Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumanne, 29 Novemba 2016

RC GAMBO ATOA PIKIPIKI 200 KWA WANDESHA BODA BODA -ARUSHA


Posted by Esta Malibiche on Nov 29,2016 in NEWS
 boy4
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (aliyesimama) akiongea na madereva wa boda boda kuwaelezea mpango wa Serikali wa kuwapatia Pikipiki 200.

boy2
Baadhi ya waendesha boda boda wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
boy3
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Polycarp Nkuyumba(aliyesimama) akiwakaribisha viongozi na wadau kwenye Kikao na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.

boy5
Lucas Malusu ni dereva wa boda boda Kutoka Kata ya Elerai (aliyesimama katikati) akitoa maoni yake katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
boy6
Serafini Shirima(aliyesimama) ni dereva wa boda boda kutoka Kata ya Levolosi akichangia uanzishwaji wa umoja wa wandesha boda boda Wilaya ya Arusha (UBOJA)
boy7
Viongozi wa mpito waliochanguliwa kusimamia taratibu za uanzishjwaji wa Umoja huo pamoja na utoaji wa Pikipiki wa vijana nane wa Kila Kata.
boy8
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akihitimisha kikao chake na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.
Nteghenjwa Hosseah
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amekutana na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha na kuwajulisha kuhusu mpango wa Serikali wa kuwakwamua kiuchumi kwa kuwawezesha kupata Pikipiki bila Riba wala dhamana.
Rc Gambo amekuja na Mpango huu wa Kuinua uchumi wa Vijana kwa kuwapatia Pikipiki  baada ya kukutana na kundi hili la waendesha boda boda  kwa mara na kusikiliza malalamiko yao huku miongoni mwa kero yao kubwa ni kutozwa fedha nyingi na wamiliki wa boda boda hizo.
 
Akiongea na waendesha boda boda Rc Gambo alisema ninaona jinsi mnavyojituma katika kujitafutia riziki lakini hamthaminiki na kazi hii imekua ikidharaulika, sasa  muda umefika kwa  kazi hii kuwa ya heshima mbele ya Jamii, kila kijana aliyepo katika biashara hii ataweza kumiliki Pikipiki yake na sio kuendesha Pikipiki za watu ambao wamekuwa wakiwanyonya kila siku kwa kuwatoza Fedha nyingi na wao kuzidi kuneemeka wakati ninyi mnazidi kuwa masikini.
 
“Kundi hili limekuwa likitumiwa kwa maslahi ya watu wachache kwa kuwa wamekuwa wakipewa Pikipiki hizo kwa faidi kubwa na mmiliki anapokea Fedha zaidi yya mara mbili ya bei ya kununulia Pikipiki hiyo ndipo aamue kummilikisha kijana pikipiki hiyo au aamue kuendelea kupokea Fedha kwa kipindi chote wakati ninyi mnapata tabu barabarani huko na mnaambulia Fedha kidogo kiasi ambacho hamuwezi fikia hatua ya kumiliki Pikipiki zenu” Alisema Gambo.
 
Aliongeza kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imeona ni vyema ikawajengea uwezo vijana waliopo katika kazi hii kwa kuwapa mafunzo na kuwapatia Pikipiki ambazo mtatakiwa kurejesha kiasi cha Fedha halali iliyonunuliwa Pikipiki hiyo kisha kumilikishwa chombo bila ya riba yeyote wala dhamana.
Aliendelea kusema utoaji wa Pikipiki hizi utazingatia Kata zote zilizopo katika Jiji la Arusha ili Pikipiki ziweze kuwafikia walengwa na zoezi hili litaendelea kwa vijana wengine kadiri ya mahitaji; Tutaongeza usimamizi kwa wote watakaopata Pikipiki hizi ili waweze kurejesha  Fedha  kama inavyotakiwa na tuweze kuwanunulia vijana wengine hatimaye tuwafikie vijana wote wenye uhitaji wa kumiliki na kufanya biashara ya bodaboda.
Serafini  Shirima ni dereva wa boda boda Kata ya Levolosi akizungumza katika Kikao hicho alisema kwa mara ya kwanza Katika Mkoa huu wamepata mlezi anayetambua na kuthamini kazi ya boda boda na aliyethubutu kuwatafutia Pikipiki za bei nafuu ili kuongeza kipato cha vijana wa Arusha.
Shirima alishauri kuundwa kwa kamati ya mpito itakayosimamia na kuratibu mchakato mzima wa vijana watakaoanza kupewa Pikipiki hizo na kukamilisha taratibu zote za uanzishaji wa umoja wa wandesha Boda boda utakaofahamika kwa jina la (UBOJA) chini ya Mlezi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Gambo.
RC Gambo alikamilisha Kikao hicho kwa kusimamia uchaguzi wa viongozi wa mpito kutoka katika Kila Kata na hatimaye kupatikana viongozi watano watakaoratibu mpango wa awali wa utoaji wa Pikipiki kwa vijana.
Pikipiki zitakazotolewa katika awamu ya kwanza ni 200 zikiwa na  thamani ya Tsh Mil 400 na zitatolewa sanjari na Bima kubwa(Comprehensive Insurance) kwa vijana 200 ambapo kila Kata itatakiwa kutoa vijana 8.
Vijana wa Arusha watakabidhiwa Pikipiki hizi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa   tarehe 03/12/2016 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Jumatatu, 28 Novemba 2016

WAZIRI LWENGE ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MABOMBA NCHINI

Posted by Esta Malibiche on Nov 29,2016 in TEKNOLOJIA
kilu1
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiangalia aina ya bomba lililotumika kwenye mradi wa Ruvu Chini na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh (kulia)  pamoja na Meneja Biashara, Ryan Koh.
kilu2
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye karakana ya kiwanda hicho.
kilu3
Mafundi wakiwa kazini katika karakana ya Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited.
kilu4
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh na kujionea moja ya mabomba yanayotengenezwa na kiwanda hicho.
……………………………………………………..
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge mwishoni mwa wiki alitembelea Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP) kilichopo Shekilango, Dar es Salaam.

Kiwanda hicho kinachotengeneza mabomba ya maji, ambayo pia yanatumika katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, ukiwemo mradi ya maji ya Ruvu Chini, KASHWASA na Ruvuma.
“Nimeridhishwa na uwekezaji wa kiwanda hiki cha mabomba, ambacho kina uwezo wa kuzalisha mabomba yenye ubora wa kutekeleza miradi yetu ya maji nchini”.

“Hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuinua uchumi wa viwanda nchini, hivyo maendeleo ya kiwanda hiki ni hatua nzuri ya kufikia lengo hilo”, alisema Waziri Lwenge.

Inj. Lwenge alisema uwezo ilionao kiwanda hiki ni chachu ya maendeleo kwa Sekta ya Maji na Umwagiliaji kwani kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikununua mabomba kutoka nje ya nchi, na hata yanayotengenezwa hapa mengi ni ya plastiki ambayo hayadumu muda mrefu ukilinganisha na ya chuma.

Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP)  alisema nia yao kubwa ni kutengeneza bidhaa nzuri zenye ubora wa kimataifa na kushindana katika soko la kimataifa, na kuiomba Serikali itumie bidhaa za wawekezaji wa ndani zenye ubora wa hali ya juu.

Alisisitiza bidhaa zao zinatengenezwa hapa nchini tangu hatua ya awali na wala si kuagizwa kutoka nje, zina uwezo wa kudumu mpaka miaka 50, zinatumika nje ya nchi ikiwemo Rwanda, ambapo zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maji.

Dhumuni la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea uwezo wa kiwanda hicho kwa upande wa uzalishaji na ubora wa bidhaa zao.

RAIS DKT.MAGUFULI AMWANDALIA RAIS EDGAR LUNGU DHIFA YA KITAIFA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Posted by Esta Malibiche on Nov29,2016 in NEWS

 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili AlhajAli Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu kwa dhifa hiyo ya kitaifa aliyomwandalia mgeni wake Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Meza kuu ikiwa imesimama kwa Wimbo wa Taifa
 Rais Dkt Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia kusalimiana na viongozi mbalimbali
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akisherehesha hafla hiyo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akigonganisha glasi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Wimbo wa Taifa 
 Viongozi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Zambia ukipigwa
 Viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na Mkuu wa Itifaki wa Zambia wakiwa wamesimama kwa wimbo wa Taifa 
 Sehemu ya Mawaziri waliohudhuria wakiwa wamesimama
 Viongozi wakiwa wamesimama
 Makatibu wakuu na sehemu ya ujumbe wa Zambia
 Wageni waalikwa na viongozi wa vyama vya siasa
 Baadhi ya mabalozi mbalimbali waliohudhuria
 Wageni mbalimbali
 Mabalozi mbalimbali
 Mabalozi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje 
 Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali
  Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali na maafisa wa Wizara ya Mambo ya nje
 Viongozi wa taasisi mbalimbali
 Viongozi wa kidini na wageni mbalimbali
 Makatibu wakuu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace Mujuma
 
 Mrisho Mpoto na Banana Zorro na Mjomba band akitumbuiza
 Mrisho Mpoto akighani wimbo maalumu
 Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi 
 Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi 
 Rais Edgar Lungu akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein
 Rais Edgar Lungu akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Rais Edgar Lungu akisindikizwa na mweyeji wake Rais Dkt Magufuli
 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakiondoka baada ya dhifa
Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu Dkt.  Jakaya Mrisho kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakifurahia jambo mara baada ya dhifa hiyo ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es salaam.
 PICHA NA IKULU