Alhamisi, 7 Aprili 2016

JK AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ITALY LEO

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) katika mgogoro wa Libya, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete leo amekutana na Naibu  Waziri wa Mambo ya nje wa Italy Dk. Mario Giro, katika Ofisi Ndogo ya  Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo maalum.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo, Msaidizi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Suleyman Mwenda alisema, Dk. Kikwete amekuwa na mahusiano ya kirafiki ya muda mrefu na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italy Dk. Mario Giro, hivyo Naibu Waziri huyo amefanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya kumjulia hali kama rafiki yake wa muda mrefu.
“Pamoja na kuja kumsalimia kama rafiki wa siku nyingi, lakini lengo hasa la Naibu waziri huyo ni kutaka maelezo juu ya suala la Libya’ alisema Mwenda na kuongeza  “Kama mnavyofahamu kuwa Dk. Kikwete ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika (AU) kuwa mwakilishi katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa Libya”.
Alisema, Italy inalipa umuhimu wa kipekee suala la Libya kutokana na kwamba nchi hiyo  ni jirani hivyo ina maslahi mapana na ya karibu juu ya suala la amani ya Libya, Dk. Giro ameiwakilisha nchi yake katika kujua hatua ya usuluhishi na  hatma ya mgogoro wa Libya.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri huyo aliambatana na Balozi wa Italy hapa nchini, Luigi Scotto pamoja na Dk. Raffaele De Lutio, Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Italy.

SHIRIKA LA POSTA LAZINDUA HUDUMA MPYA YA POSTA MLANGONI JIJINI DAR ES SALAAM

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akimkabidhi Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, moja ya kifurushi kwa ajili ya kupelekwa kwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akimkabidhi Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, moja ya kifurushi kwa ajili ya kupelekwa kwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora (kushoto) na Mwakilishi wa Umoja wa Posta Barani Afrika (PAPU), Naibu Katibu Mkuu, Kola Aduloju (mwenye miwani kulia).
 
Juu na Chini: Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akimkabidhi moja ya kifurushi hicho, mfanyakazi wa Posta kwa ajili ya kukipeleka nyumbani kwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
 
Mwakilishi wa Umoja wa Posta Barani Afrika (PAPU), Naibu Katibu Mkuu, Kola Aduloju, akitoa hutuba yake katika uzinduzi wa huduma hiyo.
Meneja Msaidizi wa Biashara ya Barua, Jason Kalile akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akibonyeza kitufe cha kompyuta kwa ajili ya kuzindua rasmi huduma hiyo, huku akishuhudiwa na Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Maria Sasabo (katikati).
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akimkabidhi Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, moja ya kifurushi kwa ajili ya kupelekwa kwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
 
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akimkabidhi Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, moja ya kifurushi kwa ajili ya kupelekwa kwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora (kushoto) na Mwakilishi wa Umoja wa Posta Barani Afrika (PAPU), Naibu Katibu Mkuu, Kola Aduloju (mwenye miwani kulia).

0 maoni:

Chapisha Maoni