombinu ya maji ambayo imekosa usimamizi wa kutosha.

Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji mara baada ya kusimamia makabidhiano ya mradi wa maji ulioibuliwa na halmashauri ya Iramba kabla ya kuundwa kwa halmashauri ya Mkalama ulipo mradi wa maji wa Iguguno wenye thamani ya shilingi milioni 847,099,550 na unahudumia watu elfu kumi.

Amesisitiza kuwa serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutengeneza miradi ya maji ili kuwapunguzia wananchi adha ya upatikanaji wa maji safi na salama ambapo miradi hiyo imekuwa haileti mafanikio yaliyotarajiwa kutokana na kukoa usimamizi wa kutosha.

“Naelekeza taarifa ya miradi yote ya maji iletwe ofisini kwangu, nataka nifahamu miradi ambayo imefikia lengo la kuwapatia wananachi maji na ile ambayo wananchi hawajaanza kunufaika kwa kupata maji safi na salama lakini fedha za umma zimetumika”, amesema Dokta Nchimbi. 

Aidha, Dkt. Nchimbi amewaaigiza watendaji wa vijiji na kata kusimamia na kutunza miundo mbinu mbalimbali ikiwemo ya maji katika maeneo yao huku akielekeza kuwa endapo uharibifu utatokea mtendaji aliyepo katika eneo husika atawajibishwa kwa uzembe. 

Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Nchimbi ametembelea chanzo cha maji cha Mwankoko kinachotoa maji katika halmashauri ya manispaa ya Singida na kisha kupanda miti ili kutunza mazingira na kuhifadhi chanzo hizo.

Akitoa taarifa ya chanzo hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (SUWASA) mjini Singida Hosea Maghimbi amesema zaidi ya shilingi bilioni 1.5 sawa na asilimia 99.2 kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/17 kwa ajili ya fidia kwa wakazi walio jirani na chanzo hicho.

Maghimbi amesema SUWASA iko katika ujenzi wa mradi wa mtandao wa maji na mfumo wa maji safi Singida mjini pamoja na kuboresha huduma ya maji kwa miji midogo ya Manyoni na Kiomboi.

Amesema baadhi ya changamoto zinazokabili SUWASA ni pamoja na wateja kutolipa madeni kwa wakati hasa taasisi za serikali, wateja wanaokatiwa huduma kwa sababu ya madeni kutorejeshewa huduma hizo na badala yake kununua maji kwa majirani, kujifungia maji na kuchepusha dira za maji.

Maghimbi ametoa wito kwa wananchi kutokata miti, kuchoma moto, kuchungia mifungo na kufanya shughuli zangine za binadamu kwenye vyanzo vya maji. 

“Nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi kufichua watu wanaojiunganishia maji kiholela, wanaojifungia maji na kuchepusha dira ya maji, kwamba SUWASA inatoa zawadi ya shillingi 50,000 kwa ye yote atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana na watu hao, ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria”, amesema Maghimbi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama Bi Joyce ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia baadhi ya wananchi wa kijiji cha Iguguno Wilaya ya Mkalama kwenye maadhimishio ya kilele cha wiki ya maji. Pamoja na mambo mengine Dkt. Nchimbi ameagiza askari wa usalama barabarani kupanda miti ya matunda ili waweze kula matunda kuboresha afya za macho yao waweze kuona vizuri kipindi wanatekeleza majukumu yao barabarani.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 27,2017

Posted by Esta Malibiche on MARCH 27,2017

ZANTEL YAZINDUA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI WA 4G NA HUDUMA ZA KIBENKI KWA NJIA YA SIMU KISIWANI PEMBA

Posted by Esta Malibiche on MARCH 27,2017

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said wakipongezana mara baada ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na benki hiyo kwa wananchi wa kisiwani Pemba. Katikati ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada (wa tatu kushoto) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili kushoto), Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha (kushoto) na Meneja wa Benki ya watu wa Zanzibar-Pemba Mohamed Musa (kulia) mara baada ya kuzindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua rasmi mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa wananchi wa kisiwani Pemba. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said wakizindua huduma za mtandao wenye kasi zaidi wa 4G wa Zantel na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na Benki hiyo kisiwani Pemba. Wanaoshughudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (kushoto) na Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba. 

Kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL imezindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G sambamba na huduma za kibenki zinazozingatia kanuni za kiislamu kwa njia ya simu ikiwa ni hatua ya kuboresha na kupanua huduma zake kwa wateja.

Katika hatua ya kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya simu, Zantel imeshirikiana na BENKI ya watu wa Zanzibar (PBZ) katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma zote za kibenki kama vile kuweka au kutoa fedha, mikopo, kulipia ankara zao za huduma mbalimbali kama vile maji, umeme au kununua vocha za simu n.k.

Akizindua huduma hizo leo (23/03/2017) kisiwani Pemba, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada alisema huduma hizo kutoka Zantel zimekuja katika wakati muafaka kwa wananchi wa Pemba na kuongeza kuwa yeye na Wizara yake wanaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na mitandao mingine ya simu katika kuhakikisha huduma za simu zinaboreshwa zaidi visiwani humo.

“Uzinduzi wa huduma ya mtandao wenye kasi zaidi wa 4G sambamba na huduma ya kibenki kwa njia ya simu ni vitu ambavyo wananchi wa Pemba wamekua wakivisubiria kwa muda mrefu. Niipongeze Kampuni ya mawasiliano ya Zantel kwa kulitambua jambo hili na kulifanyia kazi kwa haraka” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin amesema uzinduzi wa huduma hizo mpya ni moja kati ya jitihada zinazofanywa na kampuni yake katika kutoa huduma zenye ubora nchini ili kutimiza mahitaji mbalimbali ya wateja wao.

Aliongeza kuwa huduma ya kibenki kwa njia ya simu za mkononi imewalenga watu wote ila zaidi ikiwa ni jamii ya kiislamu kwani inazingatia kanuni na misingi yote ya kiislamu wakati wa utoaji wa huduma.

“Pamoja na kurahishisha huduma za kibenki huduma kwa njia ya simu, huduma hii pia itasaidia kuokoa muda, ni huduma rafiki kwa kila mtu na yenye usalama mkubwa” alisema Benoit.

Kwa mujibu wa Taarifa za Benki kuu ya Tanzania (BoT) ni kuwa watumiaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mikononi wamefanya miamala yenye thamani ya bilioni 988.9 katika kipindi cha pili cha mwaka jana,huku mitandao ya simu ikigeuka kuwa njia muhimu katika miamala ya malipo mbalimbali.

Janin aliendelea kuwahakikishia wateja wa Zantel kuwa kampuni ya Zantel imekuwa katika ushindani kwa muda mrefu na kuwa bado wanaendelea kuwekeza ili kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora zaidi kwa kiwango kikubwa na teknolojia bora zaidi

“Tutaendelea kufikisha huduma hizi kwenda sehemu mbalimbali za hapa nchini, huu ni mwanzo tu kwa wateja wa Zantel ningependa wategemee mambo mazuri zaidi”.

Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Zantel, inaongoza kwa asilimia 80 kwenye soko la mitando ya simu kwa Zanzibar na ndiyo kampuni ya kwanza kutambulisha huduma za kibenki kwa njia ya simu hapa nchini.

Ni hivi karibuni tu ambapo, Zantel kwa kushirikiana na Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) walizindua huduma mpya ya “Zantel Madrasa” inayolenga kutoa mafundisho ya dini na kuwaunganisha wadau wa dini hiyo kujifunza zaidi juu ya uislamu kwa kupitia simu zao za mikononi au kujipatia jumbe mbalimbali na mawaidha ya kiislamu kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15586.

Alhamisi, 23 Machi 2017

KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI YA UMMA YATEMBELEA MIRADI YA KITUO CHA KIMATAIFA CHA MIKUTANO ICC

Posted by Esta Malibiche on march 23,2017 in NEWS

 Mkurugenzi miliki na miradi wa miradi wa kituo cha mikutano cha AICC Victoria Kamagenge akiwa anawaonyesha kamati Ya uwekezaji wa mitaji yauma  PAC moja ya mradi unaojegwa na kituo cha mikutano cha AICC  jijini Arusha mradi unaogarimu kiasi cha shilingi bilioni 2.8

 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC) wakiwa wanateta jambo

 Wakiendelea kukagua
 Mbunge wa jimbo la  Bunda mjini   Ester Bulaya akiwa
anakula na wakandarasi wa jengo jipya la maonyesho linalojengwa na kituo
cha mikutano cha AICC wakati walipofanya ziara na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC) wakiwa katika picha ya pamoja
Na Woinde Shizza,,Arusha

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC)
imeyataka mashirika ya umma 265 yalilopo hapa nchini, kuanza kujiandaa
kuchangia bajeti ya  serikali kuanzia
mwaka ujao wa fedha .

Aidha wakurugenzi na wenyeviti wa bodi wa mashirika
hayo kuanzia mwakani  watatakiwa  kuwasilisha bajeti zao bungeni ili kuweza
kupitishwa na bunge na hakuna shirika lolote la serikali litakaloweza kupiitishwa  bajeti bila kuithinishwa  na bunge.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti  wa kamati hiyo  ,Albart Obama Mtabaliba mbunge wa jimbo la
Buhigwe, mkoani Kigoma, wakati kamati hiyo ilipotembelea miradi ya kituo cha
kimataifa cha mikutano (AICC)nakujionea miradi mbalimbali inayoendeshwa na
kituo hicho ikiwemo ujenzi wa nyumba za kupangisha ,hosp italpamoja na jengo la
maonyesho na mikutano linaloendelea kujengwa na kituo hicho.

Alisema kuwa  licha ya mashirika hayo kuwa na thamani kubwa ya
shilingi trilioni 26 lakini yamekuwa hayachangii ipasavyo bajeti ya serikali
,hivyo yanatakiwa  yabadilike na kuanza
kulipa kodi ipasavyo pamoja na kutoa gawio serikalini.

‘’Mashirika yote ya umma yaliyopo hapa nchini
yanadhamani ya shilingi trilioni 26 na kwa mwaka yamekuwa yakitoa faida ya
shilingi bilioni 450 pekee ,ambayo ni sawa na asilimia 1.08% kitu ambacho hakiwezekani
ukilinganisha na mtaji uliopo wa trilioni 26
,na hivyo wakurugenzi na wenyeviti wa bodi wametakiwa wahakikishe mapato
yao kwa serikali yanapanda na angalau weweze kuchangia trilioni mbili kwa mwaka
“alisema Mtabaliba

Akizunguzia kituo  cha mikutano cha kimataifa  AICC alipongeza miradi inayoendeshwa na kituo
hicho na kushauri  waanze kuchukuwa hatua
ya kuanza kukabiliana na soko na pia wajitahidi kuwekeza zaidi katika ujenzi wa
vituo vya mikutano vya kisasa ,na kuwataka kuelekeza nguvu zaidi ya kujenga
kituo kikubwa cha mikutano katika mji mkuu wa Tanzania  ambapo ni Dodoma.

Hata hivyo mmoja wa  wabunge wa  kamati hiyo,Ester Bulaya alikosoa  gharama za ukarabati zilizotumika kukarabati
ukumbi wa Simba hall  uliopo katika kituo
hicho ambapo kiasi cha shilingi bilioni tatu na nusu zilitumika jambo ambalo
hawakuafiki na kushauri kwamba fedha hizo ninyingi sana na zingeweza kutumika
kwenye uwekezaji mwingine .

Naye mkurugenzi mtendaji  wa AICC
Elishilia Kaaya  alisema kuwa
amefurahishwa  na ujio wa kamati hiyo
kuwatembelea  na pia wamekutana nao na
wamepewa elimu nzuri ya uwekezaji na wametaza baadhi ya  mambo yale ambayo ayajaenda sawa
wamewarekebisha pale ambapo awapo vyema wamewafundisha hivyo wanaamini  walivyoambiwa mtazamo ubadili utabadilika
kulingana na hali ilivyo.

Hata hivyo alisema kwa sasa wameanzisha mradi
ujenzi wa kumbi za mikutano,mahoteli na maonyesho  unaogarimu kiasi cha shilingi shilingi bilioni
2.8,mradi ambao unatarajiwa kukamilika mapema May 4 ambapo wanategemea
utasaidia kuongeza mapato ya kituo hicho pamoja na ajira kwa watanzania.

Mhe. Samia Suluhu Hassan Leo amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati Bw. Sunil Kaushal

Posted by Esta Malibiche on march 23,2017 inNEWS

MAKA1
Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati  Bw. Sunil Kaushal pamoja na ujumbe wake uliomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
MAKA2
Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  na Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati  Bw. Sunil Kaushal ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
MAKA3 MAKA4